Sunday, 27 October 2013
CHAMA CHA WALIMU KANDA YA KUSINI CHA MPONGEZA MKUU WA WILAYA YA TUNDURU.
Na STEVEN AUGUSTINO TUNDURU
UMOJA wa Vyama vya walimu Tazania (CWT) kanda ya Kusini
inayoihusisha Mikoa ya Ruvuma,Mtwara na Lindi
(UWARUMLI)kilichofanyika katika ukumbio wa Klasta ya walimu mlingoti
Wilayani Tundsuru wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Chande
Nalicho kwa uamuzi wake wa kushika chaki na kufundisha Somo la
Hisabati Katika Shule ya sekondari ya Mataka.
Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa Mkutano huo, Mwenyekiti wa
(CWT) Mkoa wa Lindi Mwl. Mlami Seba wakati akifungua Mkutano mkuu wa
Kawada wa wajumbe wa Umoja huo katika kanda ya Kusini inayoihusisha
Mikoa ya Ruvuma,Mtwara na Lindi (UWARUMLI) na kuongeza kuwa Mkuuwa
Wilaya huyo ni Wakutolewa mfano kutokana na kuwa na moyo wa pekee.
Mwl. Seba aliendelea kufafanua kuwa Dc, Nalicho anapaswa kutolewa
mfano kutokana na kuwa na upendo nan i mwana taaluma wa kweli kwa
madai kuwa kwani wapo Viongozi wengi ambao baada ya kuchaguliwa ama
kuteuliwa kushika nyadhifa zingine huacha kuzifanyia kazi taaluma
walizozisomea kwa madai ya kuwa na kazi nyingi za Kitaifa.
Mwl. Seba aliyasena hayo muda mfupi baada ya Kamati ya Walimu
waliokwenda kutembela Shule ya Mataka Sekondari kwa lengo la
kusikiliza Kero mbali mbali kutoka kwa walimu wa shule hiyo ambao
pamoja na mambo menginen walidai kushtushwa na kitendo cha kumukuta
Mkuu wa Wilaya hiyo akiwafundisha Wanafunzi wa Kidato cha Nne
wanaotarajiwa kufanya Mtihani wa taifa wa kidato mwanzoni mwa mwezi
November mwaka huu.
Dc, Chande Nalicho aliahidi kuingia Darasani na kuanza kufundisha Somo
la Hisabati topck ya Acaunts ambayo kila mtihani wa taifa hutoa swali
moja ambalo lina Point 10 kama mchango wake kwa kwa kuanza na
wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya kutwa ya Mataka .
Dc, Nalicho alisema kuwa ameamua kujitoa kama mwana taaluma ili
kupunguza ikama ya upungufu wa wafanyakazi wa idara ya Elimu ili
kujionea hali hali ya utendaji kazi wa Walimu anaodaiwa kulegalega na
kusababisha Wilaya yake kufanya vibaya katika matokeo ya wanafuzi
waliofanya mtihani wa kumaliza daraza la saba mwaka 2012.
Mwisho
WAFANYAKAZI WA TBC SONGEA WAKIFANYA USAFI KATIKA ENEO LA OFISI YA BOMBAMBILI
Mkuu wa kanda Hannah Mayige
Aliyekuwa juu ya ngazi ni Mhasibu Xavery Kapinga
Anayefagia ni Fundi Mitambo Meckzedeck Kikoti
Shehan Mzania mlinzi
Kulia ni Yusuph Mhango fundi mitambo
PACRAS MHAGAMA
Catherine Nyoni
Da cathy pendeza wewe.
Saturday, 26 October 2013
HALI ILIVYOKUWA KATIKA MKUTANO WA WANACHI WA JIMBO LA PERAMIHO NA MBUNGE WAO JENISTER MHAGAMA
VIONGOZI WA KINGONI WAKIMKABIDHI SILAHA ZA JADI WAKIMTAKA MBUNGE JENISTER AKOMAE NA WAPINZANI.
