Mkuu wa mkoa wa Ruvuma bw:Said Mwambungu
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu amewataka wakazi wa mkoa wa Ruvuma kukataa kwa nguvu zote kuchochewa kufanya fujo na kusababisha kumwagika kwa damu za watu wasiokuwa na hatia.
Mkuu huyo wa
mkoa wa Ruvuma ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini yaliyofanyika katika viwannja vya mahakama kuu kanda ya Songea katika manispaa ya
Songea.
Kaimu jaji mfawidhi Hamisa Kalombola
Said mwambugu amesema wakazi wa
Ruvuma wakikubali kushawishiwa kufanya fujo ndipo watu wanapojichukulia sheria mkononi wakati vyombo vya sheria vipo.
Amesema
tabia ya watu kujichukulia sheria mkononi inapaswa kupingwa kwa nguvu
zote kwa kuwa vitendo hivyo vinavunja amani ya nchi.
Kaimu jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Songea mheshimiwa Hamisa Kalombola Kuna madhara makubwa ya watu kupuuza utawala wa sheria mfano wananchi wanaojiita wenye hasira na kujichukulia sheria mkononi, na kuua na kujeruhi watu ambao hawana hatia.
Jaji Kalombola amesema utawala wa sheria una umuhimu katika jamii kwa kuwa unaleta usawa kati ya watawala na watawaliwa na ndio maana hata serikali ikikosea inafikishwa mahakamani.
Baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya siku ya sheria Jaji wa mahakama kuu kanda ya Songea alikagua gwaride
.
No comments:
Post a Comment