Monday, 20 May 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHANI MSIBA WA ALLY SYKES JIJINI DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mjane wa marehemu Ally Sykes, Zainab Ally, wakati alipofika kuhani msiba huo wa mwasisi wa TANU, aliyefariki jana jijini Nairobi. Marehemu Sykes anazikwa leo jioni jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa marehemu Ally Sykes, wakati alipofika kuhani msiba huo wa mwasisi wa TANU, aliyefariki jana jijini Nairobi. Marehemu Sykes anazikwa leo jioni jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiaga na Mzee, Harith Mwapachu na kulia ni Balozi. Paul Rupia wakati  wakati alipokuwa akiondoka baada ya kuhani msiba wa mwasisi wa TANU, Ally Sykes, aliyefariki jana jijini Nairobi. Marehemu Sykes anazikwa kuzikwa leo jioni jijini Dar es Salaam.
 
Chanzo cha habari ni Mrokim blog

Sunday, 19 May 2013

PICHA ZA TUKIO ZIMA LA KUKMBUKUMBU YA KUZALIWA WAYNE GERSON MSIGWA ILIYOFANYIKA NYUMBANI KWAKE BOMBAMBILI SONGEA RUVUMA

                                                                  WAYNE GERSON
                                                                            JUICE

                                                                                 KEKI

                                    Wayne na mpambe wake kevin nyuma ni kaka yake Wayne
                                                                     Wayne anakata keki
                                                             Rafiki wa Wayne Jovita


                                                Wayne na kaka yake Chester akimpongeza


                                                          Wayne na dada yake sabina
                                                       Wayne na dada yake Ombeni






                                                                    Happy birthday to you

Saturday, 18 May 2013

Wakazi wa Manispaa ya Songea walalamikia uchafu uliokithiri

Hili ni moja ya Ghuba lililopo pembezoni ya Mjia wa Songea

Ghuba hili lipo mtaa wa mahenge ambalo pia limesahulika kuzolewa taka
  Pichani hapo juu ni ghuba lililopo Mtaa wa Sovi barabara iendayo kituo kikuu cha Polisi likiwa limejaa uchafu .
Wafanya biashara wa Mabucha ya Nyama na wauza Viungo wakiendelea na biashara huku pembeni kukiwa na hali ya uchafu uliokithiri wasiwe na wasiwasi.  Chanzo:www.demashonews.blogspot.com
  .......................................................................

 BAADHI ya wakazi wa halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamelalamikia kukithiri kwa uchafu katika maeneo yote ya Manispaa hiyo na kusababisha maghuba ya kuhifadhia taka kufurika kwa muda mrefu yakiwemo yanayozunguka maeneo ya soko kuu,Majengo na kituo kikuu cha mabasi cha mjini Songea.

 Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema kuwa mazingira ya usafi kwa ujumla katika Manispaa ni mabaya na yanaweza yakaleta madhara makubwa ya kiafya ikiwa hali hiyo haitachukuliwa hatua za haraka na maafisa afya wa Manispaa hiyo kwa sababu baadhi ya maghuba yamefurika na kutoa harufu kali.

 Walisema kuwa ni muda mrefu hali hiyo ya uchafu imeendelea kuwepo na hakuna jitihada zinazofanyika kuiondoa hali hiyo ambayo ni kero kubwa kwa wakazi walio wengi wa Manispaa hiyo licha ya kuwa wamekuwa wakilipa ushuru wa usafi wa mazingira kila mwezi.

 Wakizungumza Sebastiani Komba na Elizabeth Luambano wakazi wa Bombambili walisema kuwa ni vyema halmashauri ya Manispaa hiyo ikachukua hatua za haraka za kuiondoa adha hiyo ambayo imekuwepo kwa muda mrefu huku Adam Haule na Edson Kumbuka wakazi wa Majengo wakisema kuwa maghuba ya kuhifadhia taka yaliyopo yamefurika kupita kiasi na watoto wakicheza kwenye maghuba hayo hali ambayo inaweza ikawasababishia madhara.

 Naye Seleman Said mfanyabiashara wa soko kuu alielezea kusikitishwa kwake na hali ya kukithiri kwa uchafu ndani ya eneo la soko kuu ambamo kuna ghuba la kuhifadhia taka ambalo ni muda mrefu gali la kuzoa taka halijafika kuchukua taka taka zilizofurika kwenye ghuba hilo na Rashid Husein wa kituo kikuu cha mabasi cha mjini Songea alisema kuwa taka taka zilizopo kwenye ghuba ambalo lipo kando kando mwa kituo hicho zimekuwa kero kwa wasafiri na wapiti njia.

