WABUNGE wa Wilaya ya Tunduru, Alhaji Mtutura Mtutura wa Jimbo la
Tunduru Kusini na Eng. Ramo Makani wa Tunduru kaskazini wamesema kuwa
wapo tayari kuachia nafasi zao za uwakilishi endapo wanachi wa majimbo
hayo hawata kuwa ridhaa kuwachagua katika Uchaguzi mkuu ujao.
Wabunge hao waliweka wazi dhamila yao hiyo wakati wakiongea na
wananchi katika Mkutano wao wa pamoja walioufanya katika viwanja vya
Baraza la idd mjini hapa na kubainisha kuwa kinacho umiza vichwa vyao na
kuwavyima ushingizi ni kufikilia jinsi gani wataweza kutatua kero za
wananchi katika kipindi hiki wanachotekeleza wajibu wakuwatumikia
kutokana na ridhaa waliyopewa mwaka 2010.
Kufuatia hali hiyo wabunge hao waliwataka Wazee ambao wanao watu wenye
uwezo wa kuongoza katika Majimbo hayo kujiandaa kwa kuwaita ili
waende kupambana nao katika mchakato wa Uchaguzi mkuu ujao na
wakiwashinda wataa waachia nafasi hizo na wao kufanya kazi nyingine
zikiwemo Biashara na hata Kulima.
“ choko choko zote za chinichini mnazotufanyia tuazifahamu na
kwa tarifa yenu sisi hatuogopi kuachia nafasi za uwakilishi
mlizotupatia kwa ridhaa yenu mwaka 2010”, walisema Wabungea hao na
kuongeza kuwa mkitaka waandaeni watoto na ndugu zenu waje tupambane
wakato wa mchakato wa kuwania kuwania nafasi zetu na endapo
watatushinda tutawaachia bila kivyongo.
“
mimi ni Mkulima mzuri wa mpunga, kila mwaka ninalima Ekari 100 na
hadi sasa ninazo Gunia 250 za mpunga, mwenzangu Eng. Ramo anafanya PHD
muda wowote ataitwa Dokta na hivyo hatakosa kazi endapo ataomba sehemu
yoyote” alifafanua mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini na kuongewza kuwa
kwa maandalizi hayo hawataishi maisha magumu hata wakinyimwa nafasi
tulizo.
Mkutano huo ulio onekana kujaa vijembe,kejeri na maneono ya kihuni
uliitishwa na Wabunge hao kwa nia ya kutoa ufafanuzi juu ya kuzagaa
kwa maneneno ya uongo, propaganda kejeri nyingi kuwa Wabunge hao ndio
kikwazo cha Wilayaa yao kugawanywa katika maeneo matatu ya utawala na
kwamba wamekuwa wakifanya hivyo kwavile hawana uchungu na maendeleo ya
Wilaya yao kwavile siyo wazawa wa wilaya hiyo.
Huku wakishangiliwa na makundi ya mamia yua watu waliohudhulia mkutano
huo Wabunge hao waliwaeleza Wananchi hao kuwa pamoja na kejeri zao
wasidhani kuwa wao hawana watu kabisa, na kwamba wao hawayasikii
manaeno na mipango yao mibaya ambayo wamekuwa wakikaa na kuipanga juu
yao bali wamekuwa wakikaa kimya kama wajinga lakini wakiwa wanajua
kila kinachoendelea juu yao kila uchao na kuongeza kwa kuwataka
wasiwatenge bila sababu za msingi.
Wakifafanua utaratibu uliotumika kwa ajili ya kuomba mgawanyo wa
Wilaya yao na kuomba Mkoa, walisema kuwa kabla ya Ujio wa Ziara ya
Wairi Mkuu wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda waliwaita
baadhi ya Wazee na Viongozi wa Kimila na kufanya nao vikao na kuweka
mikakati hiyo ambayo baada ya kuiwakilisha kwa kiongozi huyo alilidhia
na kushauri wafanye vikao vya kuanda utaratibu mzuri wa kuigawa Wilaya
yao katika maeneo mawili ya utawala ili waweze kuungana na wenzao wa
Wilaya ya Namtumbo ili kuunda Mkoa huo mpya.
