Jaji mkuu OTHMAN CHANDE amempongeza Rais
JAKAYA KIKWETE kwa hatua mbalimbali za kuimarisha na kuboresha shughuli za
kimahakama na sheria na kuzingatia misingi ya utawala bora.
Akizungumza wakati wa mkutano Rais
KIKWETE kuwaaga viongozi na watumishi wa mahakama Jaji CHANDE amesema
anamshukuru Rais kwa kufuatilia na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili
sekta hiyo.
Jaji Mkuu ametaja baadhi ya changamoto
zilizopatiwa ufumbuzi kuwa ni pamoja na ujenzi na maboresho ya majengo ya
mahakama na ujenzi wa nyumba za mahakimu na kuongeza idadi ya watendaji wa
mahakama wakiwemo mahakaimu na majaji.
Aidha pia amempongeza Rais KIKWETE kwa
kuweka uwiano mzuri wa uteuzi wa watendaji wa mahakama kwa kuzingatia usawa wa
kijinsia ambapo hivi sasa majaji wanawake wamefikia asilimia 41 kati ya majaji
wote TANZANIA.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Majaji wa
mahakama kuu majaji wafawidhi majaji wastaafu, majaji wakuu wa rufani na majaji
viongozi. Waziri wa katiba na sheria, Rais wa chama cha wanasheria Tanzania,
wasajili wakurugenzi na watumishi wa mahakama.
@@@@@@@@@
Wadau wa mazingira katika nchi za Jumuiya ya AFRIKA Mashariki
wametakiwa kushirikiana ili kukabiliana na ongezeko la mmea wa GUGUMAJI ambao
unatishia kutoweka kwa viumbe wa majini kwenye ziwa VICTORIA.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Ushirikiamo wa AFRIKA Mashariki Dakta
ABDULLA JUMA SAADALA mwishoni mwa ziara yake ya kutembelea kituo cha kuzalisha wadudu aina ya
MBAWAKAVU ambao wanatumika kushambulia mmea wa GUGUMAJI kilichopo katika Chuo
Cha Uvuvi cha NYEGEZI mkoani MWANZA.
Naibu Waziri SAADALA amesema kuwa licha ya wadudu hao kufanikiwa kupunguza
mmea wa GUGUMAJI katika ziwa victoria jitihada zaidi bado zinahitajika.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi WILIAM LUKUVI ametoa muda wa miezi
Mitatu kwa Halmashauri ya Jiji la MBEYA kuhakikisha
makubaliano yanafikiwa na wakazi wa eneo la
SISITIRA kabla ya wakazi hao kutoa maeneo yao ili kupisha ujenzi
wa Chuo Kikuu Cha Sayansi na
Teknolojia MBEYA – MIST.
Waziri LUKUVI ametoa muda huo mara baada ya
kutembelea eneo hilo la SISITIRA ambalo kwa muda
mrefu wakazi wake wamekua wakitaka walipwe fidia kabla
ya kupisha ujenzi wa Chuo Kikuu hicho.
Mara baada ya kuzungumza na wakazi wa eneo hilo, wa
ziri LUKUVI pamoja na mambo
mengine ametaka kufanyika upya kwa tathmini ya maeneo ya wakazi hao.
@@@@@@@@@@@@@
Zoezi la ukoaji
linaendelea katika bahari ya Mediteranian baada ya boti waliokuwa wakisafaria
wahamiaji haramu kuzama katika pwani ya LIBYA.
Vikosi vya
ukoaji vikiongozwa na jeshi la majini vya IRELAND pamoja na ITALIA vinaendelea na kazi ya
uokoaji ambapo watu 400 wameokolewa wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Katika
ajali hiyo watu 25 wamepoteza maisha.
Mmoja ya
waokoaji amesema zoezi hilo limekabiliwa na changamoto kutokana kutofahamika
idadi kamili ya watu waliokuwa wakisafiri katika boti hiyo.
Wakati huo huo
msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani- UNHCR ,MELISSA FLEMING amesema idadi kubwa ya
wahamiaji wamekuwa wakikimbia vita na machafuko katika nchi zao
LEMING amekiri
kuwa safari za wahamiaji wanaokimbilia barani ULAYA zimekuwa zikihatarisha
maisha yao.
@@@@@@@@@@@
Wataalamu wa
ndege kutoka nchi za UFARANSA, MALAYSIA na AUSTRALIA wamegudua kuwa bawa la
ndege lililopatikana Magharibi mwa bahari ya HINDI katika visiwa vya REUNION,
lilikuwa la shirika la ndege ya MALAYSIA MH 370.
Waziri mkuu wa
MALYSIA NAJIB RAZAK amezungumza baada ya matokea hayo na kusema licha ya
maumivu watakayopata familia za waathirika uthibitisho huo utatoa uhakika wa
kile kilichotokea.
Ndugu wa familia
zilizoathirika wamekuwa na mashaka kuhusu uchunguzi huo na kudai kuwa wanahitaji miili ya wapendwa wao
waweze kuwafanyia mazishi ya heshima.
Aidha serikali ya AUSTRALIA kupitia waziri wake
mkuu,TONY ABBOTT imesema ugunduzi huo umetoa mwanga katika kutatua tatizo.
Ndege ya shirika
la ndege la MALYSIA MH 370 ilipotea March mwaka jana wakati ikifanya safari
zake ikitokea KUALA LUMPAR kuelekea BEIJING na kuuwa abiria woete
239 kwenye ndege hiyo.