Wednesday, 5 August 2015

CATHY AKIPONGEZWA NA LUCY WAKATI WA MAHAFALI YA KUPATA GAMBA


                                                                CATHY NA LUCY



                                             
                                                SIBONIKE, HANNAH NA CATHERINE
                                       HANNAH MAYIGE       NA CATHERINE NYONI
                                                            MR AND MRS MAYIGE

RAIS JAKAYA KIKWETE AMEWAAPISHA MAJAJI 14 IKULU LEO.





Rais JAKAYA KIKWETE amewaapisha MAJAJI 14 ambao wameteuliwa hivi karibuni katika hafla fupi iliyofanyika IKULU jijini DSM hafla amabyo imeudhuriwa na viongozi na wadau mbalimbali wa sekta ya mahakama.




Majaji KUMI na WATATU  walioapishwa wanatarajiwa kwenda kufanya kazi MAHAKAMA KUU na JAJI mmoja ni wa MAHAKAMA ya RUFANI.




MAJAJI wa Mahakama kuu walioapishwa ni PAUL KASTUS , LAMECK MLACHA ,SALIMA CHIKOYO, ISAYA KWEKA  ADAM MAMBI,ISSA MAIGE, REHEMA KEREFU , JULIUS MALABA na SILUS MATUPA.




Wengine ni LUCIA GAMUYA, BIN HAJI SHABAN, VICTORIA LYIMO MAKANI, na WIRFRED PETER ambapo jaji RICHARD MZIRAY ameapishwa kuwa jaji wa mahakama ya Rufani.

WATU 30 WAMEKUFA NCHINI INDIA



 Watu 30 wamekufa na wengine 25 kujeruhiwa katika jimbo la MADHYA PRADESH nchini INDIA, baada ya treni mbili za abiria kupinduka. Treni hizo zimepinduka, baada ya mataruma ya reli kusombwa na maji, kutokana na mafuriko makubwa yaliyoikumba nchi hiyo.



Mabehewa yaliyokuwa yakikokotwa na treni hizo mbili yalipinduka, na waokoaji wamekuwa wakiendelea na zoezi la kuwanasua watu walionasa katika mabehewa ya treni hizo, usiku kucha wa kuamkia leo.



Mvua za msimu zilizokuwa zikiendelea kunyesha mfululizo kwa wiki mbili nchini INDIA, zimesababisha maeneo mengi kuwa chepechepe, na hivyo hata mataruma ya reli kushindwa kuhimili uzito wa treni. Shirika la reli la INDIA limesema kuwa, limekuwa likifanya ukaguzi wa mara kwa mara wa reli zake.



Hata hivyo kuna habari kuwa, kingo za bwawa moja kubwa lililoko karibu na njia za reli zilipasuka na kufanya maji yake kusambaa, hivyo na hivyo kutatiza njia za reli. Wakati huohuo




Umoja wa Mataifa umesema, raia wapatao elfu TANO wameuawa nchini AFGHANISTAN katika kipindi cha miezi sita iliyopita. Taarifa iliyotolewa na umoja huo inasema watu waliokufa zaidi nchini humo ni wanawake na watoto.




Mapigano yanayoendelea nchini AFGHANISTAN ni moja kati ya sababu za vifo nchini humo, huku kundi la wapiganaji wa TALEBAN, likishutumiwa. Mtu mmoja aliyehojiwa anasema, mapigano hayo yamesababisha raia kushindwa kupata huduma muhimu za kibinadamu.




Thursday, 5 February 2015

KIKAO CHA KWANZA CHA BODI YA MRADI WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI GEREZA KIGONGONI – BAGAMOYO KATI YA SHIRIKA LA MAGEREZA NA KAMPUNI YA TARBIM CHAFANYIKA LEO MJINI BAGAMOYO

unnamedX1 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim, Bw. Baddal Calikusu akitoa maelezo mafupi kabla ya Ufunguzi wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya Mradi wa Ubia wa Kilimo cha Umwagiliaji unaotarajiwa kuanza rasmi kutekelezwa katika eneo la Magereza, Gereza Kigongoni Bagamoyo(kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Green Park iliyoko Bagamoyo. unnamedX3Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim, Bw. Baddal Calikusu (aliyesimama) akitoa utambulisho kwa wajumbe wapya wa Bodi kabla ya Ufunguzi wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya Mradi wa Ubia wa Kilimo cha Umwagiliaji unaotarajiwa kuanza rasmi kutekelezwa katika eneo la Magereza, Gereza Kigongoni Bagamoyo . unnamedX4Mpimaji Ardhi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza,Mrakibu Msaidizi wa Magereza Habibu Yusuph akiwaonesha wajumbe wa Bodi mchoro wa Ramani katika mradi wa ubia wa Kilimo cha Umwagiliaji cha Gereza Kigongoni kati ya Kampuni ya Tarbim na shirika la Magereza.MAGEKamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Gideon Nkana akiwa na Wajumbe wengine wa Bodi ya mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji Gereza Kigongoni wakikagua eneo la Mradi utakapotekelezwa unnamedX5 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tarbim, Bw. Baddal Calikusu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji Gereza Kigongoni mara baada ya Kikao cha kwanza kilichofanyika katika Hoteli ya Green Park iliyopo Mjini Bagamoyo (wa kwanza kulia) ni Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Gideon Nkana(wa tatu kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Magereza,Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza John Masunga(

SERIKALI KUDHIBITI UJANGILI WA BIASHARA HARAMU MAZAO YA MALIASILI

mgi
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahmoud Mgimwa akijibu swali bungeni.
……………………………………………………………………………………
Na Lorietha Laurence-Maelezo,Dodoma SERIKALI imejidhatiti katika kudhibiti ujangili na biashara haramu ya mazao ya maliasili kwa kuridhia na kutekeleza mikataba minne ya kudhibiti ujangali wa tembo na unaovuka mipaka na kulinda mapori ya akiba.

Kuingia kwa sekta ya afya katika BRN kunaleta matumaini mapya

Mtendaji Mkuu wa PDB Bw. Omari Issa akielezeaumuhimu wa sekta ya Afya kuingia BRN kuungana na sekta nyingine zilizotangulia zinazoendelea kuzaa matunda

TUPE MAONI YAKO