Monday, 29 July 2013

WAANDISHI WAPATA TUZO YA USALAMA WA BARABARA

Marwa Press 26.07.2013 009 
 Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Habari maelezo Bi. Zamaradi Kawawa akionyesha tuzo aliyoipokea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw.Assa Mwambene  iliyotolewa na Automobile Association of Tanzania kwa waandishi wa habari walishiriki katika kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu matumizi mazuri ya  barabarani.
Marwa Press 26.07.2013 016 
 Rais wa Automobile Association of Tanzania Bw.Nizar Jivani kulia, akitoa tuzo kwa bw. Abdilahi Kombo ambaye ni mratibu wa AAT kwa ushiriki mzuri wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu matumizi mazuri ya barabara.
Marwa Press 26.07.2013 020 
 Bw. Judica Benedict mwandishi wa habari wa gazeti la  The Guardian kushoto akipokea tuzo kutoka kwa Rais wa Automobile Association of Tanzania Nizar Jivani kwa ushiriki mzuri wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu matumizi mazuri ya barabara.
Marwa Press 26.07.2013 024  
Bw.Fredy Mwanjala mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi kushoto akipokea tuzo kutoka kwa Rais wa Automobile Association of Tanzania Nizar Jivani  kwa ushiriki mzuri wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu matumizi mazuri ya barabara
Marwa Press 26.07.2013 027 
Rais wa Automobile Association of Tanzania Nizar Jivani (wa tano kutoka kushoto waliosimama)  akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari baada ya kupokea tuzo ya ushirikiano wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu matumizi mazuri ya barabara,(picha zote na Lorietha Laurence-maelazo)
Na Jennifer Chamila, MAELEZO.
 TAASISI ya Automobile Association Tanzania (AAT) imetoa tuzo kwa waandishi wa habari kutoka katika  vyombo vya mbalimbali vya habari walio shiriki katika kutoa habari kwa wananchi kuhusu mafunzo yalio tolewa kwa waendesha bajaji na pikipiki  2500 kuhusu matumizi salama ya barabara.
Tuzo hizo zimetolewa leo  pamoja fedha taslimu na Rais wa taasisi hiyo Bw.Nizar Jivan katika sherehe fupi ilio fanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam,Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wamewaza kujinyakulia tuzo hizo.
 Rais  huyo alitoa tuzo  hizo  kwa waandishi na watu waliosaidia kukamilisha mafunzo hayo, ambapo    miongoni mwao ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw.Assa Mwambene, ambaye tuzo yake ilikabidhiwa kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo, Zamaradi  Kawawa. 
 
Wengine waliopata tuzo hizo ni Mohamed Ugassa kutoka gazeti la The Guardian,Freginia Ole Swai kutoka ITV,Fred Mwanjara wa Channel Ten,Elias Shamt wa TBC,Miguel Suleiman wa Citizen,Nasongelya Kilyanga wa Daily News,Khadija Mussa wa gazeti wa Uhuru,Zainabu Malongo kutoka Mwananchi,Hadja Hamis kutoka Mtanzania,Abas Yusuph mwandishi wa kujitegemea,Judica Benedict wa The Guardian.
 
Akizungumza na waandishi wa habari katika sherehe hiyo Bw.Nizar amesema kuwa,anawashukuru waandishi wa habari kwa kusaidia kutoa habari kwa wananchi juu ya mafunzo hayo yalio husisha matumizi salama ya barabara na jinsi ya kuepusha ajali za barabarani.
 
Vilevile taasisi hiyo imeitaka Serikali kuweka mikakati madhubuti ambayo itarahisisha kupambana na matumizi mabaya ya barabara.
 
“Serikali ihakikishe bodaboda zote zipewe namba maalumu ili iwe rahisi huzitambua pindi uhalifu utakapotokea kama ilivyo kwa teksi,” alisema Jivan.
 
Naye mmoja wa waandishi wa habari aliyejinyakulia tuzo hizo , Ugassa kutoka gazeti la The Guardian,ametoa wito kwa waandishi wa habari kuzidisha uhamasishaji  dhidi ya  matumizi bora ya barabara na kulipa mkazo suala hilo kama wafanyavyo katika masuala mengine kama vile Ukimwi.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO