MSHINDI MISS ILALA KULAMBA MILIONI 1,500,000 KESHO
MREMBO
atakayetwaa taji la Redds Miss Ilala 2013, linalofanyika kesho Agosti
16, ataondoka na zawadi za jumla ya Sh. Milioni 1,500,000,huku mshindi
wa pili atajipatia shilingi milioni moja na wa tatu shilingi laki saba.
Mbali na zawadi hiyo, washindi hao watatu watapata ofa ya ya
miezi sita kutoka RIO gym & Spa, iliyopo Quality Center, kutumia
vifaa vyote ndani ya gym hiyo ambayo gharama yake ni Milioni 900,000 kwa
kila mtu.
Sh , 400,000 zitakwenda kwa mshindi wa nne na atakayeshika
nafasi ya tano yeye ataibuka na Sh 300,000. Washiriki wengine ambao
hawatabahatika kuingia katika nafasi ya tano bora, wote watapewa
Sh,200,000 kwa maana ya kifuta jasho.
Tumelenga zawadi za fedha zaidi, hii ni kutokana na ugumu wa
maandalizi kwa warembo ambao hugharamika zaidi, kiasi nasi kuona kuna
kila namna ya kuwapunguzia maamivu hayo.
Shindano hilo, linatarajiwa kuwa na burudani ya kipekee kutoka
kundi zima la Tanzania House of Talent (THT) wakiongozwa na mwanadada
mwenye sauti ya chiriku, Lina na Barnaba.
Kundi la Wanne Star nalo litajumuika katika kuufanya usiku wa
kesho kuwa wa burudani tosha kutokana na kuja kivingine kabisa katika
nyimbo za asili za Afrika.
Warembo watakaopanda jukwaani Julai 5 ni kutoka Kigamboni,
Kurasini na Chang’ombe ambao wanawania taji linaloshikiliwa na Miss
Tanzania namba tatu, Edda Sylvester walikuwa chini ya wakufunzi Suzy
Mwenda na Shadya Mohamed wakati kwenye kucheza nako walikuwa na walimu
wawili Super Bokilo na Charles.
Warembo wataoapanda jukwaani hityo kesho ni 14 Diana Kato, Martha Gewe, Alice Issac, Irine Mwelelo, Clara Bayo, Natasha
Mohamed, Doris Molel, Upendo Lema, Kabula Kibogoti, Shamim
Mohamed, Kazunde Kitereja, Rehema Mpanda, Johanither Kabunga,Anna
Johnson.
Shindano hilo limedhaminiwa na kinywaji cha Redd’s, Dodoma Wine,
Gazeti la Jambo Leo, Cloud’s Media, Blogu ya Wananchi (Le Mutuz),
Fredito Entertainment, CXC Africa tours & Safaris, RIO Gym& Spa,
Smile Internet, Delina Interprises na Kitwe General Traders.
Ilala Interteinment ndiyo inayoandaa mashindano haya,
inatanguliza shukrani zake
wadhamini wetu kwa miaka hiyo, sanjari na
vyombo vyote vya habari kwa ujumla wake, kwani ndio waliofanikisha
kufanikisha shughuli yetu ya kesho.
by John Bukuku
No comments:
Post a Comment