NGOMA YA ASILI YA KINGONI LIGIU
LIZOMBE
Friday, 25 October 2013
Mbunge
wa Jimbo la SOngea MJini Dkt Emmanuel Nchimbi (CCM) na Diwani wa Songea
Mjini Joseph Fuime (CHADEMA ) wakipokea maswali na hoja mbalimbali toka
kwa wananchi kwenye mkutano wa Hadhala eneo la Mahenge C kata ya Songea
Mjini Leo.mbunge yupo ziara ya kusikia toka kwa wananchi Kabla ya kikao
Cha bunge wiki Ijayo
Mbunge wa Jimbo la SOngea MJini Dkt Emmanuel Nchimbi (CCM) na Diwani wa Songea Mjini Joseph Fuime (CHADEMA ) wakipokea maswali na hoja mbalimbali toka kwa wananchi kwenye mkutano wa Hadhala eneo la Mahenge C kata ya Songea Mjini Leo.mbunge yupo ziara ya kusikia toka kwa wananchi Kabla ya kikao Cha bunge wiki Ijayo
Wednesday, 23 October 2013
TANGAZO
HYTES the organization I'm representing in Tanzania, has opened its application for Secondary School scholarships. We pay average of Shs. 300,000 per student covering tuition fee, exam fees, books and supplies.
Most
of Government school students can benefit alot as the tuition fee
ranges to Shs. 20,000. So Shs. 300,000 will cover at least every thing.
Kindly
ask as many as students from Songea Boys, Mletele, Ruhuwiko, and other
students from secondary schools in Songea to see attached application,
complete the forms and submitt them to me via my e-mail before the
deadline of 1st November 2013.
Sunday, 20 October 2013
HABARI ZA KUSIKITISHA MTANGAZAJI WA ZAMANI WA RADIO TANZANIA WAKATI ULE JULIUS NYAISANGA AFARIKI DUNIA HUKO MOROGORO.
Thursday, 17 October 2013
WACHEZAJI HAWA HATARI SANA WAKIKAMATA MPIRA WAKIWA KATIKKATI YA UWANJA UJUE NYAVU ITATIKISIKA TU
Wa kwanza kushoto anapiga chenga mpka golini aliyekuwa katikati mzee wa mashuti makali sana kipa huwa haoni mpira wake aliyeshika mpira mbaya wa kona akipiga kona haigusi mtu hadi wavuni.
Wa kwanza kushoto ni ISSA RASHIDI wa katikati ni GERSON MSIGWA na ALIYESHIKA Mpira ni FLORIAN MSIGWA.
Wa kwanza kushoto ni ISSA RASHIDI wa katikati ni GERSON MSIGWA na ALIYESHIKA Mpira ni FLORIAN MSIGWA.
Monday, 14 October 2013
KILELE CHA MBIO ZA MWENGE MKOANI IRINGA
Rais Jakaya Kikwete akiwa amekabidhiwa rasmi mwenge wa Uhuru leo baada ya kuhitimisha mbio zake nchini
Rais Kikwete akiwa ameushika mwenge wa Uhuru leo uwanja wa samora Iringa
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa mbio za mwenge kikanda na jumla leo
Rais Jakaya Kikwete akipokea mwenge kwa ajili ya kupiga picha ya pamoja na washindi wa mbio hizo kikanda
Sunday, 13 October 2013
Na Mhaiki Andrew, Songea
TIMU ya soka ya Majimaji Fc ya Songea juzi imeziduka na kuichapa Polisi Moro bao 1-0 katika mchezo
wa ligi ya Taifa ya Daraja la kwanza, mechi hiyo ilifanyika kwenye uwanja wa
Majimaji mjini hapa.
Mchezo huo ambao
ulikuwa muhimu kwa Wanalizombe kuweza kurudisha matumaini na imani kwa wapenzi,
mashabiki na wanachama wao kutokana na kuanza kwa ligi hiyo kwa kusuasua na
kupelekea kupoteza mechi mbili na moja kutoka sare na Kimondo ya Mbeya.
Majimaji ambayo
ilianza mchezo huo kwa kasi kwa kulisakama kwa kulishambulia lango la wapinzani wao ambao walionekana
kucheza kwa kujiamini zaidi, tofauti na mchezo wao uliopita na Mlale JKT ambapo maafande hao wa Polisi
Moro waliibuka na ushindi wa bao 1-0
ugenini.
