Na Mhaiki Andrew, Songea
TIMU ya soka ya Majimaji Fc ya Songea juzi imeziduka na kuichapa Polisi Moro bao 1-0 katika mchezo
wa ligi ya Taifa ya Daraja la kwanza, mechi hiyo ilifanyika kwenye uwanja wa
Majimaji mjini hapa.
Mchezo huo ambao
ulikuwa muhimu kwa Wanalizombe kuweza kurudisha matumaini na imani kwa wapenzi,
mashabiki na wanachama wao kutokana na kuanza kwa ligi hiyo kwa kusuasua na
kupelekea kupoteza mechi mbili na moja kutoka sare na Kimondo ya Mbeya.
Majimaji ambayo
ilianza mchezo huo kwa kasi kwa kulisakama kwa kulishambulia lango la wapinzani wao ambao walionekana
kucheza kwa kujiamini zaidi, tofauti na mchezo wao uliopita na Mlale JKT ambapo maafande hao wa Polisi
Moro waliibuka na ushindi wa bao 1-0
ugenini.
Katika mchezo huo
Majimaji waliweza kuwatoa kimasomaso
wapenzi, mashabiki na wanachama wao
katika dakika ya 43 na Sayuni Mtunjilwa baada ya kutokea piga ni kupige langoni
mwa maafande hao ambao wanamatumani makubwa ya kurudi tena kucheza ligi kuu ya
Bara, baada ya msimu uliopita wa ligi hiyo waliweza walishuka Daraja.
Kuingia kwa bao
hilo maafande hao wa Polisi Moro walionekana kupagawa na kuanza kucheza rafu
ambazo ziliweza kuthibitiwa na mwamuzi wa mchezo huo, Rashid Ndanje wa kutoka
Dar es Salaam pamoja na kuendelea kucheza kwa kujiamini wakiamini watasawazisha
bao hilo na kupachika jingine la ushindi na kujizolea pointi zote tatu na
kujiweka katika mazingira mazuri ya kurudi tena kucheza ligi kuu msimu ujao.
Polisi Moro hasira
zao hazikuweza kuishia uwanjani ambapo uongozi wa timu hiyo akiwemo, Fikiri
Hussein waliweza kumshambulia kwa kumpiga na kumjeruhi usoni, mmoja wa viongozi
wa kamati tendaji ya chama cha mpira katika Manispaa ya Songea(SUFA), Francis
Kasembe”Farao” wakati zikiwa zimesalia dakika 2 kumalizika kwa mpambano huo.
Ilidaiwa na baadhi
ya watazamaji wa mchezo huo kuwa kiongozi huo, Kasembe alivamiwa na kuanza
kushambulia wakati akipita kukusanya mipira kutoka kwa vijana ambao wanaookotea
mpira kwa kuhofia isije kupotea punde mwamuzi wa mchezo huo atakapopuliza
filimbi yake ya mwisho wa kumaliza mchezo huo na kubaki kuwashangaza watazamaji
kwa hatua ambayo waliochukua maafande hao.
No comments:
Post a Comment