Serikali ya awamu ya nne katika mahakama nchini Imesaidia kuboresha utoaji wa haki kwa wakati ,kukuza utawala bora, kulinda
amani ya nchi na ukuaji wa demokrasia.
Akizungumza katika hafla ya kumuaga aliyoandaliwa na
mahakama kuu nchini, KIKWETE amesema serikali yake imefanikiwa kuongeza bajeti
ya mahakama hadi kufikia bilioni 89, kuongeza watumishi wa mahakama ikiwemo
majaji kwa uwiano wa jinsia na kuboresha maslahi ya watendaji jambo
linalopelekea mahakama kufanya kazi kwa ufanisi.
Hafla hiyo ya kumuaga Rais JAKAYA KIKWETE imehudhuriwa
na viongozi mbalimbali wakiwemo wa ulinzi na usalama, majaji wa Mahakama
Kuu, wanasheria wa serikali na mawakili.
No comments:
Post a Comment