10 Agosti 2013
Halmashauri
ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imetoa tamko juu ya vibanda vya biashara
vya soko kuu la Songea kuwa mwisho wa kuchukua fomu na kujaza mikataba mipya
mwisho tarehe 30/8/2013.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ukumbi wa manispaa ya Songea meya wa manispaa
hiyo bwana Charles Mhagama amesema
atakayechelewa tarehe hiyo kuchukua fomu na kujaza mkataba mpya atanyang’anywa kibanda na kupewa ambaye
amechukua na kujaza fomu.
Tamko hilo
limetolewa hivi karibuni baada ya wafanyabiashara kugoma kuchukua na kujaza mikataba mipya ambayo inaanza upya .
Halmashauri
imeamua kupandisha pango la vibanda na huduma ya vyoo kutokana na kiwango
wanacholipa wafanyabiashara hao kupitwa na wakati.
Wafanyabishsra
hao awali walikuwa wanalipa shilingi elfu 40 hadi shilingi elfu 60 kwa sasa
mikataba hiyo inaonyesha imeongeza pango hadi kufikia shilingi 130,000 kwa
vyumba vya biashara hadi shilingi 200,000 kwa huduma za vyoo huku idadi ya
vibanda ikiwa ni 130.
Katika
maeneo ya katikati ya mji lilipo soko kuu la Songea wafanyabiashara wengine
wanalipa hadi shilingi laki 4 kwa mwezi.
Manispaa ya
Songea inakabiliwa na changamoto nyingi ambayo inahitaji fedha nyingi
kukabiliana na kero hizo kama vile kushindwa kuzoa takaka katika baadhi ya maeneo hata kwa mwaka mzima
hususani eneo la majengo ,barabara nyingi za mji bado zina makorongo na vumbi,
na huduma mbalimbali,
Changamoto
nyingine ni kwamba mfuko wa mikopo wa serikali za mitaa unaidai manispaa hiyo
zaidi ya shilingi milioni 126 hali inayoifanya manispaa hiyo kushindwa kukopa
tena kutoka katika mfuko huo ili kujenga standi kuu ya mabasi na kuboresha
huduma nyingine.
Hiyo ni
taarifa kutoka uongozi wa manispaa na wameuomba umoja wa wafanyabiashara
kutokuwa wachochezi kati ya manispaa na wafanyabiashara.
No comments:
Post a Comment