Wakazi wa Mtaa wa MIEMBENI katika Manispaa ya SONGEA Mkoani RUVUMA wamejikuta katika hali ya taharuki iliyodumu kwa saa kadhaa baada ya Nyoka Mkubwa aina ya Chatu kuvamia eneo la makazi yao na kisha kumkamata kummeza na Mbwa mmoja aliyekua akimzuia chatu huyo kuingia katika nyumba.
Hata hivyo hivyo mmiliki wa Nyumba hiyo Bwana BEDA PATRICK alijitoa mhanga kupambana na chatu hiyo kwa kumkata na panga na hivyo akamtema mbwa aliyemmeza.
Urefu wa Nyoka huyu aina ya Chatu ni futi 12.5, haijulikanani ni wakati gani alipovamia makazi ya watu wa eneo la MIEMBENI hapa katika Manispaa ya SONGEA.
Taharuki iliyotawala mapema tu kulipopambazuka ikawakusanya wakazi wa eneo la MIEMBENI kushuhudia joka hatari sio tu kwa mifugo bali pia kwa binadamu, hasa waliposhuhudia mbwa mkubwa aliyemezwa mwili mzima akiwa ametemwa baada ya joka hili kukutana na ushujaa wa mwenye mbwa BEDA PATRICK
Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa MIEMBENI wameiomba manispaa ya SONGEA kufyeka kichaka kilichopo jirani na eneo la makazi ya watu, huku wakisema licha ya kumuua chatu huyo pia kuna kenge wakubwa ambako hukamata mifugo na ni hatari kwa watu hasa watoto
Eneo la Miembeni lipo jirani na hifadhi ya LUHILA ambayo ina nyoka wengi, na mara kadhaa nyoka wamekua wakivamia makazi ya watu na kukamata mifugo hasa kuku huku wakisababisha hofu kubwa kwa watu
No comments:
Post a Comment