Gari
la Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA likirejea katika Ofisi ya Kanda ya
Kusini Magharibi ya Pori la Akiba la SELOU likitokea ndani ya Pori
Pembe za ndovu, Risasi na Silaha zilizokamatwa
Mwandishi wa Habari wa Tbc Bw. Gerson Msigwa akiangalia moja ya nyara zilizokamatwa
Mwandishi wa habari wa demashonews akiwa ameshika risasi zilizokamatwa
Kampuni
ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA kwa kushirikiana askari wanyamapori wa Selou na
Askari wa vijiji vinavyozunguka pori la Akiba la Selou wamefanikiwa kukamata
meno ya tembo 15 yenye thamani ya milion miambili, Risasi 9, Bunduki moja aina
ya RIFFLE 458 na Gobole moja ambavyo hutumika kuulia wanyama .
Doria
hiyo imechukua takribani siku tatu katika pori la Akiba la Selou ikiwa ni sehemu
ya kuwatafuta majangili wanaofanya mauaji ya wanyamapori katika pori hilo,
Akizungumza
na mwandishi wetu Bw. Mohamed Mpapa ambaye ni mwakilishi wa kampuni hiyo ya GAME
FRONTIERS OF TANZANIA, Amesema kuwa hiyo ni kujituma kutokana na motisha ya
fedha anayoitoa mwezeshaji wa kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA ndio chachu
ya mafanikio ya kukamata meno,bunduki na risasi.
Akiendelea kuzungumzia tukio hilo Bw. Mohamed
Mpapa amesmea baada ya majangili kuwaona Game Frontiers Tanzania wakiwa katika
doria ndani ya pori hilo huku wakiwa wamekamilika kimapigano majangili hao
waliweza kukimbia na kuacha nyara hizo baada ya kuona nguvu yao ni ndogo katika
kupambana na kundi la doria.
Ameongezea
kwa kusema Kampuni yake imefurahishwa na mafanikio na ushirikiano uliopo kati
yao, Serikali na wanavijiji kukabiliana na ujangili unaoendelea kuwamaliza
tembo katika Pori la Akiba la Selou pia ametoa wito kwa jamii kuendelea kutoa
ushirikiano katika kuwafichua majangili.
Nae
Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kusini Magharibi ya Pori la Akiba la Selou Bw. Bernald
Lijaji amesema Pembe zilizokamatwa ni 15 pamoja na Bunduki aina ya RIFLE 458,Gobole
moja na Risasi 9 aina ya 458 vimekamatwa katika Doria iliyofadhiriwa na
Mwekezaji wa Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA
No comments:
Post a Comment