Sunday, 31 August 2014

WAKAZI WA TUNDURU WAHIMIZWA KUSHIKAMANA BILA KUJALI ITIKADI ZA DINI ZAO ILI KUJILETEA MAENDELEO.







CHAMA cha mapinduzi Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma kimewataka waumini wa Dini kuachana na tabia za kubaguana kutokana na tofauti hizo na badala yake waunganishe nguvu zao bila kujali uwepo wa itikadi za dini zao ili kuendana sawa na maandiko ya vitabu vitakatifu.

Wito huo umetolewa na Mjumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) wilayani humo Sheikh Ajili Kalolo wakati akiongea katika uzinduzi wa Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya itakayo milikiwa na waumini wa Dini ya kiislamu ya Islamiki High School na kwamba mbali na tofauti za dini ya kiislam na kikristo, vitabu vyake havizungumzii kubaguana.

Sheikh Kalolo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo alisema kuwa  vitendo na tabia za utengano na ubaguzi ni adui mkubwa ambaye anarudisha nyuma hatua za maendeleo zinazo dhamiliwa kufanywa na taasisi au jamii yoyote kote duniani.

Aidha Sheikh Kalolo aliwaomba watu na taasisi mbalimbali kujitoa katika kusaidia ujenzi wa shule hiyo na kuifanya ianze kutoa huduma iliyodhamiliwa kufanywa kwa wakati na kuwawezesha vijana kusoma elimu dunia na elimu ya dini na akatumia anafasi hiyo kuwapongea wahisani waliokubali kuijengea taasisi hiyo jengo la utawala, na darasa moja.

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa Shule hiyo yenye kidato cha kwanza hadi cha sita, Ustadh Maulid Juma alisema kuwa kwa awamu ya kwanza ujenzi wa shule hiyo umepanga kughalimu jumla ya Shilingi Milioni 350 na kwamab fedha hizo zinatarajiwa kutokana na michango ya waumini wa dini hiyo. 
  
Alisema kwa kuanzia tayari waumini hao wemefanikisha kuchangia fedha ambazo zimeisaidia taasisi hiyo kumiliki na kupimiwa eneo la ardhi lenye ukubwa wa hekta 30, kukusanya vifaa mbalimbali vilivyo pangwa kutumika katika ujenzi huo na kufatua tofari zaidi ya laki Tatu.

Akitoa ufafanuzi baada ya taarifa hiyo katibu wa Ujenzi wa shule hiyo Sheikh Mohammed Chingwalo alisema kuwa kamati yake imepanga kuanza na ujenzi wa Madarasa Matatu, Nyumba mbili za Walimu pamoja, jengo la Utawala na Mabweni mawili hali ambayo itawezesha shule hiyo kuanza kufanya kazi kwa kusajiri wanafunzi kuanzia mhura wa masomo mwaka 2016/2017. 

Alisema katika kuhakikisha kuwa ujenzi huo ujenzi huo umepangwa kukalika mwaka 2019 ambapo shule hiyo itaanza kuchukua wanfunzi wa kidato cha tano na sita katika mikondo miwili ya masomo ya Sanaa na Sayansi.

Wakiongea kwanyakati tofauti mwenyekiti wa Baraza la waislamu Tanzania Wilayani humo Shekhe Ndawambe Salum, mwakirishi wa maustadh Sheikh Husein Mahusein pamoja na mwakirishi wa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Sheikh Athuman Nkinde pamoja na mambo mengine waliwahimiza waumini wa dini hiyo kuunganisha nguvu zao ili kuharakisha ujenzi wa shule hiyo.

‘’ ili kuiwezesha shule yetu kuyafikia mafanikio na kuiwezesha kuanza kutoa huduma kwa haraka inafaa tupendane,  tuunganganishe nguvu zetu bila kujali itikadi za imani wa dini zetu” alisisitiza Shekih Ndawambe.

Akitoa taarifa za maendeleo ya elimu Wilayani humo mwakilishi wa mafisa elimu wa Shule za msingi na Sekondari Mwl. Abudul Kazembe pamoja na kuwapongeza kwa juhudi za ujenzi wa shule hiyo aliwataka wazazi na walezi wa watoto kuondokana na tabia ya kuwakataza watoto wao kwenda shule pamoja na mazuwio ya kuwakataza kunya zizuri katika matokeo ya mitihani yao yakumaliza darasa la saba .

Mwl. Kazembe aliwatahadharisha kuwa endapa hawata timuza wajibu wao katika kuhamasisha na kusiamaia maendeleo ya elimu ipo hatari ya juhudi hizo kutozaa matunda kwani baada ya kukamilika kwa majengo hayo hawataweza kuwapata wananfunzi wenye sifa za kwanda kusoma katika shule yao. 

IMEANDIKWA NA STEVEN AUGUSTINO - TUNDURU



No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO