Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi
katika uzinduzi wa mradi wa vibanda vya biashara katika uwanja wa
Kambarage huku akishuhudiwa na Balozi wa China nchini Dr.Lu Youqinq.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka kwa baiskeli kutoka
Uwanja wa Kambarage kuelekea uwanja wa Shycom kwenye mkutano wa hadhara.
Balozi
wa China nchini Dk.Lu Youqinq akiwapungia wananchi wakati akielekea
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya
Shycom,Shinyanga mjini.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Balozi wa
China nchini wakiwasubiri wenzao tayari kuelekea kwenye uwanja wa Shycom
ambapo mkutano mkubwa ulifanyika.
Kutoka kushoto ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Balozi wa China nchini na Mbunge
wa Shinyanga mjini Steven Masele wakiendesha baiskeli kuelekea kwenye
uwanja wa Shycom ambapo mkutano mkubwa na wa kihistoria ulifanyika leo
tarehe 13 Septemba 2013.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiingia kwenye uwanja wa Shycom
na baiskeli tayari kuhutubia kwenye mkutano wa hadhara.
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto),Balozi wa China
nchini Dk. Lu Youqinq na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ,
Balozi wa China alipata fursa ya kuelezea kwa wananchi wa Shinyanga
namna uwekezaji utaweza kuunufaisha mkoa huo ambapo viwanda vya nguo,
kusindika mafuta, asali na bidhaa zitokanazo na mifugo vinategemewa
kujengwa katika mkuo huo na kutoa nafasi kwa ajira ,kuinua uchumi ,elimu
na kuondoa kabisa umasikini.
BY JOHN BUKUKU
No comments:
Post a Comment