 Afisa afya wa Manispaa ya Songea Maxmilian Mahundi alipojohojiwa na mwandishi wa habari kuhusiana na hali hiyo alikataa kusema chochote kwa madai kuwa yeye siyo msemaji hata hivyo jitihada za mwandishi wa habari zilimtafuta Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Nachowa Zacharia ambaye alikiri kukithiri kwa uchafu katika halmashauri hiyo.

 Alisema kuwa halmashauri ya Manispaa ya Songea ina magari mawili tu ambayo ni chakavu na yana zaidi ya miaka ishirini tangu yaliponunuliwa huku mahitaji ya magari mapya kwa ajili ya kuzoa taka ni sita ambayo yana uwezo wa kubeba taka tani ishirini kila moja na kijiko kimoja cha kuzolea taka badala ya kutumia vibarua ambao wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa kutumia vitendea kazi duni.

 Aidha amewahimiza wakazi wa Manispaa kuendelea kulipa ushuru wa usafi kwa kila kaya ambayo ni shilingi 150 kwa kila siku ili kupunguza adha iliyopo ya uchafu uliokithiri kwenye maeneo mengi ya Manispaa hiyo.

Friday, 17 May 2013

OSHA yashiriki kwenye maadhimisho ya hifadhi ya jamii inayoendelea mkoani Dodoma

Mwananchi akipata maelezo toka kwa ndugu Claver Happy Mwinuka mshiriki wa maonesho kwenye Banda la Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa kazi (OSHA) kwenye wiki ya Hifadhi ya Jamii Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa OSHA Dr. Akwilina Kayumba, akimkabidhi Machapisho mbalimbali ya OSHA,Bi Irene Isaka alipotembelea Banda la OSHA kwenye maadhimisho ya Wiki ya Hifadhi ya Jamii Dodoma.
Mmoja wa wafanyakazi wa Kiwanda cha kutengeneza Magodoro cha Modern Mattress cha mjini Dodoma akipima afya yake, kwenye Viwanja vya Nyerere Square, kwenye maadhimisho ya Wiki ya Hifadhi ya Jamii
Wafanyakazi wa Kiwanda cha Magodoro cha Mdoern Matresscha mjini Dodoma wakipata maelekezo kutoka kwa Dr. Wambura juu ya upimaji wa mapafu kabla ya kuanza kwa zoezi la upimaji kwenye banda la OSHA.  
Mfanyakazi akipima uwezo wa mapafu kuafanya kazi kwenye Banda la OSHA kwenye maadhimisho ya wiki ya hifadhi ya jamii Dodoma
 
 
Habari na Afisa Habari-OSHA

Thursday, 16 May 2013

UFAFANUZI WA ASKOFU MTEGA KUSTAAFU HUU HAPA

17.05.2013
Askofu Mkuu Mstaafu wa jimbo Katoliki la Songea Mhashamu NORBERT MTEGA amekutana na waandishi wa habari Mjini SONGEA Mkoani RUVUMA kwa lengo la kutoa ufafanuzi juu ya uamuzi wake wa kumuomba Baba Mtakatifu kustaafu na kusema amefanya hivyo kwa maslai ya jimbo kuu Katoliki la Songea baada ya kubaini kuwa afya yake haimwezeshi kumudu majukumu ya kiutawala ya jimbo hilo.



Aidha Askofu Mtega mwenye umri wa miaka 68 alisema licha ya kustaafu kwake ataendelea kufanya majukumu ya kitume kama kawaida na amechagua kuishi SONGEA baada ya kustaafu huku akitaka wakatoliki wa jimbo hilo wasiwe na wasiwasi na uamuzi wake



 Baada ya saa kadhaa za maombi ya wandishi wa habari waliokua na kiu ya kuzungumza na Askofu Mkuu Mstaafu NORBERT MTEGA juu ya uamuzi wake wa kuomba kustaafu na hatimaye kukubaliwa na Baba Mtakatifu PAPA FRANCIS, hatimaye wakakutana nae majira ya jioni, na kwanza ilikua ni kutaka ufafanuzi wa kwa nini amechukua hatua hiyo iliyoshitua watu wengi



Askofu akajibu kuwa yeye anajitambua kuwa hana afya nzuri itakyomwezesha kusimamia shughuli zote kwa ufanisi kwa kuwa kunahitaji kufikiri kwa hali ya juu.



