Sunday, 14 July 2013

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KUZULU MKOANI RUVUMA KWA SIKU 8, ANAWASILI LEO

 http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2013/04/Said-Mwambungu-2.jpg
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu

———————————————-

Na Nathan Mtega,Songea


WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda anatarajia kufanya ziara ya siku nane mkoani Ruvuma kuanzia tarehe 14 mpaka 21 Julai mwaka huu kwa ajili ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo,kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi iliyokamilika katika wilaya zote tano za mkoa wa Ruvuma


Akizungumza na waadishi wa habari mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu amesema kuwa ziara hiyo ambayo ni ya pili kuifanya mkoani Ruvuma ikitanguliwa na ziara maalumu aliyoifanya kwa ajili ya uzinduzi wa matrekta mwaka jana katika wilaya ya Songea itaanza kwa kuwasili mjini Songea leo Jumapili jioni majira ya saa 10:30 jioni ambapo baada ya kupokelewa na kusomewa taarifa ya maendeleo ya mkoa kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma

 siku ya Jumatatu  asubuhi  atakwenda wilayani Tunduru katika kijiji cha Milonde ambako atapokea na kukagua ujenzi wa chuo cha ualimu Kiuma na kisha kuelekea mjini Tunduru ambako atapokea taarifa ya maendeleo ya wilaya.


Na atahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara utakaofanyika katika uwanja wa michezo na kisha atarejea Ikulu ndogo

 Jumanne asubuhi ataelekea wilayani Namtumbo ambapo baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya wilaya Ikulu ndogo na kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Namtumbo na kupokea taarifa na kuzinduwa  mradi wa machinjio ya kisasa wilayani humo pamoja na kupokea taarifa ya umeme na kisha kuuzindua rasmi umeme atawahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara na kuelekea mjini Songea.


Aidha amesema kuwa Jumatano asubuhi atakwenda wilaya mpya ya Nyasa na kupokea taarifa ya maendeleo ya wilaya na kusalimia wananchi katika kijiji cha Lituhi na kuelekea katika kijiji cha Kihagara ambako ataweka jiwe la msingi kituo cha Afya cha Kihagara na kuondoka kuelekea Liuli ambako atasalimia wananchi na kuelekea kijiji cha Lundo kwa ajili ya kuona fursa ya kilimo cha mpunga na kuelekea Mbamba-bay ambako ataweka  jiwe la msingi jengo la karakana ya boti za kisasa na kisha kuhutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara na kuzindua rasmi wilaya mpya ya Nyasa.


Na siku ya Alhamis Waziri Mkuu ataelekea wilayani Mbinga ambapo baada ya kupokelewa na kusomewa taarifa ya maendeleo ya wilaya ataelekea kijiji cha Masumuni kwa ajili ya kutembelea na kukagua shamba darasa la kahawa

 na kisha kuelekea kijiji cha Lifakara ambako atapokea taarifa na kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa kufua umeme na kuelekea kituo cha mabasi ambako atapokea taarifa na kuweka jiwe la msingi kwenye kituo hicho na kisha atapokea taarifa,kukagua na kuweka jiwe la msingi katika kituo kidogo cha mradi wa kupeleka umeme Mbamba- bay wilayani Nyasa na kisha kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara .


Mkuu wa Mkoa amesema kuwa siku ya Ijumaa asubuhi Waziri Mkuu ataelekea kijiji cha Kitai wilayani Songea na kuelekea kijiji cha Mkenda ambako atapokea taarifa ya maendeleo ya wilaya na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa soko la kimataifa la Mkenda na

 kisha ataelekea kijiji cha Mitimbi ambako atazindua ununuzi wa mahindi msimu wa wa mwaka 2013 katika kanda ya Songea na kuelekea Ikulu ndogo Songea

  siku ya Jumamosi ataweka jiwe la msingi ofisi ya uhamiaji ya mkoa wa Ruvuma na kisha kuelekea Luhira ambako atatembelea na kupokea taarifa ya uzalishaji wa vifaranga vya samaki na kisha atapokea taarifa ya maendeleo ya chuo cha ufundi stadi(VETA) 

uzinduzi wa chuo hicho na kisha kuhutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Manispaa Songea na Jumapili asubuhi atafanya majumuisho ya ziara hiyo . na Jumapili asubuhi ataondoka kurejea jijini Dar Es Salaam.

Picha na habari kwa hisani ya www.demashonews.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO