Rais wa ZANZIBAR Dkt. ALI MOHAMED SHEIN ametoa wito
kwa wanawake nchini kuchangamkia fursa za mafunzo yanayotolewa katika kituo cha
kufundisha wanawake utengenezaji wa vifaa vya umeme wa jua na ujasiriamali
alichokifungua katika kijiji cha KIBOKWA, wilaya ya Kasazini ‘A’, Mkoa wa
KASKAZINI UNGUJA.
Akizungumza katika ufunguzi wa kituo hicho, Dkt. SHEIN
amesema kituo hicho kinatoa mafunzo kwa wanawake wote hata waliokosa fursa ya
kwenda shule ikiwa ni utekelezaji wa mipango ya serikali
kuwawezesha wanawake kuimarisha ujasiriamali.
Kwa upande wake, Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa
Jamii,Vijana, Wanawake na Watoto Zanzibar ZAINAB OMAR MOHAMED amesema uzinduzi
wa kituo hicho umefungua ukurasa mpya wa harakati za maendeleo ya wanawake.
Kituo hicho kimegharimu shilingi milioni mia moja na
ishirini na nne ambapo Serikali ya Mapinduzi ZANZIBAR imetoa shilingi milioni
76 wakati shilingi milioni 48 zimetolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia wanawake.
No comments:
Post a Comment