17.05.2013
Askofu Mkuu Mstaafu wa jimbo Katoliki la
Songea Mhashamu NORBERT MTEGA amekutana na waandishi wa habari Mjini SONGEA
Mkoani RUVUMA kwa lengo la kutoa ufafanuzi juu ya uamuzi wake wa kumuomba Baba
Mtakatifu kustaafu na kusema amefanya hivyo kwa maslai ya jimbo kuu Katoliki la
Songea baada ya kubaini kuwa afya yake haimwezeshi kumudu majukumu ya kiutawala
ya jimbo hilo.
Aidha Askofu Mtega mwenye umri wa miaka 68
alisema licha ya kustaafu kwake ataendelea kufanya majukumu ya kitume kama
kawaida na amechagua kuishi SONGEA baada ya kustaafu huku akitaka wakatoliki wa
jimbo hilo wasiwe na wasiwasi na uamuzi wake
Baada
ya saa kadhaa za maombi ya wandishi wa habari waliokua na kiu ya kuzungumza na
Askofu Mkuu Mstaafu NORBERT MTEGA juu ya uamuzi wake wa kuomba kustaafu na
hatimaye kukubaliwa na Baba Mtakatifu PAPA FRANCIS, hatimaye wakakutana nae
majira ya jioni, na kwanza ilikua ni kutaka ufafanuzi wa kwa nini amechukua
hatua hiyo iliyoshitua watu wengi
Askofu akajibu kuwa yeye anajitambua kuwa
hana afya nzuri itakyomwezesha kusimamia shughuli zote kwa ufanisi kwa kuwa
kunahitaji kufikiri kwa hali ya juu.
Pili,
waandishi wa Habari wakata kujua kwa nini afanye hivyo wakati umri wake wa
kustaafu kwa hiari ambao ni miaka 70 hajafikia, wala kustaafu kwa lazima ambao
ni miaka 75 hajafikia
Tatu,
tukataka kujua Askofu Mtega angependa Askofu Ajae afanye nini kwa maslai ya
jimbo kuu katoliki la Songea
Askofu Mtega akajibu kuwa askofu
atakayefika aendeleze kuimarisha imani za waumini bila kusahau huduma za
kijamii kama vile elimu na afya.
Aidha
Askofu MTEGA amesema hakuna lolote baya lilisababisha yeye astaafu kazi hii ya
kuhudumia jimbo kuu katoliki la Songea ambalo kiutawala linasimamia majimbo
nane a ya kusini mwa Tanzania
Kabla
ya kuagana na Askofu Mtega, ikawa ni swali la wapi ataishi wakati wa kustaafu
Askofu
Mstaafu Norbert Mtega atoa ufafanuzi kuwa anapenda kuendelea kuishi hapa
Songea.
No comments:
Post a Comment