Katika mchezo huo
Majimaji waliweza kuwatoa kimasomaso
wapenzi, mashabiki na wanachama wao
katika dakika ya 43 na Sayuni Mtunjilwa baada ya kutokea piga ni kupige langoni
mwa maafande hao ambao wanamatumani makubwa ya kurudi tena kucheza ligi kuu ya
Bara, baada ya msimu uliopita wa ligi hiyo waliweza walishuka Daraja.
Kuingia kwa bao
hilo maafande hao wa Polisi Moro walionekana kupagawa na kuanza kucheza rafu
ambazo ziliweza kuthibitiwa na mwamuzi wa mchezo huo, Rashid Ndanje wa kutoka
Dar es Salaam pamoja na kuendelea kucheza kwa kujiamini wakiamini watasawazisha
bao hilo na kupachika jingine la ushindi na kujizolea pointi zote tatu na
kujiweka katika mazingira mazuri ya kurudi tena kucheza ligi kuu msimu ujao.
Polisi Moro hasira
zao hazikuweza kuishia uwanjani ambapo uongozi wa timu hiyo akiwemo, Fikiri
Hussein waliweza kumshambulia kwa kumpiga na kumjeruhi usoni, mmoja wa viongozi
wa kamati tendaji ya chama cha mpira katika Manispaa ya Songea(SUFA), Francis
Kasembe”Farao” wakati zikiwa zimesalia dakika 2 kumalizika kwa mpambano huo.
Ilidaiwa na baadhi
ya watazamaji wa mchezo huo kuwa kiongozi huo, Kasembe alivamiwa na kuanza
kushambulia wakati akipita kukusanya mipira kutoka kwa vijana ambao wanaookotea
mpira kwa kuhofia isije kupotea punde mwamuzi wa mchezo huo atakapopuliza
filimbi yake ya mwisho wa kumaliza mchezo huo na kubaki kuwashangaza watazamaji
kwa hatua ambayo waliochukua maafande hao.
WABUNGE wa Wilaya ya Tunduru, Alhaji Mtutura Mtutura wa Jimbo la
Tunduru Kusini na Eng. Ramo Makani wa Tunduru kaskazini wamesema kuwa
wapo tayari kuachia nafasi zao za uwakilishi endapo wanachi wa majimbo
hayo hawata kuwa ridhaa kuwachagua katika Uchaguzi mkuu ujao.
Wabunge hao waliweka wazi dhamila yao hiyo wakati wakiongea na
wananchi katika Mkutano wao wa pamoja walioufanya katika viwanja vya
Baraza la idd mjini hapa na kubainisha kuwa kinacho umiza vichwa vyao na
kuwavyima ushingizi ni kufikilia jinsi gani wataweza kutatua kero za
wananchi katika kipindi hiki wanachotekeleza wajibu wakuwatumikia
kutokana na ridhaa waliyopewa mwaka 2010.
Kufuatia hali hiyo wabunge hao waliwataka Wazee ambao wanao watu wenye
uwezo wa kuongoza katika Majimbo hayo kujiandaa kwa kuwaita ili
waende kupambana nao katika mchakato wa Uchaguzi mkuu ujao na
wakiwashinda wataa waachia nafasi hizo na wao kufanya kazi nyingine
zikiwemo Biashara na hata Kulima.
“ choko choko zote za chinichini mnazotufanyia tuazifahamu na
kwa tarifa yenu sisi hatuogopi kuachia nafasi za uwakilishi
mlizotupatia kwa ridhaa yenu mwaka 2010”, walisema Wabungea hao na
kuongeza kuwa mkitaka waandaeni watoto na ndugu zenu waje tupambane
wakato wa mchakato wa kuwania kuwania nafasi zetu na endapo
watatushinda tutawaachia bila kivyongo.
“
mimi ni Mkulima mzuri wa mpunga, kila mwaka ninalima Ekari 100 na
hadi sasa ninazo Gunia 250 za mpunga, mwenzangu Eng. Ramo anafanya PHD
muda wowote ataitwa Dokta na hivyo hatakosa kazi endapo ataomba sehemu
yoyote” alifafanua mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini na kuongewza kuwa
kwa maandalizi hayo hawataishi maisha magumu hata wakinyimwa nafasi
tulizo.
