Mwenyekiti wa
chama cha wananchi CUF Profesa IBRAHIM LIPUMBA leo ametangaza kujiuzulu wadhifa
wake katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jijini DSM.
Profesa LIPUMBA
amesema amechukua hatua hiyo kutokana na Umoja wa Katiba ya wanananchi UKAWA
unaoundwa na vyama vya NCCR MAGEUZI, CHADEMA, CUF na NLD kushindwa kusimamia
makubaliano, ambapo amesema atabaki kuwa mwanachama tu katika chama hicho.
Wakati huo huo, Kaimu Mkurugenzi wa habari uenezi na
mawasiliano chama cha wananchi CUF Zanzibar ISMAIL JUSS LADU
amesema kuwa Chama cha Wananchi CUF hakiwezi kuyumba kwa
kuondokewa na aliyekuwa Mwenyekiti wake Prof. IBRAHIMU
LIPUMBA.
Akizungumza na
waandishi wa habari mjini Unguja JUSSA
amesema maamuzi ya kujiuzulu Prof. IBRAHIMU LIPUMBA ni maamuzi yake binafsi
ambayo wanayaheshimu na Chama kitaendelea kusonga mbele.
Hatahivyo
amesema mchango wake alioweza kuutoa katika kipindi chake cha Uongozi ,
CUF itaendelea kuuenzi na kuuheshimu licha ya yeye kujiuzulu nafasi hiyo.
Akizungumzia
kuhusu suala la umoja wa UKAWA ndio chanzo cha Profesa LIPUMBA kujiuzulu,
JUSSA amesema si kweli kwani maamuzi yote ya Chama yalikuwa yakifanywa chini
yake na kushirikishwa vyema .
Hivi sasa Baraza
Kuu la CUF limepanga kuanza kufanya vikao vyake ili kuweza kuziba pengo hilo
aliloacha Profesa LIPUMBA .
No comments:
Post a Comment