BAADHI ya Wakulima wa Korosho katika Kijiji cha Ligoma Kata ya
Namsakata Wilayani Tunduuru Mkoani Ruvuma wameonesha mashaka ya
kupatikana kwa mafanikio kupitia mpango wa Sensa ya Mikorosho na
kuwasaji Wakulima hao.
Mashaka hayo yalioneshwa na Liputa Ntenda Mbwana,Selemani Mohamed
Ally, Rashid Ibrahimu na Ishiwa Adam Njuga wakati wakiongea na
waandishi wa habari ikiwa ni muda mfupi baada ya kusajiliwa na
kuongeza kuwa endapo hakuta kuwa na udhibiti wa visumbufu vya soko la
mazao yao nguvu kubwa na lasilimali ya taifa inayotumika itakuwa
imeteketea bule.
Wakulima hao ambao walikuwa wakiongea kwa nyakati tofauti katika
mahojiano hao walivibainisha visumbufu hivyo kuwa ni pamoja na
kutokuwepo kwa mikakati ya kudumu ya kuwatafutia wakulima soko la
uhakika la mazao yao,bei mzuri na udhibiti wa wanunuzi holela ambao
wanafahamika na Serikali na hununua kwa kutumia mfumo usio rasmi kwa
kutumia vipimo vya kangomba.
Aidha Wakulima hao waliuelezea mfumo huo kuwa ni mzuri na unaweza
kuwaletea manufaa makubwa endapo mipango na mikakati yake itatekelezwa
kwa vitendo na kwamba endapo mikakati hiyo itaishia katika makaratasi
kama ilivyo katika mipango mingine iliyowahi kuibuliwa na kufukiwa zao
hilo halitaendelea kamwe.
Awali wakiongea katika ufunguzi wa mafunzo ya Wataalamu wa Idara ya
Kilimo, watendaji Kata , Vijiji watakao tekeleza zoezi hilo la
usajili wa Wakulima hao yaliyofanyika katika ukumbi wa Klasta ya
Walimu Mlingoti kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya korosho Tanzania
(CBT) Sifuni Fadhili na Mkurugenzi wa Kilimo na Ubanguaji wa zao hilo
Luseshelo Silomba walimweleza Mkuu wa Wilaya hiyo Chande Nalicho
ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa zoezi hilo kuwa zoezi
hili likikamilika litaisaidia serikali kuandaa na kupanga mikakati ya
uhakika na kuwainua wakulima wa zao hilo nchini.
Alisema kutokana na muhimu zoezi hilo Bodi ya Korosho Tanzania
imejipanga na kuhakikisha kuwa zoezi hilo linakamilika kwa uhakika na
kwamba kwavile wao ndio watakao iwakilisha bodi ya korosho katika
zoezi hilo pia aliahidi kuwatembelea mara kwa mara wakati watakapo
hitajii ya mikorosho na uzalishaji wake hasa katika uandaaji wa
hahitaji ya madawa wakati wa kupulizia.
Nae Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania Mudhihir Mohamed
Mudhihir alimweleza Mkuu wa Wialaya hiyo kuwa Bodi ya korosho Tanzania
imedhamini na kuuenzi mchango wa wakulima wa zao hilo na kuamua
kufanya uzinduzi huo Kitaifa katika Tarafa za Namasakata na Nakapanya
Wilayani Tundnuru.
Alisema katika utekelezaji huo Bodi ya Korosho Tanzania kwa
kushirikiana na Mfuko wa kuendeleza tasnia ya zao la Korosho Tanzania
wamepanga kufanya usajili wa Mikorosho na wakulima wa zao hilo katika
Wilaya zote 41 zinazolima zao hilo.
Akiongea na Wakulima hao katika uzinduzi wa Sensa hiyo ya Mikorosho na
usajiri wa wakulima hao Mgeni rasmi, Mkuu wa wilaya ya tunduru Chande
Bakari Nalicho pamoja na mambo mengine aliwataka Viongozi wote katika
maeneo yao kuacha tabia za kufanya kazi kwa mazowea na akawaasa
kutimiza wajibu wao kwavitendo ili kufanikisha zoezi hilo.
Dc Nalicho aliendelea kubainisha baadhi ya faida za mpango huo kuwa ni
pamoja na kuisaidia Serikali kupanga na kuandaa mikakati itakayo
wasaidia wakulima kusimamia na kuhudumia mazao yao kwa uhakika,
itaongeza uzalishaji na kudhibiti wanunuzi holela wa Korosho hizo
kutoka kwa wakulima kwani wataweza kuwahoji watu wasio wakulima yaliko
mashamba yao na waliko zitoa korosho wanazo ziuza.
Mwisho
No comments:
Post a Comment