Mkutano huo ulio onekana kujaa vijembe,kejeri na maneono ya kihuni
uliitishwa na Wabunge hao kwa nia ya kutoa ufafanuzi juu ya kuzagaa
kwa maneneno ya uongo, propaganda kejeri nyingi kuwa Wabunge hao ndio
kikwazo cha Wilayaa yao kugawanywa katika maeneo matatu ya utawala na
kwamba wamekuwa wakifanya hivyo kwavile hawana uchungu na maendeleo ya
Wilaya yao kwavile siyo wazawa wa wilaya hiyo.
Huku wakishangiliwa na makundi ya mamia yua watu waliohudhulia mkutano
huo Wabunge hao waliwaeleza Wananchi hao kuwa pamoja na kejeri zao
wasidhani kuwa wao hawana watu kabisa, na kwamba wao hawayasikii
manaeno na mipango yao mibaya ambayo wamekuwa wakikaa na kuipanga juu
yao bali wamekuwa wakikaa kimya kama wajinga lakini wakiwa wanajua
kila kinachoendelea juu yao kila uchao na kuongeza kwa kuwataka
wasiwatenge bila sababu za msingi.
Wakifafanua utaratibu uliotumika kwa ajili ya kuomba mgawanyo wa
Wilaya yao na kuomba Mkoa, walisema kuwa kabla ya Ujio wa Ziara ya
Wairi Mkuu wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda waliwaita
baadhi ya Wazee na Viongozi wa Kimila na kufanya nao vikao na kuweka
mikakati hiyo ambayo baada ya kuiwakilisha kwa kiongozi huyo alilidhia
na kushauri wafanye vikao vya kuanda utaratibu mzuri wa kuigawa Wilaya
yao katika maeneo mawili ya utawala ili waweze kuungana na wenzao wa
Wilaya ya Namtumbo ili kuunda Mkoa huo mpya.
Waliendelea kufafanua kuwa katika mapendekezo yao hayo wote
walizingatia kuwa Wilaya ya Tunduru ambayo kwa sasa inayo Majimbo
mawili ya uchaguzi ya Tunduru Kusini na Tunduru Kaskazini yanao wakazi
298,274 kwa mujibu wa Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012,inalo
eneo la utawala lenye ukubwa wa Kilometa za mraba 18,778 ,Tarafa
7,Kata 35,Vijiji 148 na Vitongoji 1,015 na kwamba hali hiyo pia ndiyo
iyowasukuma hata wataalamu kutoa mapendekezo ya ainahiyo.
Aidha waliwataka wananchi hao wasiwahukumu eti kwavile tu wao pia ni
wajumbe wa kamati za ushauri (DCC) kilichotoa mapendekezo ya kuigawa
Wilaya hiyo katika maeneo mawili ya Utawala na kupingana na
mapendekezo ya Baraza la madiwani ambalo lilitoa mapendekezo ya
mgawavyo wa Wilaya tatu na badala yake wawaelimishe Watoto wao
wawafahamishe madhara ya kugoma kuhesabiwa katika sense ya Watu na
makzi itakayofanyika miaka 10 ijayo .
Aidha Wabunge hao pia wakafafanua kuwa kupitia mgawanyo Wilaya mbili
inaopendekezwa kuundwa na Jimbo la Uchaguzi la Tunduru Kasikazini
utakuwa na tarafa 4, Kata 21 Vijiji 86, utakuwa na eneo lenye ukubwa
wa kilometa za mraba 11,425, wakazi 163,447 kati yao wanaume ni
78,915 sawa na asilimia 48.28% ya wakazi hao na wanawake ni 84,532
sawa na asilimia 51.72 ya wakazi hao, hii ni kwamujibu wa sense ya
watu na makazi 2012
Walisema upande wa Jimbu la uchaguzi wa Tunduru Kusini litakuwa na
tarafa 3, Kata 14 Vijiji 62 ,ukubwa wa eneo la Mraba 7,353 itakuwa na
wakazi 134,832 wakiwemo wanawake 70,087sawa na asilimia 51.9% ya
wakazi hao na wanaume 64,745 sawa na asilimia 48.01% ya wakazi hao
hii ni kwamujibu wa sense ya watu na makazi ya mwaka 2012.