Waliendelea kufafanua kuwa katika mapendekezo yao hayo wote
walizingatia kuwa Wilaya ya Tunduru ambayo kwa sasa inayo Majimbo
mawili ya uchaguzi ya Tunduru Kusini na Tunduru Kaskazini yanao wakazi
298,274 kwa mujibu wa Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012,inalo
eneo la utawala lenye ukubwa wa Kilometa za mraba 18,778 ,Tarafa
7,Kata 35,Vijiji 148 na Vitongoji 1,015 na kwamba hali hiyo pia ndiyo
iyowasukuma hata wataalamu kutoa mapendekezo ya ainahiyo.
Aidha waliwataka wananchi hao wasiwahukumu eti kwavile tu wao pia ni
wajumbe wa kamati za ushauri (DCC) kilichotoa mapendekezo ya kuigawa
Wilaya hiyo katika maeneo mawili ya Utawala na kupingana na
mapendekezo ya Baraza la madiwani ambalo lilitoa mapendekezo ya
mgawavyo wa Wilaya tatu na badala yake wawaelimishe Watoto wao
wawafahamishe madhara ya kugoma kuhesabiwa katika sense ya Watu na
makzi itakayofanyika miaka 10 ijayo .
Aidha Wabunge hao pia wakafafanua kuwa kupitia mgawanyo Wilaya mbili
inaopendekezwa kuundwa na Jimbo la Uchaguzi la Tunduru Kasikazini
utakuwa na tarafa 4, Kata 21 Vijiji 86, utakuwa na eneo lenye ukubwa
wa kilometa za mraba 11,425, wakazi 163,447 kati yao wanaume ni
78,915 sawa na asilimia 48.28% ya wakazi hao na wanawake ni 84,532
sawa na asilimia 51.72 ya wakazi hao, hii ni kwamujibu wa sense ya
watu na makazi 2012
Walisema upande wa Jimbu la uchaguzi wa Tunduru Kusini litakuwa na
tarafa 3, Kata 14 Vijiji 62 ,ukubwa wa eneo la Mraba 7,353 itakuwa na
wakazi 134,832 wakiwemo wanawake 70,087sawa na asilimia 51.9% ya
wakazi hao na wanaume 64,745 sawa na asilimia 48.01% ya wakazi hao
hii ni kwamujibu wa sense ya watu na makazi ya mwaka 2012.
Wakizungumzia upande mgawavyo wa mapendekezo yaliyotolewa na Baraza la
madiwani na yanayo onekana kuungwa mkono na kundi kubwa la watu wanao
jita Wazawa wa Wilaya hiyo Wilaya Tatu walisema kuwa Wilaya mpya
inayopendekezwa kundwa na Tarafa za Matemanga na Nampungu itakuwa na
Ukubwa wa eneo ni kilometa za mraba 6,339, wakazi 57,984, Kata 8, na
Vijiji 32, Wilaya mpya inayopendekezwa kuundwa Tarafa Lukumbule na
Nalasi ikuwa na eneo la kilometa za mraba 5,706, idadi ya wakazi
itakuwa 96,311, Tarafa 2 ,kata 9, na Vijiji42 na kwa upande wa Wilaya
mpya inayoundwa na tarafa za Mlingoti, Nakapanya na Namasakata
itakuwa na Tarafa 3 kata 18 vijiji 74. inao wakazi 143, 984.
Walisema mgawanyo huo unaodaiwa kuzingatia Vigezo vya ukubwa wa eneo
la sasa kuitawala,jigrafia na mtandao mgumu na ubovu wa miundombinu ya
mawasiliano na barabara, kwamujibu wa sharia Namba 12 ya mwaka 1994
ya uanzishaji wa Mikoa na wilaya Mapendekezo hayo yanakosa baadhi ya
vigezo vya Kitaifa vinavyoelekeza kuwa kila Wilaya inapaswa kuwa na
idadi ya tarafa 5, kata zisizopungua 15 Vijiji 50, na idadi ya wakazi
wasipungua 100,000 uononekana kukosa vigezo vingi vikiwemo vigezo
vikubwa vya matumizi ya takwimu zinazozungumzia Idadi ya watu,Vijiji,
Kata na tarafa zilizopo Wilayani humo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment