Sherehe za kutangaza vivutio vya
asili vya bara la Afrika zinategemea kufanyika katika hoteli ya Mt
Meru katika jiji la Arusha Tanzania tarehe 11 February 2013 kuanzia saa
nane mchana.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Bodi
ya Utalii Tanzania viongozi mbali mbali wa kitaifa na kimataifa ambao
wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo ambayo mgeni rasmi atakuwa Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda.
Rais wa Taasisi iliyoendesha
shindano hilo la kutafuta Maajabu hayo Saba la Seven Natural Wonder Dr
Philip Imler kutoka Marekani anatarajiwa kuwasili tarehe 9/2/2013 tayari
kutangaza vivutio Saba vya Asili vya bara la Afrika.
Tanzania ilikuwa na vivutio vitatu
vilivyoingia kwenye kinyanganyiro hicho ambavyo ni Mlima wa Kilimanjaro,
Bonde la Ngorongoro na wanyama wanaohama wa Seregeti. Tanzania
imekwisha tajwa kuwa miongoni mwa washindi ambao angalau kivutio kimoja
ama zaidi Saba ya Asili Afrika.
Macho na masikio ya watanzania ni kujua ni kivutio au vivutio gani hivyo vya Tanzania vimeweza kushinda.
No comments:
Post a Comment