Friday, 29 March 2013

RAIS KIKWETE AFIKA ENEO LA TUKIO NA KUSHUHUDIA HALI HALISI YA KUANGUKA KWA JENGO LA GHOROFA 16 JIJINI DAR,HALI YA UOKOAJI UNAENDELEA


Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mbunge,Mh Mbatia muda mfupi mara baada ya kufika na kujionea hali halisi ya jengo la Ghorofa lililoporomoka mapema leo asubuhi na kupelekea watu wawili kupoteza maisha na wengine 17 kujeruhiwa vibaya.,aidha shughuli za ukoaji zinaendelea kwani inadaiwa kuna watu wengi zaidi wamefunikwa na jengo hilo.


Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar Es Salaam,Mh Said cMeck Sadick shoto akiwa ameambatana na Rais Jakaya Kikwete muda mfupi mara baada ya kufika na kujionea hali halisi ya jengo la Ghorofa lililoporomoka mapema leo asubuhi na kupelekea watu wawili kupoteza maisha na wengine 17 kujeruhiwa vibaya,kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.

Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadcik akifafanua jambo kwa Rais Jakaya Kikwete muda mfupi mara baada ya kufika na kujionea hali halisi ya jengo la Ghorofa lililoporomoka mapema leo asubuhi na kupelekea watu wawili kupoteza maisha na wengine 17 kujeruhiwa vibaya,kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.

Rais Kikwete akiondoka eneo la tukio mara baada ya kujionea hali halisi ya tukio zima la kuanguka kwa ghorofa linalodaiwa kuwa na idadi ya ghorofa 16.



Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadick akipewa pole na Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.Dkt.ASha-Rose Migiro kuhusiana na tukio zima la kuanguka kwa jengo la Ghorofa mapema leo asubuhi,jijini Dar

Kikosi cha Jeshi kikiwasili eneo la tukio kusaidia shughuli ya uokoaji.




Gari lililokuwa karibu na jengo hilo likiwa limebonyezwa kama chapati likitolewa eneo la tukio kuweza kuwato majeruhi waliofunikwa na kifusi cha gorofa hilo.



Gari lililokuwa limegandamizwa baada ya jengo hilo kuporomoka likinyanyuliwa na winchi.. 

Ni moja ya Kifaa pekee kilichokuwepo eneo hilo Trekta, likifukua kifusi ili kuokoa watu wanaodaiwa kufukiwa na kifusi hicho.

Baadhi ya watu waliwahi kufika kujaribu kutoa msaada bila mafanikio hapa wakiwa wamekwama baada ya kukosa vifaa vya kutosha.

Wahindi nao walikuwapo kutoa msaada hapa wakilielekeza Trekta kusogea mahala walipo wao wakihisi kuwa kuna mtu mahala hapo.

Waokoaji wakijitahidi kutumia mikono kuondoa kifusi hicho ili kuweza kuwaokoa watu waliofukiwa

Trekta likiendelea kuondoa kifusi hicho.

Waokoaji wakiwa hoi......


Juhudi zinaelekea kulala.........

Moja kati ya magari yaliyokuwa eneo hilo likiwa limeangukiwa na mabaki ya jengo hilo.

Trekta likiendelea kuondosha kifusi.

Sehemu ya wananchi wakishuhudia tukio hilo.

Vijana wakishusha mitungi ya gesi ili kuwasaidia kukata nondo.... baada ya kuona vimekosekana vifaa vya haraka.




Changamoto ya uokoaji ni ngumu, lakini vikosi mbalimbali vinaendelea na zoezi hilo, ili kunusuru maisha ya waliofukiwa na kifusi.

Hizi nia aina ya nondo ambazo kimsingi sio imara kuweza kuhimili ujenzi wa ghorofa ndefu kama hili, kuna haja mamlaka husika likatupia macho kampuni za ujenzi ili kuokoa maisha ya wajenzi na watumiaji wa majengo hayo

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO