Na Steven Augustino, Tunduru
MWENYEKITI
wa kamati ya Ulinzi ya Wilaya ya Tunduru, Mkuu wa Wilaya hiyo Mkoani
Ruvuma Chande Nalicho ametoa wiki moja kwa Wakulima na Wafugaji wa jamii
ya Kisukuma kuondoka katika eneo la hifadhi ya msitu wa Shamba la Bibi
vinginevyo hatua kali za Kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Dc,
Nalicho alitoa maagizo hayo baada ya kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Wilaya hiyo kufanya ziara ya kushtukiza katika msitu huo na kujionea
hali halisi ya uhalibifu wa vyanzo vya maji, mabwawa na misitu iliyopo
katika hifadhi hiyo inayo unganisha Vijiji vya Nangunguru, Majala na
Mkalekawana katika Tarafa ya Nampungu kata ya Nandenbo Wilayani humo.
Alisema
anatoa siku Saba kwa watu wote waliovamia msitu huo wa hifadhi kuondoka
kwani haiwezekani watu waendelee kuishi wanavyo penda na kuharibu
mazingira katika vyanzo vya maji na hifadhi ya misitu kana kwamba
serikali haipo
Mkuu huyo aliwataka Watendaji Kata
,Vijiji kwa kushirikiana na Maafisa Tarafa Wilayani humo kutekeleza
majukumu yao ikiwemo kuwaelekeza wafugaji kufuata taratibu za kuonana na
viongozi wa Vijiji husika, kufanya mikutano inayo wahusisha wananchi
katika maamuzi ya kuwapokea wafugaji hao ili kuyaondoa maeneo yao katika
migogoro ya aina hiyo.
“Kwavile mifugo ni muhimu kwetu na endapo
itatumika vizuri na kwa kuzingatia kanuni, miongozo na maelekezo
yanayotolewa na Serikali italeta manufaa kwa Wananchi wetu” alisema Dc,
Nalicho na kuongeza kuwa mtindo wa kuishi kwa uhasama kati ya wafugaji
na wakulima hauwezi kuwa na tija.
Awali akiongea katika ziara hiyo Afisa misitu wa Wilaya la Tunduru Rashid
Mtotela alimweleza Dc, Nalicho kuwa Wakulima na wafugaji hao walivamia
msitu huo mwaka 2006 /2007 na kuendelea kujiimarisha kila mwaka baada ya
kubaini kutokuwepo kwa vikwazo vyovyote kutoka Serikalini.
Alisema hifadhi hiyo ambayo awali ilikuwa
imeunganishwa na Hifadhi ya Taifa (Selous) tangu mwaka 1974 na baadae
kuunda hifadhi shirikishi mwaka 2007 kupitia mradi wa Jont participatory
Forest Menegement (JPFM) liyounganisha Vijiji vya Nangunguru,
Mkalekawana na Majala kila Kijiji kimekuwa kikikwepa majukumu yake ya
kulinda hifadhi hiyo hali ambayo imechangia kuendelea kuhalibika kwa
mazingira hayo.
Wakiongea kwaniaba ya Wananchi wa Vijiji
hivyo Mwenyekiti wa Kijiji cha Nangunguru Bw.Said Rashid Mkwekwele,
Mtendaji wa Kijiji hicho Zainabu Twaha na Afisa Tarafa wa Nampungu
Joshua John wakawashushia lawama baadhi ya wakuu wa Idara katika
halmashauri ya Wilaya hiyo kuwa umekuwa na kigugumizi katika ufuatiliaji
na uchukuzi wa maamuzi juu ya migogoro hiyo.
No comments:
Post a Comment