Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii, inawatangazia Wahitimu wa taaluma
zilizotajwa hapo juu kuwa zipo nafasi za kazi katika Mikoa na
Halmashauri zote nchini isipokuwa Mkoa wa Dar es Salaam na Halmashauri
zake.
Waombaji wanatakiwa kuambatanisha nyaraka zifuatazo katika maombi yao:-
- Vyeti vya Elimu ya Sekondari.
- Cheti cha Kuhitimu mafunzo ya taaluma husika.
- Kwa wale wanaotakiwa Kwa mujibu wa sheria kufanya mafunzo kwa vitendo, wawasilishe cheti cha kuhitimu mafunzo hayo.
Mwisho wa kupokea maombi ni wiki mbili kuanzia tarehe ya tangazo hili kutoka. Aidha, juu ya bahasha iandikwe nafasi inayoombwa.
Majina ya watakaopangiwa vituo vya kazi yatatangazwa kwenye tovuti ya Wizara www.moh.go.tz
Barua zote zipitie Posta. Aidha, barua zitakazoletwa kwa mkono hazitopokelewa
Maombi hayo yatumwe kwenye anuani ifuatayo:-
KATIBU MKUU,
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII,
S.L.P. 9083,
DAR ES SALAAM.
No comments:
Post a Comment