Monday, 7 October 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

KAMANDA-DIWANI-ATHUMANIKAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  
“PRESS RELEASE” TAREHE 07. 10. 2013.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA MICHE YA BHANGI.
MNAMO TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO ENEO LA UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA JULIUS S/O MWAMBENJE, MIAKA 23,  KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA NSALAGA- UYOLE  AKIWA NA BHANGI MISOKOTO 15  SAWA NA UZITO WA GRAM 75. MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KWENYE MFUKO WA RAMBO. MTUHUMIWA NI MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

WILAYA YA MBEYA MJINI – KUINGIA NCHINI BILA KIBALI
MNAMO TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 23:30HRS HUKO ENEO LA STENDI KUU JIJI  NA  MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA 1. NYELAKOZI D/O MELANIA, MIAKA 33,,MKULIMA,  NA 2. NDAISHIMILI D/O TEONYA,MIAKA 33,WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI BURUNDI  WAKIWA NA WATOTO 11 AMBAO PIA NI RAIA WA BURUNDI WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. MBINU NI KUSAFIRI KWA NJIA YA  KIFICHO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAKABIDHIWE IDARA YA  UHAMIAJI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO  KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA  MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA WAHAMIAJI HARAMU ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]
MNAMO TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 08:30HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MAJENGO KIJIJI CHA LUPA WILAYA YA CHUNYA   MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA LYIDIA D/O AMBAKISYE, MIAKA 25,  KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA LUPA  AKIWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI[GONGO] UJAZO WA LITA 5. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO]  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
MNAMO TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 09:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MAGUNGA KIJIJI CHA MAMBA WILAYA YA CHUNYA   MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA JOHN S/O LUTIMBO, MIAKA 29, MSUKUMA, MKULIMA, MKAZI WA MAMBA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 4. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO]  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
 [DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

PATA HABARI KATIKA MAGAZETI KWA LEO.

DSC 0013 193f0
DSC 0014 7b671
DSC 0015 c8256
DSC 0016 b0c35
DSC 0017 29e37
DSC 0018 af2c6
DSC 0019 12637
DSC 0020 2a31a
DSC 0021 15696
DSC 0022 58bdf

Saturday, 5 October 2013

TASWIRA YA SEMINA INAYOHUSU MADINI YA URANI ILIYOFANYIKA KATIKA WILAYA YA NAMTUMBO MKOANI RUVUMA

             Mkuu wa wilaya ya Namtumbo ABDALLAH LUTAVI akifungua semina hiyo


                                                                    WASHIRIKI




                                                               Waandishi wa habari




Thursday, 3 October 2013

WAZEE WA WILAYA YA TUNDURU WAILALAMIKIA HALMASHAURI YAO INAKWAMISHA MAENDELEO YAO.

                                          PICHA SIO YA ENEO LA TUKIO
                                                                  
                                          


Na Steven Augustino, Tunduru

Halmashauria ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma imelaumiwa kuwa imekuwa
ni kikwazo cha kuinua vipato vya Wazee na kuwafanya waendelee kuwa
tegemezi na kuwa omba omba  kwa watu wenye uwezo hali ambayo imekuwa
ikiwasababishia kupata manyanyaso.
 

Kero hiyo imebainishwa na Wazee kupitia Risala iliyosomwa katika
maadhimishao ya siku ya Wazee duniani iliyo adhimishwa katika ukumbi
wa Klasta ya walimu Milingoti Miji hapa na kuongeza kuwa hali hiyo
imetokana na halmashauri yao kushidwa kukamirisha ufungaji wa Mradi wa
mashine ya kukamulia Mafuta tangu mwaka 2005.
 

Katika kudhibitisha umuhimu wa mahitaji ya Mashini hizo Mstaafu wa
jeshi la Polisi Issa Kapopo na Condradi Ally Chikulo wakamweleza mkuu
wa Wilaya hiyo kuwa hadi hivi sasa wanashindwa kukamua mazao ya
alizeti waliyo yalima baada ya kuhamasishwa kuwa mashine hiyo ingeweza
kuwakomboa baada ya kuanza kufanya kazi hiyo ya kukamua mafuta.
 

Kero nyingine ambayo ilianishwa na Wazee hao kuwa ni pamoja na
halmashauri hiyo kushindwa kusimamia agizo la waziri Mkuu Mizengo
Pinda juu ya upatikanaji wa Matibabu bure kwa  Wazee hao.
 

 Kwamujibu wa taarifa hiyo ambayo ilisomwa na katibu wa umoja huo,
Mwalimu Mstaafu Salum Tabu alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2012/
2013 jumla ya wazee 360 wakiwemo wanawake 236 na wanaume 134
waliotibiwa katika mazingira magumu huku wengi wao wakitakiwa kwanda
kununua Dawa katika maduka ya madawa.
 

Akifafanua taarifa hiyo Katibu wa Chama cha Wazee na wastaafu Wilayani
humo Salum Tabu alisema kuwa Chama chao kinakabiliwa naa changamoto
kubwa ya kukosa fedha za kuwawezesha kuwafikia na kuwasajili Wazee
wenzeo katika
 

Aidha katika Risala hiyo pamoja na kukemea mmomonyoko wa maadili
unaoonekana kutawaliwa na kuiga tamaduni ya kimaghalibi pia Wazee
wakatumia nafasi hiyo kuwaonya wanaohatarisha amani ya nchi yetu kwa
kutumia miaamvuli ya dini na wakaitaka serikali kuwachukulia hatua
kali za kisheriaq ili kukomesha vitendo hivyo .
 

Akiongea na Wazee hao, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Chande Nalicho
pongeza kwa ubunifu wao wa kuanzisha kikundi cha uzalishaji mali na
akamuomba Mkurungenzi Mtendaji wa Halamsahauri ya Wilaya hiyo
kuvitambua vikundi vya wazee na kuangalia uwezekano wa kuwakopesha
mikopo yenye riba nafuu ili kuwakwamua katika matatizo yao ya
kimaisha.
 

 Alisema  kuwa serikali inatambua umuhimu wa kada hiyo ya Wazee ambao
wamekuwa ni hazi ya kutoa ushauri na busala katika matukio mbali mbali
huku akitumia semi za Wahenga kuwa “Ukiona Nyani amezeeka ujue
amekwepa mishale mingi”.
 

Alisema hivyo Wazee ni lasilima, nia hazi kubwa katika uendelezaji wa
Taifa  hili nakuongeza kuwa Wazee hao ndio walioitunza maliasili na
rasilimali amabzo kwa sasa zinaonekana  kuanza kutugombanisha
akawataka vijana kuiga mifano ya mambo mema na kufanya maandalizi ya
utunzaji wa maliasili.
 

Aidha aliwataka wazee kuwa wavumilivu wakati Serikali ikiendelea
kukamilisha mikakati yake kulingana na sera ya taifa ya wazee ya mwaka
2003 na kuhakikisha kuwa inafanya kazi.
 

 Dc, nalicho pia akamuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya
wilaya ya Tunduru kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa upatikanaji wa
kudumu katika ufuatiliaji wa upatika wa huduma ya bure kwa wazee wa
Wilaya hiyo ili kluondoa manung’uniko ambayo yamekuwa yakijitokeza.
 

Dc, Nalicho pia akatumia nafasi hiyo kuwapongeza Wazee hao kwa
utaratibu waliojiwekea wa kupeana Ng’ombe kila mwaka kupitia mpango wa
kopa ng’ombe Lipa Ng’ombe ambapo mwaka huu Mzee Idd Ausi Mpemba
alipokea Ndama kutoka kwa Bibi Catherine Komba.
 

Awali Mwenyekiti wa Chama cha Wazee na wastaafu Wilaya ya Tunduru (
CHAWATU) Said Ally Kabora sema kuwa maadhimisho hayo yatasaidia
kuikumbusha Serikali juu ya umuhimu wa kuwalipa pensheni kwa wazee
wote bila ubabuzi . 


 Mwisho

Wednesday, 2 October 2013

VIJANA JKT MLALE SONGEA RUVUMA WAKO TAYARI KULIJENGA TAIFA

 Wa kwanza kushoto ni Major THOMAS MPUKU akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga      SENYI NGAGA wakitazama vijana waliohitimu mafunzo katika kikosi cha JKT MLALE
                                                                  Heshima kulia
                                                 Wamesimama kupokea heshima ya Gwaride
                                     Hapo hakuna mchezo vumbi linaashiria wapo kazini


                             Angalia mguu wa kiongozi wa  kikosi cha gwaride alivyonyosha mguu
                                                               Macho mbele

Tuesday, 1 October 2013

WAZEE WA KIJIJI CHA SINAI WALILIA PENSHENI ITOLEWE HARAKA KWAKUWA WENGI WANAISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.

                                         SOMA MABANGO WANA MADAI MENGI




          Wazee wanatoka kuangalia Zahanati inayojengwa kwa nguvu za wanachi na serikali

WAZEE WA SONGEA WATUMIA SIKU YA WAZEE KUPELEKA MAJINA NA SAINI ZA WAZEE KWA MKUU WA WILAYA YA SONGEA KUIKUMBUSHA SERIKALI KUWALIPA PENSHENI.

 Mkuu wa wilaya ya Songea JOSEPH JOSEPH MKIRIKITI akiwaasa wazee waliokwenda ofisini kwake kuendelea kutumia fursa walizonazo kujipatia kipato.
                              Baadhi ya wazee wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Songea

Hapa Mzee mwalimu Hassara anamkabidhi Mkuu huyo wa wilaya majina na saini za wazee

TUPE MAONI YAKO