Watu 30 wamekufa na wengine 25 kujeruhiwa
katika jimbo la MADHYA PRADESH nchini INDIA, baada ya treni mbili za abiria
kupinduka. Treni hizo zimepinduka, baada ya mataruma ya reli kusombwa na maji,
kutokana na mafuriko makubwa yaliyoikumba nchi hiyo.
Mabehewa yaliyokuwa yakikokotwa na treni hizo mbili
yalipinduka, na waokoaji wamekuwa wakiendelea na zoezi la kuwanasua watu
walionasa katika mabehewa ya treni hizo, usiku kucha wa kuamkia leo.
Mvua za msimu zilizokuwa zikiendelea kunyesha
mfululizo kwa wiki mbili nchini INDIA, zimesababisha maeneo mengi kuwa
chepechepe, na hivyo hata mataruma ya reli kushindwa kuhimili uzito wa treni.
Shirika la reli la INDIA limesema kuwa, limekuwa likifanya ukaguzi wa mara kwa
mara wa reli zake.
Hata hivyo kuna habari kuwa, kingo za bwawa moja
kubwa lililoko karibu na njia za reli zilipasuka na kufanya maji yake kusambaa,
hivyo na hivyo kutatiza njia za reli. Wakati huohuo
Umoja wa Mataifa umesema, raia wapatao elfu TANO
wameuawa nchini AFGHANISTAN katika kipindi cha miezi sita iliyopita. Taarifa
iliyotolewa na umoja huo inasema watu waliokufa zaidi nchini humo ni wanawake
na watoto.
Mapigano yanayoendelea nchini AFGHANISTAN ni moja
kati ya sababu za vifo nchini humo, huku kundi la wapiganaji wa TALEBAN,
likishutumiwa. Mtu mmoja aliyehojiwa anasema, mapigano hayo yamesababisha raia
kushindwa kupata huduma muhimu za kibinadamu.
No comments:
Post a Comment