Na Amon Mtega,
Namtumbo.
WATOTO wa nne wa Familia moja wa kijiji cha Ligunga kata ya
Lusewa tarafa ya Sasawala wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wamefariki dunia na wengine 12 wamelazwa
katika Hospitali ya mkoani humo na katika kituo cha Afya cha Lusewa kwa madai
ya kula chakula kilicho kuwa kimewekwa sumu.
Akiongea na
waandishi wa habari katibu tarafa wa Sasawala Fred Maliyao alisema kuwa wanafamilia
hao walikula vyakula vya karibu aina tatu na walikuwa 19 ambapo chakula kingine
kilisadikika kuwa kilikuwa na sumu ambayo iliweza kuwazuru na kusababisha vifo
hivyo.
Maliyao alifafanua
kuwa katika siku ya sikukuu ya IDD wanafamilia hao walikula chakula ugari kwa
mboga ya samaki ,mbonga ya majani aina ya chaina na utumbo wa kuku ambao
usadikika ulikuwa umechemshiwa mchuzi wa samaki huku wengine walikula ugali kwa
mboga ya mbaazi ,utumbo wa kuku na mboga majani chaina.
Alisema kuwa walikula
chakula kwa baba yao mdogo na mkubwa kwa
zamu ambapo walikuwa wakiifurahia sikukuu ya IDD kwa familia hiyo kutembeleana
na kufarijiana kwa sikukuu.
Kwa upande wake
mwanafamilia Bilahi Mumba alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 9 mwaka huu
majira ya saa 5 hadi saa sita mchana baada ya watoto hao kula chakula kwa Baba
yao mdogo Mumba ambaye anadai kuwa alinunua samaki hao kwa mtu mmoja katika
eneo la Lusewa kwa bei ya shilingi 1500.
“Nasisi
tunashangaa tuliona muda mfupi baada ya kula chakula hicho walianza kuanguka na
wengine kutapika huku tukijitahidi kuokoa maisha ya watoto hao lakini wanne wameweza
kufariki na wengine tuliwakimbiza kituo cha afya cha Lusewa.
Mumba aliiwataja
watoto hao waliyokufa kuwa ni Zidane Mumba[2.5] Tazamio Mumba [9] Selemani
Mumba [7] na Zahara Mumba [2] na kuwa wote ni wafamilia moja.
Naye muuguzi wa
kituo cha afya za Lusewa Edrisa Ndauka alisema kuwa walipokelewa wagonjwa 16
katika kituo hapo na wanne walifariki watano walikimbizwa hospitali ya mkoa
Songea na kuwa wengine walibaki kituoni hapo.
Hata hivyo
mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani humo Abdula Lutavi ambaye naye alienda
kushuhudia tukio hilo alisema kuwa tatizo hilo ni kubwa kwa kuwa waliyoathirika
ni watoto wa familia moja.
Lutavi
alisema licha ya watalamu kuchukua matapishi na mabaki ya vyakula hivyo kwa
kwenda kuvipima lakini taarifa za awali zinaonyesha kuwa sumu iliwekwa kwenye
samaki maana wote waliyo gusa samaki au
mchuzi wake wamepata athari.
Mkuu huyo ametoa onyo kwa baadhi ya watu wakijiji hicho ambao huvua samaki kwa kutumia sumu mbalimbali
zikiwemo za zao la Tumbaku kwa ajili ya kujipatia kitoweyo ,sasa waache mchezo
huo badala yake watumie ndowano na nyavu.
Kamanda wa
polisi mkoani Ruvuma Deusdedit Nsimeki amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
wanamshikilia mtu mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Salumu kwa mahojiano
zaidi kuhusiana na tukio hilo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment