Hili ni sanduku lililowekwa masalia ya Mtumishi wa Mungu Sista Bernadeta Mbawala katika kanisa la jimbo kuu katoliki la Songea Mkoani Ruvuma ambaye 14.1.2013 jimbo lilifunga mchakato wa kumtangaza mwenyeheri kwa kuadhimisha misa takatifu na kusafirsha taarifa zake zilizokusanywa na mahakama ya mchakato.
Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki Mhashamu Norbert Mtega akitoa wito kwa watanzania kuchangia mchakto wa kumtangaza sista Bernadeta kuwa Mwenyeheri. na baadaye mtakatifu.
Maandamano yakielekea ndani ya kanisa kwa ajili ya kuadhimisha misa ya mchakato huo.
Masista wakiwa wameshika picha ya sista Bernadeta Mbawala
Masista wakiimba katika misa takatifu ya mchakato huo.
Hao ni mapadre wa kanisa katoliki la Songea wakiwa ndani ya kanisa
Hili ni sanduku lililowekwa masalia ya Mtumishi wa Mungu sista Bernadeta Mbawala.
Jimbo
kuu katoliki la Songea leo limeadhimisha misa takatifu ya kufunga
mchakato wa kumtangaza sista BERNADETA MBAWALA OSB kuwa mwenye heri na
baadaye mtakatifu katika ngazi ya jimbo.
****************************
Akizungumza
na waumini wa jimbo katoliki la Songea Askofu mkuu wa jimbo la Songea
Mhashamu NORBERT MTEGA alisema jimbo kwa upande wake tayari
limeshafanya utafiti na kukusanya taarifa mabalimbali alizoziandika
sista Bernadelta Mbawala, ambapo wamepata barua alizoandika enzi za uhai
wake zaidi ya mia moja, na machapisho mbalimbali ya magazeti.
Pia
walipata sala alizotunga mwenyewe na kuzitumia kusali lakini kazi kubwa
ilikuwa ni kuhoji watu kadiri ya sheria za kanisa ambapo tayari
wamehoji watu 83, wakiwemo mapadre na watawa kutoka Songea na njombe.
Askofu
Mtega aliongeza kuwa kanisa sasa limechukua hatua ya kuanza kutafiti
na kuzungumza hadharani ili sista Bernadeta OSB aweze kupata heshima ya
kutangazwa mtakatifu.
Askofu
huyo wajimbo kuu katoliki la Songea Mhashamu Norbert Mtega katika
Mahubiri yake hayo alisema kama sista BERNADETA OSB atafanikiwa
kutangazwa kuwa mtakatifu atakuwa ni mtanzania wa kwanza kufikia hatua
hiyo, na kuwaomba waumini waendelee kuomba ili mchakato huo ufanikiwe.
Alisema
baada ya kumaliza mchakato huo wa ngazi ya jimbo kinachosubiliwa sasa
ni kutokea kwa miujiza miwili na miujiza hiyo itokee popote duniani,
ukitokea muujiza kwanza basi sista Bernaderta atatangazwa kuwa mwenye
heri na ukitokea muujiza wa pili atatangazwa kuwa mtakatifu.
Askofu
alitumia nafasi hiyo kuwaomba watanzania kuchangia kwa hali na mali
zoezi hili la mchakato kwa kuwa kunahitajika zaidi ya dola 20,000/= ili
uweze kukamilika.
Aidha
Askofu Mtega alimuelezea Sista Bernadeta OSB Kuwa alizaliwa mnamo
mwaka 27/10/1911 katika kijiji cha likuyufisi wakati huo kwa sasa ni
manispaa ya Songea, wazazi wake ni Stefan Msikazonge na Agata Mayanda,
alibatizwa 5/11/1911 peramiho, kipaimara alipata tarehe 8.12.1921
peramiho, na alijiunga na utawa 7.08.1929 peramiho, Nadhiri za kwanza
alipata 11.11.1934 wakati huo hakukuwa na nadhiri za daima na alikufa
ta29.11.1950.
Sista
Bernadeta Mbawala OSB kutoka nyumba ya mtakatifu Agnes ya chipole
maisha yake na wazazi wake yalikuwa ni ya sala na kuabudu sana na
alikuwa anatokewa na moyo mtakatifu wa yesu n aalikuwa anazungumza sana
na bikira maria na mtakatifu Agnes,
Aliugua
sana lakini aliunganisha mateso yake nay a yesu kristu na hakuwahi
kutamka kutafuta dawa za mitishamba, alitolea mateso yake kwa kuwaombea
wakosefu na hivyo amewafundisha wakristu kuyapokea mateso kwa imani kwa
kuwa mateso ni moja ya sala na sadaka.
Baada
ya kufa kwake miaka 61 baadaye kanisa limeshuhudia watu wakienda
kusali katika kaburi lake na kufanikiwa mambo yao huku hakuna kiongozii
wa dini aliyeagiza watu wafanye hivyo huo ni ushuhuda kuwa sista
BERNADETA anafaa kuwa mtakatifu.
Kazi
kubwa imefanywa na mahakama ya mchakato huo ya kuandaa taarifa za sista
Bernadeta ambazo taarifa hizo zimekamilika na Askofu mtega ametia saini
na kugonga muhuri tayari kwa kusafirishwa kwenda ROMA kwa mchakato
zaidi.
Naye
padre CAMILIUS HAULE naibu wa askofu aliyemwakilisha askofu katika
kufanya kazi kwenye Mahakama ya mchakato huo akiwa ni mtetezi wa haki
ametoa tamko .nanukuu hakuna kitu chochote cha kutiliwa shaka kati ya
yale yote yaliyokusanywa na mahakama ya mchakato na ndio yatamkwe hivyo.
Kwa
upande wake waziri wan chi ofisi ya makamu wa Rais mazingira dokta
terezya huvisa ametoa ushuhuda mbele ya waumini kuwa amekuwa akiomba
katika kaburi la sista Bernadeta na kupata mafanikio ikiwa pamoja na
uongozi na ametoa mchango wa shilingi milioni mbili kwa ajili ya mchakto
na ujenzi wa kanisa la lizaboni katika manispaa ya songea.
Taarifa
za sista bernadeta ndio zinazosafirishwa kwenda ROMA kwa ajili ya
kuendelea na mchakato zaidi lakini Masalia ya mwili wake yamebaki katika
sanduku la mbao katika kanisa la jimbo kuu katoliki la songea kwa wale
wote wanaohitaji kusali katika masalia hayo wanaalikwa.
No comments:
Post a Comment