Serikali ya CAMEROON imesema wapiganaji wa kikundi cha BOKO HARAM cha nchini NIGERIA wamewateka nyara watu 135, kaskazini mwa CAMEROON. Wapiganaji hao pia wamewaua watu wengine wanane katika eneo hilo.
Wapiganaji wa kikundi cha BOKO HARAM mara kadhaa
wamekuwa wakifanya mashambulio ya kigaidi nchini NIGERIA, na katika nchi jirani
na hivyo kuhatarisha usalama katika nchi hizo. Viongozi wan chi za AFRIKA
Magharibi, walikubaliana kuunganisha majeshi yao ili kupambana na wapiganaji
hao wa kikundi cha BOKO HARAM.
Hata hivyo
wapiganaji hao wamekuwa wakiendelea na mashambulio dhidi ya raia katika maeneo
mbalimbali ya nchi hiyo. Wiki iliyopita rais MUHAMADU BUHARI, wa NIGIERIA,
alikwenda nchini CAMEROON, kuomba msaada zaidi ya kijeshi ili kuwadhibiti wapiganaji
hao wa kikundi cha BOKO HARAM.
Serikali ya MISRI inatarajia kupanua mfereji ya
SUEZ, unaotumika kupitishia meli kubwa za kibiashara kutoka barani ULAYA kwenda
katika maeneo mengine ya dunia.
MISRI imedhamiria kupanua mfereji huo, ili kuongeza
idadi ya meli zinazosafiri kupitia mfereji huo na kuliongezea taifa hilo pato.
Kupanuliwa kwa mfereji huo pia kutasaidia kupunguza misululu ya meli
zinayosubiri kupita katika mfereji wa SUEZ.
Ujenzi wa mfereji huo unaotarajiwa kuanza leo
ALHAMIS utagharimu YURO Bilioni SABA. Mfereji wa SUEZ unaoziunganisha bahari za
MEDITERANIAN, mto NILE na hatimaye kuelekea kwenye yaSHAM ni kiungo kikubwa
kati ya nchi za ULAYA na ASIA.
Vikosi vya ukoaji vya nchini ITALIA, vikiongozwa na
jeshi la majini la IRELAND vinaendelea na zoezi la uokoaji katika bahari ya
MEDITERANIAN baada ya boti iliyokuwa imebeba abiria zaidi ya 600 kuzama
baharini.
Hadi sasa waokoaji wamefanikiwa kuwaokoa watu 400
wengi wao wakiwa wanawake na watoto.
Watu 25 wamethibitika kufa katika ajali hiyo iliyotokea karibu na pwani
ya LIBYA na watu hao walikuwa ni wahamiaji waliokuwa wakielekea barani ULAYA.
Wokoaji wanasema, zoezi hilo linakabiliwa na
changamoto kwa waokoaji kutojua idadi kamili ya watu waliokuwa wakisafiri ndani
ya boti hiyo.
Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi
duniani- UNHCR ,MELISSA FLEMING amesema
idadi kubwa ya wahamiaji wamekuwa wakikimbia vita na machafuko katika nchi zao
Polisi nchini KENYA wamewaachia huru wanafunzi TISA,
kati ya wanafunzi KUMI NAMMOJA waliotiwa nguvuni kwa tuhuma za kuchoma bweni
katika shule ya sekondari ya wavulana, wanayosoma ya STEPH JOY.
Polisi pia wamewafungulia mashtaka ya kuhusika na
vifo, wanafunzi watatu wa shule hiyo waliokamatwa mapema wiki hii. Wanafunzi
watatu wa shule hiyo ya sekondrii ya STEPH JOY, walikufa baada ya bweni lao
kuchomwa moto.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo alilazimika kukimbizwa
hospitalini baada ya kupoteza fahamu, kutokana na mshituko wa tukio hilo.
Polisi wanasema moto huo haukutokana na hitilafu ya umeme, bali uliwashwa kwa
makusudi na watu.
Baadhi ya ndugu na jamaa za watu waliokufa baada ya
ndege ya MALAYSIA, MH 370 kupotea katika mazingira ya kutatanisha mwaka jana,
wanasema hawaamini kwamba mabaki, ya ndege hiyo yamepatikana katika bahari ya
HINDI.
Watu hao, kutoka CHINA wanataka serikali ya MALAYSIA
kuwapatia maelezo ya kutosha kuhusiana na ndugu zao.
Idadi kubwa ya abiria
waliokuwa ndani ya ndege hiyo ni raia wa CHINA na wanasema hawaamini kama bawa
na ndege lililookotwa katika visiwa vya RE-UNION ni la ndege hiyo.
Waziri mkuu wa MALAYSIA, anadai kuwa mabaki kipande
cha bawa hilo lililookotwa ni sehemu ya ndege hiyo iliyopotea mwaka jana, na
hakupatikana hadi leo. Amesema kupatikana kwa ndege hiyo kutasaidia kubainisha
kile kilichotokea kabla ya ndege hiyo kuanguka.
Zaidi ya watu 15 wamekufa na wengine 20 kujeruhiwa nchini
SAUD ARABIA, baada ya mtu mmoja kujitoa mhanga ndani ya msikiti mmoja. Habari
zinasema idadi kubwa ya watu wanaopendelea kuswali katika msikiti huo ni askari
wa kikosi maalum cha jeshi la SAUDI ARABIA.
Tukio hilo limetoka katika jimbo la ASIR,
linalopakana na nchi jirani ya YEMEN. Habari zinasema milipuko mingine miwili
ilitokea ikiambatana na mlipuko huo wa mskitini.
Ingawa hadi sasa hakuna kikundi chochote kilichodai
kuhusika na tukio hilo, lakini wapiganaji wa kikundi cha IS na wale wa kikundi
cha HOUTHI cha nchini YEMEN wanatuhumiwa kuhusika.
Mizigo ipatao elfu mbili, iko katika uwanja wa ndege
wa BARCELONA nchini HISPANIA, ikisubiri kuchukuliwa na abiria, waliyolazimika
kuiacha kwenye uwanja huo wa ndege baada ya shirika moja la ndege kufuta safari
zake.
Shirika hilo la ndege la HISPANIA linaushutumu
uongozi wa uwanja wa ndege wa FUMACHINO, ambao ulilazimika kuufunga uwanja huo
ukihofia moto uliotatiza safari za ndege. Moto ulio ulikuwa ukiwaka kwenye
msitu, unaopakana na wanja wa ndege wa FUMACHINO, na hivyo kutatiza safari za
ndege.
Abiria wanaomiliki mizigo hiyo wametakiwa kwenda
kwenye uwanja huo wa ndege kuitambua.
No comments:
Post a Comment