Mtumishi
katika mnara wa Canton, mrefu kuliko yote nchini China na watatu
duniani kwa urefu, Sarah Xie, akimuonyesha mandhari ya jiji la
Guangzhou, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati Kinana na
ujumbe wake walipopanda hadi mwisho mnara huo wenye urefu wa zaidi ya
futi 100, Machi 13, 2013. Wengine Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya
Maganga Sengelema na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine shigella. Kinana na
ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko
wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC). (Picha na Bashir Nkoromo). Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakitazama maumbo ya
mandhari ya mji wa Guanzhou, China, yaliyopo ndani ya mnara wa Cnton
wenye urefu wa zaidi ya mita 100, walipotembelea mnara huo, Machi 13,
2013. Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya
kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC). (Picha
na Bashir Nkoromo).
Katibu
wa NEC, Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kushoto) na
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa mjini Magharibi, Yussuf Mohamed Yusuf wakitaza
bidhaa zinazouzwa kwenye kilele Mnara wa Canton ambao ni mrefu kuliko
yote nchini China ukiwa na urefu wa zaidi ya mita 100, mjini Guangzhou,
China. Dk. Asha-Rose Migiro na Yusuf ni miongoni mwa viongozi
walioambatana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika ziara ya
siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China
(CPC). (Picha na Bashir Nkoromo).
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi na wanachama wa Jumuia ya watanzania waishio nchini China
NA BASHIR NKOROMO, DONGGUAN,CHINA
CHAMA Cha Kikomunisti cha China
(CPC) kimeeleza matumaini yake kwamba upo uwezekano wa Tanzania kupiga
hatua kubwa kichumi kama inajikita kwa dhati katika kuzitumia rasilimali
ilizonazo ikiwemo ardhi.
Hayo yalisemwa Machi 13, 2013 na
Kamishna wa Maadili na nidhamu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC),
jimbo la Donguan, China, Cuo Jian, wakati akizungumza na Katibu Mkuu
wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, katika hoteli ya Exhibition
Internation mjini hapa.
Jian ambaye pia ni Meya wa jiji la
Donguan, alisema, Tanzania kama zilivyo nchi kadhaa za Afrika, inaweza
kupiga hatua kiuchumi ikiwekeza juhudi zake katika kuzitumia rasilimali
ilizonazo kwa kuwa rasilimali ndiyo msingi wa kwanza katika kuinua
uchumi wa nchi yoyote.
Alisema, anatambuwa kwamba
Tanzania ni moja ya nchi za Afrika zenye ardhi kubwa, hivyo haina budi
juhudi zake za kuinua uchumi kuzielekeza katika rasilimali hiyo
ikiitumia kwa kilimo cha kisasa, kujenga viwanda na vitegauchumi
mbalimbali ambavyo vitachochea kukua haraka kwa uchumi.
“Hata hivyo nawapongeza Tanzania,
kwa hatua mliyofikia sasa katika kukuza uchumi, asilimia sita ya GDP,
inaridhisha, la msingi serikali kuongeza juhudi na kuwahamasisha
wananchi kushiriki katika juhudi hizo”, alisema, Jian.
Akijibu swali na Mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Simiyu, ambaye yupo kwenye msafara wa Kinana katika ziara hiyo,
Titus Kamani aliyetaka kujua ni nini hasa China ilifanya hadi kuufanya
uchumi wake ukue haraka na kuwa nchi ya pili dunia kwa maendeleo, Jian
alisema, China imefikia mafanikio hayo kutokana na kuamua kuwekeza kwa
nguvu zake zote kwenye rasilimali ya ardhi.
“Zipo njia nyingi za kuweza kuinua
uchumi wa nchi yoyote, juhudi hizo baadhi zinafanana na nyingine ni
tofauti kutokana na nchi na nchi, lakini sisi (Wachina) tulifahamu
kwamba tuna ardhi kubwa sana, hivyo tukaamua kuimua rasilimali hii kwa
kila namna iliyo bora. Licha ya eneo kuwa kubwa lakini tumehakikisha
hakuna eneo linaloachwa bila faida”, alisema.
Kwa upande wake Kinana aliupongeza
uongozi wa China chini ya chama cha CPC na wananchi wa nchi hiyo kwa
kuweza kufanikisha kuinua uchumi wa nchi hiyo kwa kiwango kibwa cha
sasa.
“Bila shaka ni uchapakazi usio na
kikomo na wakujituma sana kwa pamoja kati ya serikali na wananchi ndiyo
maana mmefanikiwa hivi, napenda kuchua fursa hii niwapongeze kwa dhati
kwa mafanikio haya, nasi kama nchi rafiki tunapata kiu kubwa kuhakikisha
tunafika mlipo au angalau kuwakaribia”, alisema Kinana.
Kinana yupo nchini China
akiambatana na ujumbe wa viongozi na maofisa wa Chama kwa ajili ya ziara
ya mafunzo, katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kisiasa, na pia
kudumisha urafiki wa kindugu wa siku nyingi kati ya Chama Cha Mapinduzi
na Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo.
Katika ziara hiyo Kinana
amefuatana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai, Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM, Khadija Aboud, Katibu wa NEC, Siasa na Uhuaisno
wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa
CCM, Martine Shigela, Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi, Khamis Suleiman
Dadi na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi Mohammed Yusuf
Mohamed.
Wengine ni Mwenyekiti wa CCM mkoa
wa Iringa, Jesca Msambatavangu, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Titus
Kamani, Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengelema na maofisa wa
Chama. ziara hiyo
Kinana anafanya ziara hiyo
kutokana na mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China, na anafanya
ziara hiyo ikiwa ni ya kwanza kuifanya nje ya nchi, tangu alipoteuliwa
kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Oktoba mwaka jana mjini Dodoma