Wakizungumzia upande mgawavyo wa mapendekezo yaliyotolewa na Baraza la
madiwani na yanayo onekana kuungwa mkono na kundi kubwa la watu wanao
jita Wazawa wa Wilaya hiyo Wilaya Tatu walisema kuwa Wilaya mpya
inayopendekezwa kundwa na Tarafa za Matemanga na Nampungu itakuwa na
Ukubwa wa eneo ni kilometa za mraba 6,339, wakazi 57,984, Kata 8, na
Vijiji 32, Wilaya mpya inayopendekezwa kuundwa Tarafa Lukumbule na
Nalasi ikuwa na eneo la kilometa za mraba 5,706, idadi ya wakazi
itakuwa 96,311, Tarafa 2 ,kata 9, na Vijiji42 na kwa upande wa Wilaya
mpya inayoundwa na tarafa za Mlingoti, Nakapanya na Namasakata
itakuwa na Tarafa 3 kata 18 vijiji 74. inao wakazi 143, 984.
Walisema mgawanyo huo unaodaiwa kuzingatia Vigezo vya ukubwa wa eneo
la sasa kuitawala,jigrafia na mtandao mgumu na ubovu wa miundombinu ya
mawasiliano na barabara, kwamujibu wa sharia Namba 12 ya mwaka 1994
ya uanzishaji wa Mikoa na wilaya Mapendekezo hayo yanakosa baadhi ya
vigezo vya Kitaifa vinavyoelekeza kuwa kila Wilaya inapaswa kuwa na
idadi ya tarafa 5, kata zisizopungua 15 Vijiji 50, na idadi ya wakazi
wasipungua 100,000 uononekana kukosa vigezo vingi vikiwemo vigezo
vikubwa vya matumizi ya takwimu zinazozungumzia Idadi ya watu,Vijiji,
Kata na tarafa zilizopo Wilayani humo.
Mwisho
HABARI ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE ZINASEMA MTANGAZAJI WA ITV UFOO SARO AMEPIGWA RISASI NA KUJERUHIWA NA MAMA YAKE KAPIGWA RISASI NA KUFARIKI HAPO HAPO.
Monday, 7 October 2013
HAWA NDIYO WASHIRIKI WA NNE WATAKAO IWAKILISHA TANZANIA KATIKA TUSKER PROJECT FAME..!!!
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 07. 10. 2013.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA MICHE YA BHANGI.
MNAMO
TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO ENEO LA UYOLE JIJI NA
MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA JULIUS S/O
MWAMBENJE, MIAKA 23, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA NSALAGA- UYOLE AKIWA NA
BHANGI MISOKOTO 15 SAWA NA UZITO WA GRAM 75. MBINU NI KUFICHA BHANGI
HIYO KWENYE MFUKO WA RAMBO. MTUHUMIWA NI MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA
JAMII KUACHA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA
NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUINGIA NCHINI BILA KIBALI
MNAMO
TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 23:30HRS HUKO ENEO LA STENDI KUU JIJI
NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA 1. NYELAKOZI
D/O MELANIA, MIAKA 33,,MKULIMA, NA 2. NDAISHIMILI D/O TEONYA,MIAKA
33,WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI BURUNDI WAKIWA NA WATOTO 11 AMBAO PIA
NI RAIA WA BURUNDI WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. MBINU NI
KUSAFIRI KWA NJIA YA KIFICHO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAKABIDHIWE IDARA
YA UHAMIAJI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA
KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI
PAMOJA NA WAHAMIAJI HARAMU ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]
MNAMO
TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 08:30HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA
MAJENGO KIJIJI CHA LUPA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI
WAKIWA DORIA WALIMKAMATA LYIDIA D/O AMBAKISYE, MIAKA 25, KYUSA,
MKULIMA, MKAZI WA LUPA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] UJAZO WA
LITA 5. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI
AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA
MATUMIZI YA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA
NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
MNAMO
TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 09:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA
MAGUNGA KIJIJI CHA MAMBA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI
WAKIWA DORIA WALIMKAMATA JOHN S/O LUTIMBO, MIAKA 29, MSUKUMA, MKULIMA,
MKAZI WA MAMBA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 4.
MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA
POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI
KWA AFYA YA MTUMIAJI.
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
Subscribe to:
Posts (Atom)