Thursday, 3 October 2013

WAZEE WA WILAYA YA TUNDURU WAILALAMIKIA HALMASHAURI YAO INAKWAMISHA MAENDELEO YAO.

                                          PICHA SIO YA ENEO LA TUKIO
                                                                  
                                          


Na Steven Augustino, Tunduru

Halmashauria ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma imelaumiwa kuwa imekuwa
ni kikwazo cha kuinua vipato vya Wazee na kuwafanya waendelee kuwa
tegemezi na kuwa omba omba  kwa watu wenye uwezo hali ambayo imekuwa
ikiwasababishia kupata manyanyaso.
 

Kero hiyo imebainishwa na Wazee kupitia Risala iliyosomwa katika
maadhimishao ya siku ya Wazee duniani iliyo adhimishwa katika ukumbi
wa Klasta ya walimu Milingoti Miji hapa na kuongeza kuwa hali hiyo
imetokana na halmashauri yao kushidwa kukamirisha ufungaji wa Mradi wa
mashine ya kukamulia Mafuta tangu mwaka 2005.
 

Katika kudhibitisha umuhimu wa mahitaji ya Mashini hizo Mstaafu wa
jeshi la Polisi Issa Kapopo na Condradi Ally Chikulo wakamweleza mkuu
wa Wilaya hiyo kuwa hadi hivi sasa wanashindwa kukamua mazao ya
alizeti waliyo yalima baada ya kuhamasishwa kuwa mashine hiyo ingeweza
kuwakomboa baada ya kuanza kufanya kazi hiyo ya kukamua mafuta.
 

Kero nyingine ambayo ilianishwa na Wazee hao kuwa ni pamoja na
halmashauri hiyo kushindwa kusimamia agizo la waziri Mkuu Mizengo
Pinda juu ya upatikanaji wa Matibabu bure kwa  Wazee hao.
 

 Kwamujibu wa taarifa hiyo ambayo ilisomwa na katibu wa umoja huo,
Mwalimu Mstaafu Salum Tabu alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2012/
2013 jumla ya wazee 360 wakiwemo wanawake 236 na wanaume 134
waliotibiwa katika mazingira magumu huku wengi wao wakitakiwa kwanda
kununua Dawa katika maduka ya madawa.
 

Akifafanua taarifa hiyo Katibu wa Chama cha Wazee na wastaafu Wilayani
humo Salum Tabu alisema kuwa Chama chao kinakabiliwa naa changamoto
kubwa ya kukosa fedha za kuwawezesha kuwafikia na kuwasajili Wazee
wenzeo katika
 

Aidha katika Risala hiyo pamoja na kukemea mmomonyoko wa maadili
unaoonekana kutawaliwa na kuiga tamaduni ya kimaghalibi pia Wazee
wakatumia nafasi hiyo kuwaonya wanaohatarisha amani ya nchi yetu kwa
kutumia miaamvuli ya dini na wakaitaka serikali kuwachukulia hatua
kali za kisheriaq ili kukomesha vitendo hivyo .
 

Akiongea na Wazee hao, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Chande Nalicho
pongeza kwa ubunifu wao wa kuanzisha kikundi cha uzalishaji mali na
akamuomba Mkurungenzi Mtendaji wa Halamsahauri ya Wilaya hiyo
kuvitambua vikundi vya wazee na kuangalia uwezekano wa kuwakopesha
mikopo yenye riba nafuu ili kuwakwamua katika matatizo yao ya
kimaisha.
 

 Alisema  kuwa serikali inatambua umuhimu wa kada hiyo ya Wazee ambao
wamekuwa ni hazi ya kutoa ushauri na busala katika matukio mbali mbali
huku akitumia semi za Wahenga kuwa “Ukiona Nyani amezeeka ujue
amekwepa mishale mingi”.
 

Alisema hivyo Wazee ni lasilima, nia hazi kubwa katika uendelezaji wa
Taifa  hili nakuongeza kuwa Wazee hao ndio walioitunza maliasili na
rasilimali amabzo kwa sasa zinaonekana  kuanza kutugombanisha
akawataka vijana kuiga mifano ya mambo mema na kufanya maandalizi ya
utunzaji wa maliasili.
 

Aidha aliwataka wazee kuwa wavumilivu wakati Serikali ikiendelea
kukamilisha mikakati yake kulingana na sera ya taifa ya wazee ya mwaka
2003 na kuhakikisha kuwa inafanya kazi.
 

 Dc, nalicho pia akamuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya
wilaya ya Tunduru kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa upatikanaji wa
kudumu katika ufuatiliaji wa upatika wa huduma ya bure kwa wazee wa
Wilaya hiyo ili kluondoa manung’uniko ambayo yamekuwa yakijitokeza.
 

Dc, Nalicho pia akatumia nafasi hiyo kuwapongeza Wazee hao kwa
utaratibu waliojiwekea wa kupeana Ng’ombe kila mwaka kupitia mpango wa
kopa ng’ombe Lipa Ng’ombe ambapo mwaka huu Mzee Idd Ausi Mpemba
alipokea Ndama kutoka kwa Bibi Catherine Komba.
 

Awali Mwenyekiti wa Chama cha Wazee na wastaafu Wilaya ya Tunduru (
CHAWATU) Said Ally Kabora sema kuwa maadhimisho hayo yatasaidia
kuikumbusha Serikali juu ya umuhimu wa kuwalipa pensheni kwa wazee
wote bila ubabuzi . 


 Mwisho

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO