Monday, 2 September 2013

 Na Steven Augustino, Dodoma
Serikali Imekiri kuwa mfumo wa stakabadhi ghalani unakabiliwa  na
changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa usimamizi,uadilifu wa watendaji,
viongozi wa vyama msingi vya ushirika hali ambayo imesababisha
wakulima kuendelea kunyonywa na kudhurumiwa.

Hayo yamebainishwa jana Naibu waziri wizara ya Kilimo, chakula na
ushirika Adam Malima wakati alipokuwa anajibu  hoja za wajumbe wa
mkutano  wa siku mbili wa wadau wa tasnia ya korosho uliofanyika
mjini Dodoma.

Aidha Waziri Malima alisema kutokana  na changamoto hizo zote  wizara
imechukua jukumu la  kufanyiwa kazi, kwa kupeleka muswada wa kisheria
na wizara ya viwanda na Biashara, utagusia zaidi juu ya mfumo ili
kuboresha  kwa lengo la kuwaondolea adha wakulima wa zao hilo.

Akichangia mada hiyo katika mkutano huo Mkuu wa wilaya ya Liwale
Ephraim Mbaga alisema mfumo huu wa staabadhi ghalani umekosa mwelekeo
kutokana na  wakulima  kutolipwa fedha zao za malipo ya pili hali
iliyosababishwa  vurugu kwa baadhi ya  maeneo  hali iliyopelekea mali
za madiwani, mbunge kuchomewa moto katika wilayani Liwale.

Mmbaga alisema chanzo kikuu ni kutokana kutolipwa malipo yao ya pili
ya sh 600  kama ilivyotangazwa na bodi ya korosho katika msimu
uliyopita kwa visingizio kuyumba kwa soko la dunia.

Mwingine aliyepata nafasi ya kuwatetea Wakulima wa zao hilo alikuwa
Naibu waziri wa nchi  Tamisemi katika ofisi ya waziri mkuu Kassimu
Majaliwa na kusema kuwa umefika wakati wa idara husika kuridhia maombi
ya wakulima wa wilaya za Liwale, Nachingwea na Ruangwa ambazo
zimeazimia kujiondoa kutoka chama kikuu cha ushirika mkoa wa Lindi
Ilulu  waanzishe chama kwao.

Alisema ili mfumo huo wa stakabadhi mazao ghalani uweze  kuondoa
changamoto zilizokuwapo wakulima hao wameamua kuanzisha chama  kwa
lengo la kuboresha utekelezaji.

Naye Mkuu wa mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila alikiambia kikao hicho
kuwa mkulima anaanza kuibiwa kuanzia vyamavya ushirika alitoamfano
alikusanyiwa kilo kumi akilipwa fedha za kg Nane, kwa kama kuna
wakulima wapatao zaidi ya 100 wanachukuliwa zaidi ya kg 50 kwa hiyo
mtendaji wa ghala anakuwa na uwezo wa korosho zaidi ya tani 200 bila
ya kulima.

Mwananzila alisema vyama vya msingi havikuna wataalamu wa mahesabu
hali yo inasababisha kuingia mikataba na taasisi za fedha mwisho wa
siku wanakuwa na madeni ambayo yanakuwa  mali  ya wakulima ambayo
ulipa bila kushirikishwa

Mwishoooo

Friday, 30 August 2013

KUELEKEA SIKU YA MAHUJAA ASKARI WA JWTZ BRIGEDIA YA KUSINI YA FANYA USFI KATIKA MANISPAA YA SONGEA MKOANI RUVUMA

                                     Hapa ni katika ghuba lililopo katika soko la Manzese Songea
                                                     Takataka zilikuwa zinaziba barabara

                                                      Hapa ni hospitali ya mkoa wa Ruvuma


Thursday, 29 August 2013

WALEMAVU WAKUTANA RUVUMA KUTOA MAONI YAO YANAYOPENDEKEZWA KUINGIA KWENYE KATIBA MPYA


                                         Hapa wakiwa kwenye makundi kujadili maoni




                                                               Wanafunzi wa Songea boys

                                    Wanfunzi wa shule ya msingi luhila nao walishiriki

Tuesday, 27 August 2013

WANAFUNZI WA VYUO VIKUU FACULT YA JOURNALISM WALIPOTEMBELEA WILAYA YA NAMTUMBO MKOANI RUVUMA KWA MAFUNZO ZAIDI

                                          Mwenye shati jeupe ni Vicenti kazimoto kutoka UDSM

                   Mariamu Juma kutoka Sauti Mwanza na Rashid Issa kutoka UDSM
 Wa kwanza kushoto ni Rauph Mohamedi kutoka Musoma collage wakielekea kwenye ghala la Tumbaku

STORY YA PUNDA

Siku moja punda wa mkulima alianguka ndani ya kisima. Mnyama huyo alipiga kelele kinyonge kwa masaa kadhaa wakati mkulima akijaribu kufikiri nini cha kufanya.
 
Hatimaye, aliamua kwakuwa punda wake alikuwa mzee, na pia kisima hicho kilihitaji kufunikwa juu, Akaona hapakuwa na haja ya kumtoa.
 
Akaita majirani zake wote waje kumsaidia. Wao wote wakachukua makoleo na kuanza kuchota taka kwa koleo na kuzitupia ndani ya kisima.
 
Mara ya kwanza, punda aligundua nini kilikuwa kinatokea akapiga kelele kwa nguvu. Basi, ikawashanganza wale watu punda aliponyamaza ghafla!
Baada ya kutupa taka kadhaa kwenye hicho kisima. Huyo mkulima alishangazwa na kile alichokiona. Kwamba kila koleo la taka lililorushwa juu ya mgongo wa punda, punda alikuwa akifanya kitu cha kushangaza. Alikuwa akijitikisa ili taka zimwagike chini huku akipiga hatua moja kuja juu.

Kadri mkulima na majirani walivyoendelea kutupa uchafu kwa koleo juu ya punda yule, alizidi kutikisa mgongo wake na kupiga hatua moja kuja juu. Muda mfupi baadae, kila mtu alishangaa jinsi punda alivyozidi kutokeza ndani ya kisima na kuja juu.



FUNZO:
Maisha yatakutupia kila aina ya uchafu. Ili utoke nje ya kisima wahitaji kujitikisa na kuchukua hatua moja juu. Kila tatizo ulilonalo, ni jiwe la kukuwezesha kukanyaga na kupiga hatua kuja juu. Tunaweza kutoka nje ya kisima kirefu kwa kuongeza bidii ya kupiga hatua moja kuja juu bila kuacha na kutokata tamaa kamwe. Tikisa itikisa uchafu mbali na kuchukua hatua kuja juu.
Kumbuka kanuni 5 rahisi ili uwe na furaha:
1. Weka huru moyo wako mbali na chuki - Samehe.

2. Weka huru akili yako mbali na wasiwasi - Wengi hushindwa kabisa kipengele hiki.

3.Tosheka / rizika na ulichonacho.

4. Toa zaidi.

5. Tarajia vichache kutoka kwa watu lakini zaidi kutoka kwako mwenyewe
.

Una uchaguzi wa aina mbili ...
i) Tabasamu na funga ujumbe huu,
ii) au tuma ujumbe huu kwa mtu mwingine ili ashiriki somo hili

Imetumwa na: Dr. Emeria A. Mugonzibwa - Mwanga.
 

JESHI LA POLISI LAMWAGA AJIRA


JESHI la Polisi nchini, limetangaza ajira mpya kwa vijana waliohitimu kidato cha nne na sita mwaka jana. Taarifa za jeshi hilo, ambazo zimewekwa kwenye mtandao wa jeshi hilo, zinasema vijana katika mikoa yote wanatakiwa kufika kwenye ofisi za makamanda wa polisi mikoa kwa ajili ya usaili.

Taarifa hiyo, ilisema kila mkoa umepangiwa siku yake na kwamba kila kijana anapaswa kuwa na vyeti halisi vya elimu yake pamoja na cheti cha kuzaliwa. “Kwa wale wote walioomba nafasi hii, wanapaswa kufika kwenye ofisi husika, hasa vijana waliohitimu kidato cha nne mwaka 2012 na wale waliohitimu kidato cha sita mwaka 2013.

“Katika kundi hili, wapo waliochaguliwa wajitokeze kwenye usaili kabla ya kujiunga na jeshi la polisi,” ilisema taarifa hiyo.

“Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye kulingana na tarehe zinavyoonesha, ili mradi tu awe amejiridhisha kuwa ni miongoni mwa walioitwa kwenye usaili.

“Jeshi la Polisi, halitahusika na lawama yoyote ile kwa mtu atakayekwenda kwenye kituo cha usaili ilhali jina lake si miongoni mwa walioitwa kufanya usaili.

“Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili aje na vyeti vyake vyote vya masomo [(Academic Certificate(s)/Results slip(s) & Leaving certificate(s)], nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (Original Birth certificate). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo, ilisema kuwa kila mwombaji anapaswa kuwa na namba ya simu itakayotumika kumjulisha endapo atachaguliwa.

“Kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa usaili. Pia waombaji waje na kalamu za wino kwa ajili ya usaili wa kuandika.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema ni mapema kutoa idadi kamili ya vijana wanaotakiwa kwa sababu bado wapo kwenye mchakato.

“Siwezi kukwambia tunachukua wangapi, tumetangaza nafasi za kazi bado tupo kwenye mchakato… hii inategemeana na bajeti yetu tuliyonayo, tukikamilisha tutawaambia tu,” alisema Senso.

Monday, 26 August 2013

BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA BMT LAFANYA MAFUNZO YA WAAMUZI WA MICHEZO KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI NA MSINGI _RUVUMA

Na Mhaiki Andrew, Songea


BARAZA la michezo la Taifa(BMT) kwa kushirikiana na Mashirikisho matatu ya michezo ikiwemo Soka(TFF), riadha(RT) na wavu(TAVA) wataendesha mafunzo ya waamuzi wa michezo hiyo kwa wanafunzi wa Sekondari na shule za msingi mkoani Ruvuma, mafunzo hayo yanatarajia kuanza kufanyika (Jumatatu).


   Akizungumza na mwandishi wa habari hii  jana, Afisa Michezo,Utamaduni na vijana mkoa wa Ruvuma, Hassan Katuli alisema kuwa mafunzo hayo yatafanyika kwa siku nne kwa lengo la kuwapata waamuzi ambao watachezesha mashindano ya UMISSETA na UMISHUMTA kwenye ngazi ya mkoa.


   Alisema mafunzo hayo yatashirikisha wilaya zote sita za mkoa wa Ruvuma na Maofisa Michezo ndio walioachiwa majukumu ya kuraatibu na kuteua washiriki wa kushiriki mafunzo hayo kwa kuteua vijana kutoka shule za msingi na Sekondari katika wilaya zao,wilaya hizo sita kuwa Nyasa, Namtumbo, Tunduru, Mbinga, Songea Manispaa na Songea vijijini.


   Alisema kila wilaya itateua vijana 10 kuhudhuria mafunzo ya soka, 12 watahudhuria mafunzo ya uamuzi wa mpira wa wavu na wanafunzi 13 watapata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya uamuzi wa riadha ambayo yataendeshwa kwa vitendo na nadharia na wanafunzi ambao wanaotarajia kumaliza elimu ya msingi na Sekondari hawataruhusiwa kuhudhuria mafunzo hayo.


  Katuli, pia alisema Afisa michezo  hatakaye shindwa kuteua wanafunzi wa kuhudhuria mafunzo hayo kutokana na chuki zake binafsi alidai ofisi ya Mkuu wa mkoa itamchukulia hatua kwa kumwajibisha kwa kufuata misingi ya utumishi wa umma, ili kuweza kudhibiti uzembe ambao unaweza kujitokeza na kuwepo na visingizio vya kushindwa kutekeleza hilo


    Alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa wanafunzi kwani yatakuwa yanamjengea uwezo na hamasa ya kupenda michezo kwa kujiendeleza baadaye, punde atakapomaliza elimu ya msingi na Sekondari , badala ya kutegemea kuomba waamuzi kutoka kwenye vyama na kwenda kuchezesha mashindano ya UMISSETA na UMISHUMTA kila mwaka.


MWISHO

TUPE MAONI YAKO