Tuesday, 10 September 2013

MAHAFALI YA CHUO KIKUU CHA ST JOSEPH SONGEA YAFANA







Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi dokta Shukuru Kawambwa amewataka wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini waliokopeshwa mikopo kwa ajili ya kupata elimu ya juu warejeshe mara wanapopata ajira ili kuwawezesha watanzania wengi zaidi kunufaika na mikopo hiyo.

Dokta kawambwa amesema hayo wakati akitoa hotuba katika mahafali ya nne ya chuo kikuu cha mtakatifu joseph kinachoto mafunzo ya tekinologia ya mawasiliano kilichopo songea mkoani Ruvuma.



Dokta kawambwa ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wajiri kushirikianan na serikali kuwatambua wafanyakazi wanaodaiwa mikopo na kuhakikisha wanalipa kwani kati ya shilingi trilioni 1.45 ni bilioni 35 tu ambazo zimesharudishwa.


Akizungumzia utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma diploma ambalo ni ombi la jumiya ya chuo cha matakatifu joseph waziri wa elimu huyo amesema serikali itaangalia uwezekano lakini ni ngumu kwa hata wanafunzi wa shahada sio wote wanaopata mikopo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya songea mheshiwa Joseph Mkirikiti amekihakikishia kuwa ombi la kupata eneo  la ekari 2000 kwa ajili ya chuo cha kilimo litafanyiwa kazi hata kama sio zote kwa mara moja.


Naye askofu wa jimbo la mbinga JOHN NDIMBO amesema chuo hicho kinachukua wanafunzi wa dini mabalimbali na hata wasiokuwa na dini kwa lengo la kuboresha mahusiano mema . Katika mahafali ya mwaka huu jumla ya wanachuo 97 wamehitimu wakiwemo 59 wa shahada na 38 stashahada.

Chuo kikuu cha st joseph kinadhaminiwa na DMI na tayari kina vituo katika mikoa ya ARUSHA , SONGEA, DAR ES SALAAM. Na njombe.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO