Katibu Mkuu wa Chama
cha Mapinduzi CCM ABDULRAHAMAN KINANA ameanza ziara yake ya siku 23 katika
Mikoa ya RUVUMA na MBEYA kwa kuanzia wilayani TUNDURU Mkoani RUVUMA ambako
amekutana na kero ya wananchi juu ya matatizo ya zao la Korosho na kuwahakikishia
kuwa Serikali ya CCM imeanza kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na
matatizo hayo.
KINANA ambaye
ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi NAPE NNAUYE na Katibu wa NEC,
Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dr ASHA-ROSE MIGIRO amesema Wizara husika na
tatizo la Korosho tayari zimeagizwa kuchukua hatua za haraka kutatua matatizo
ya Korosho na pia kunyang’anya viwanda vyote vya korosho ambavyo tangu
vibinafsishwe havibangui Korosho
Karibu kwa katibu Mkuu
wa CCM Komredi ABDULAHAMAN KINANA hapa
RUVUMA ilikua ni katika kijiji cha NAKAPANYA wilayani TUNDURU ambako yeye
pamoja na katibu wa NEC Itikadi na Uenezi NAPE NNAUYE na Katibu wa NEC Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa Dr ASHA-ROSE MIGIRO wamekaribishwa kwa kilio juu ya zao
la Korosho.
Kilio hiki kimetolewa
mara baada ya KINANA kuvalishwa vai la Jadi la na kutunukiwa cheo cha Heshima
kwa kabila la wayao cha SULTANI LINYAMA, na mvalishaji akatumia fursa hiyo
kutanabaisha kuwa wananchi wapo taabani kutokana zao wanalolitegemea
kuwaangusha
Majibu ya KINANA kwa
Kilio hiki yakawa tayari Kamati Kuu ya CCM imeziagiza wizara husika kutafuta
majibu haraka iwezekanavyo na kupeleka ripoti katika kikao kijacho cha Kamati
kuu ya CCM lakini akabainisha kuwa Mchezo unaofanywa na wanunuzi wa Korosho
hauipendezi CCM wala Serikali yake
No comments:
Post a Comment