Mheshimiwa Balozi Hamisi Kagasheki (MB)Waziri wa Maliasili na Utalii akisalimiana na wageni toka Lichinga Msumbiji.
Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) Akivalishwa Vazi la kijadi.
Baadhi
ya wazee wakiwa wameshika Silaha za Jadi walizotumia mababu zetu
kupigania dhidi ya kupinga utawala wa Wakoloni wa Kijerumani
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akiweka Sime.
Kamanda wa Jeshi la wananchi akiweka upinde
Mpiganaji
wa vita kuu ya pili ya Dunia Mzee Komba akisindikizwa na kamanda wa
Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwenda kuweka shahada ya uwa katika mnala
wa mashujaa.
Hii ni kwa nje ndivyo hali ilivyokuwa
Mhe
Balozi Hamisi Kagasheki(MB)Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na
viongozi wengine wakitoa salamu ya heshima kwa mashujaa wa majimaji
Hapo wanajeshi wakiendelea kutoasalamuza maombelezi kwa njia ya kijeshi
Kuinamisha kichwa chini ni dalili ya kumwomba
mwenyezi Mungu awaweke Mahali pema Mashujaa walioo tangulia Mbele
zahaki
Katika kuwakumbuka Mashujaa
waliotangulia mbele za Haki Jeshi la Wananchi limeweka Utaratibu Maalumu
ikiwa ni pamoja na kulipua mizinga na Fataki katika kuwakenzi Mashujaa.
Jeshi la
Wananchi wa Tanzania likitoka nje ya Uwanja wa Mashujaa baada ya kumaliza taratibu zote za
Maombolezo.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mzuri na wakuelimisha juu ya vita vya majimaji.
Moja ya wageni waliohudhuria toka mikoa mbalimbali pamoja na nchi jilani ya Mozambiq
Chief Emanuel Zulu akiweka shada katika kaburi la pamoja la mashujaa wa vita vya majimaji
Bw. Balthazali Nyamusya Mhifadhi Kiongozi Makumbuaho ya Taifa Maji Maji Songea
Hili ndilo Kaburi la halaiki walipozikwa mashujaa wa vita vya Maji Maji , watu waliozikwa hapa ni 66
Eneo hili walilozikwa mashujaa hawa limekuwa eneo muhimu.
Humu ni ndani ya Nyumba yenye vifaa vya kumbukukumbu na hapa inaonekana baadhi ya watu wakiona picha zenye vielelezo
Mhe.Balozi Hamisi Kagasheki akipewa maelezo juu ya Kaburi la Songea Mbano ambaye alizikwa peke yake na jina la Mji wa Songea limetokana na jina lake
Balthazar Nyamusya Mhifadhi Kiongozi wa Makumbusho Ya Taifa Maji Maji Sonhgea akitoa maelezo kwa Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) alipokuwa akizuru ukumbi wa historia ya vita vya maji maji.Miongoni mwa vionyeshwa katika ukumbi wa historia ni zawadi iliyokabidhiwa na MeyaAugusto Assique wa Jimbo la Lichinga kwa kutambua mashirikiano ya kihistia na kitamaduni
Wazee wa Kimila wakibadilishana mawazo juu ya uwelewa wa kila mmoja kuhusu vita vya Majimaji
Baad
Wanakikundi cha Better Life wakitumbuiza katika sherehe za kumbukizi la Mashujaa wa vita vya Maji MAJI
Pichani ni Balozi Khamis Kahgasheki9m(MB),Dkt Rehema Nchimbi mkuu wa mkoa wa Dodoma na Kepten mstaafu Aseri Msangi RC njombe.
Mkuu
wa mkoa wa ruvuma Bw. Said Thabiti Mwambungu akiteta jambo na
Mhe.Balozi Hamisi Kagasheki (MB)Waziri wa Maliasili na Utalii akiweka
Ngao .
Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma
hukumbuka Mateso waliyoyapata Babu zao, Hapo wapo katika Viwanja vya
Mashujaa Mahenge Manispaa ya Songea kushuhudia Maombolezo yaliyoongozwa na
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamis Kagasheki.
Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Saidi Thabit Mwambungu akisalimiana na Mjuukuu wa
mpiganaji wa Vita kuu ya pili alishikana nae na pembeni yake ni Mzee
Komba ambaye ndiye mpiganaji wa Vita kuu ya pili.