 Pili, waandishi wa Habari wakata kujua kwa nini afanye hivyo wakati umri wake wa kustaafu kwa hiari ambao ni miaka 70 hajafikia, wala kustaafu kwa lazima ambao ni miaka 75 hajafikia



 Tatu, tukataka kujua Askofu Mtega angependa Askofu Ajae afanye nini kwa maslai ya jimbo kuu katoliki la Songea



Askofu Mtega akajibu kuwa askofu atakayefika aendeleze kuimarisha imani za waumini bila kusahau huduma za kijamii kama vile elimu na afya.



 Aidha Askofu MTEGA amesema hakuna lolote baya lilisababisha yeye astaafu kazi hii ya kuhudumia jimbo kuu katoliki la Songea ambalo kiutawala linasimamia majimbo nane a ya kusini mwa Tanzania



 Kabla ya kuagana na Askofu Mtega, ikawa ni swali la wapi ataishi wakati wa kustaafu



 Askofu Mstaafu Norbert Mtega atoa ufafanuzi kuwa anapenda kuendelea kuishi hapa Songea.

UFAFANUZI WA ASKOFU MTEGA KUSTAAFU HUU HAPA


Baba Askofu Mstaafu Norbert Mtega, akijibu maswali ya waandishi wa habari mkoani Ruvuma leo.




MAAJABU::WAOMBOLEZAJI WAKIMBIA JENEZA BAADA YA MAITI KUFUFUKA NCHINI ZIMBABWE

Waombolezaji katika msiba nchini Zimbabwe walipigwa na butwaa pale mtu aliyekufa alipoamka wakati wakipita kando ya jeneza lake kutoa heshima za mwisho, shirika la habari za nchi hiyo limeripoti jana.

Brighton Dama Zanthe, mwenye miaka 34, aliingizwa ndani ya jeneza Jumatatu iliyopita baada ya kuwa amefariki nyumbani kwake baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Familia iliyojawa na huzuni ya mfanyakazi huyo wa usafirishaji ilifunika mwili wake kwa mablanketi na kufanya mipango ya kumhamishia kwenye mochari ya mjini humo, kwa mujibu wa  ripoti iliyochapishwa katika gazeti la The Herald.

Lakini siku iliyofuata marafiki wa Zanthe na jamaa zake walisambaratika wakiwa hawaamini pale alipoanza kutembea wakati wakipita mbele ya jeneza kuaga mwili wa 'marehemu' huyo.
Bosi wa 'marehemu' huyo, Lot Gaka alieleza kuhusu mkasa huo alipobaini mfanyakazi wake alikuwa bado angali hai.

Alisema: "Kwanza niligundua miguu ya Zanthe ikisogea wakati nilipokuwa kwenye ya foleni kutazama mwili wake. Hili lilinishitua mno. Kwanza sikuweza kuamini macho yangu lakini baadaye nilibaini kwamba kulikuwa na kusogea kwa viungo kadhaa katika mwili wake huku waombolezaji wengine wakiwa hawaamini kinachoendelea."

Gaka, ambaye anaendesha kampuni ya mabasi katika mji wa Gweru, alisema Zanthe alikuwa hana afya njema kabla ya 'kifo' chake wiki iliyopita.
Alielezea minsi alivyotembelea nyumbani kwa familia hiyo kutoa msaada pale mke wa mfanyakazi wake alivyompigia simu kumweleza kwamba Zanthe alikuwa amefariki.
Alisema: "Zanthe alikuwa katika likizo ya ugonjwa kwa kipindi fulani na kila mmoja kazini alikuwa akifahamu kwamba hali yake ilikuwa mbaya.

"Tulimtembelea nyumbani kwake.
"Sikushangaa pale nilipopokea simu kutoka kwa mke wa Zanthe Jumatatu usiku wiki iliyopita akisema kwamba mume wake alikuwa amefariki."

Aliongeza: "Nilitembelea maduka mawili yanayouza majeneza mjini humo kwa ajili ya kuulizia gharama kabla ya kuelekea nyumbani kwa Zanthe hivyo kuweza kuchukua mwili wake na kuuhifadhi katika mochari.

TUPE MAONI YAKO