ZAIDI
ya Wafanyakazi 45 wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Mkoni Ruvuma wamenusulika
kufa baada ya Basi lenye namba za usajiri T 966 AXQ mali ya kampuni ta
Ng’itu Expres walilokuwa wakisafiria kupinduka.
Sambamba
na tukio la ajali hiyo taarifa zinaeleza kuwa watu wane (4) wamejeruhiwa
kutokana na kuumia sehemu mbalimbali za miili yao kukimbizwa katika Hospitali ya serikali ya
Wilaya ya Tunduru.
Wakiongea
kwa njia ya simu baadhi ya manusula hao walisema kuwa ajali hiyo ilitokea
katika eneo la Lumesule mpakani mwa Wilaya zaTunduru Mkoni Ruvuma na Mangaka
Mkoani Mtwara.
Kwamujibu
wa taariha hizo watumishi hao ambao walifuatana na wakuu wao wa idara walikuwa
wana kwenda Wilayani Masasi Mkoani Mtwara kwa ajili ya kushirki katika Mazishi
ya aliyekuwa Mkurugenzi wa hamalshauri yao Marehem Robert Nehatta.
Akifafanua
taarifa za tukio hilo Dkt. Jacob Madondola ambaye ni kati ya manusula hao
alieleza kuwa mbali na gari hilo kuwa katika mwendo kasi chanzo cha ajali hiyo
kilisababishwa na kuchomoka kwa Stelingi na kumshinda dereva.
Katika
taarifa hiyo mashuhuda hao waliwataja watu waliojeruhiwa kaatika ajali hiyo
kuwa ni Bw. John Kamwela (afisa Biashara wa Halmashauri hiyo), Bi. Malisela
Mapunda(afisa manunuzi wa halamsahauri hiyo), Mwl. Joseph Makina ( msaidizi wa
afisa elimu wa Shule za Sekondani Wilayani humo) pamoja na Bw.Joseph Mtauchila
(Mkaguzi wa ndani).
Mganga
mfawidhi katika Hospitali ya Wilaya Dkt. Joseph Ng’ombo amekiri kuwapokea majeruhi
hao na kuwapatia matibabu na kwamba halizao zinaendelea vizuri.
Akizungumzia
tukio hilo kwa njia ya Simu, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw. Chande Nalicho ametoa pole kwa wahanga hao alisema kuwa
ajali hiyo imetokea katika mazingira ya uzembe wa wamiriki wa gari hilo
kutolifanyia uchunguzi wa kina wa mara kwa mara.
Alisema
Maremu Robert Nehatta alifariki Dinua usiku wa kuamkia Agost 26 mwaka huu akiwa
katika Hospitali nchini India ambako alienda kwa ajili ya matibabu ya Figo
yaliyokuwa yakimsumbua.
No comments:
Post a Comment