Baraza la Kimila la Makumbiusho ya Vita vya Majimaji wakitumbuiza,
Kikundi cha kucheza mziki wa kizazi kipya kikitoa burudani mbele ya wageni waliofika katika makumbusho
Nimoja ya wageno toka mikoa mbalimbali wakifatilia kwa makini kinachoendela uwanjani hapo
Mkuu wa Wilaya ya Binga Bi.Senyi Ngaga akifanya utambulisho wa baadhi ya viongozi
Kama inavoonekana katika picha hapo juu baadhi ya wazee wakiwa katika hali tofauti juu ya uchungu wa mateso waliopata ndugu zao
Huyo ni mchekeshaji maarufu wa mkoa wa Ruvuma Bw. Chaku akitoa vitu vyake mbele ya jukwaa kuuHapo kila mmoja akisikiliza kwa hisia huku wengine wakiwa katika majonzi makubwa
Umati wa watu waliohudhuria katika katika tamasha la kumbukizi ya vita vya majimaji
wanafunzi wakisikiliza kwa makini juu ya historia ya vita vya majimaji iliyokuwa ikisomwa
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu akitoa maelezo juu ya Vita vya maji maji
Mama huyu kavaa vazi la magome ya miti ambalo vazi hili limetumia sana na wazee wa zamani ila kwa sasa vazi hili ni adimu
Mhe
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB)akisoma hutuba
Dkt
Rehema Nchimbi mkuu wa mkoa wa Dodoma akiwa na viongozi wengine
wakipitia vitabu vya Wizara ya Maliasili na Utalii, Kitabu cha
Maadhimisho ya kumbukizi ya vita vya Maji Maji Mkoa wa Ruvuma , Toleo la
1,mwaka 2006,2010-2012Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) akitoa zawadi kwa mzee JJ gama tuzo kwa niaba ya bisiwajibu Gama ikielezea mchango wa vifaa alivyotoa kwa mchango wa makumbusho ya Taifa,
Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) akitoa cheti cha ushiriki kwa kampuni ya Mantra .
Mhe Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) akimkabidhi mwanafunzi zawadi ya ushiriki kwa kuchora picha zilizobeba ujumbe wa vita vya majimaji
Chiefu Emmanuel Zuru akiwa na Mhe
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB)
Mhe
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) akitoa cheti cha ushiriki kwa kundi la Better Life
Picha ya pamoja ya viongozi waliotoka mikoa mbalimbali
Balaza la wazee wa mila za kijadi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi
Mhe
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamisi Kagasheki (MB) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Makumbusho
.............................................................................
Maadhimisho
ya Tamasha la Kumbukizi ya Vita vya
Majimaji na Utalii wa Utamaduni Kitaifa yamekuwa yakiadhimishwa kila
mwaka
tarehe 27 Februari, Mkoani Ruvuma kuanzia mwaka 2010. Dhana ya
maadhimisho haya ni kufanya Kumbukizi za Vita ya Majimaji ziwe
kichocheo
cha mabadiliko kwa jamii kifikra na Kiutamaduni. Kuwaleta pamoja wadau
wa historia ya Vita vya
Majimaji
Pia kuwakumbuka Mashujaa wa Vita vya Maji Maji walionyongwa tarehe 27
Februari,1906 na Wajerumani ambao wamezikwa katika eneo la Makumbusho ya
Kumbukizi ya Vita vya Majimaji – Songea
Vilevile Kutoa fursa kwa jamii kushiriki katika
kuenzi na kuendeleza urithi wetu kupitia
shughuli za kimila zinazofanywa na Wazee
wa Baraza la Mila na desturi za jamii iliyohusika katika tukio la Vita
vya Maji Maji.
Na kutoa elimu kwa Umma wa Watanzania kwa ujumla
kuhusu Kumbukumbu za Kimakumbusho kupitia matukio ya kimila na kihistoria.
Kuweka dhahiri madhumuni ya kuanzishwa kwa
Makumbusho ya Taifa nchini kwa vitendo.
Katika maadhimisho haya Waziri wa Mali asili na utalii Dkt.Hamis
Kagasheki ameitaka jamii nchini kuenzi harakati hizo zilizofanywa na mababu wa
taifa hili katika kupinga utawala wakikoloni.
Pia
amesema amefurahishwa kuona kuwa maadhimisho ya kumbukizi ya vita vya majimaji
yamekuwa na historia ya kuadhimishwa mwezi februari Mkoani Ruvuma katika ngazi
ya mkoa tangu nchi yetu ipate uhuru, Hii imelenga kuwakumbuka Mashijaa wa Vita vya Maji Maji.
Hii
imeonyesha kwa jinsi Uongozi wa mkoa , Wazee wa Baraza la Mila na Desturi na
wananchi wanavyothamini mchango waliokuwa nao Mashujaa hawa hata kujitoa mhanga
kutetea uhuru, haki na utawala wao pamoja na kulinda mila , tamaduni na
rasilimali zilizopatikana kwenye maeneo yao kwa manufaa ya jamii na taifa kwa
ujumla.
Hili
ni jambo la kuigwa na kila mtu kuthamini na kulinda urithi wetu wa utamaduni
kwa ajili ya vizazi vilivyopo na vijazo.
Akiendelea kusema ameshuhudia kuwepo kwa taarifa za mwanamke mmoja
aliyejulikana kwa jina la Mama Mkomanile ambaye alishiriki katika harakati hizo
za mapambano dhidi ya utawala wa kikoloni hivyo ni ishara kuwa akina mama nao
walishiriki kikamilifu katika mapambano hayo dhidi ya ukoloni ambapo kwa upande
wa Tanganyika ilikuwa ni Vita ya Maji maji ,na kwa upande wa Kenya ilikuwa ni
Mau mau na vyote vilikuwa ni chanzo cha vuguvugu la ukombozi wa bara la Afrika.
Pia ametoa wito kwa wadau wa utafiti kufanya utafiti zaidi habari za
mwanamke huyo ili nazo ziweze kuingizwa kwenye historia ya kumbukizi hiyo ya
vita ya Maji Maji ambayo pia ilikuwa ni chachu ya ukombozi wa bara la Afrika
kwa ujumla.
Habari na picha kwa hisani ya www.demashonews.blogspot.com