Wakazi wa
wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wamelalamikia uharibifu mkubwa wa mazao yao ya
mahindi na mpunga unaofanywa na mifugo aina ya ng'ombe walioingizwa wilayni
humo kinyume na sheria.
Akizungumza
kwa niaba ya wakazi wa wilaya ya Tunduru mkuu wa wilaya hiyo ABDALLAH LUTAVI
amesema ng'ombe hao wameenea katika maeneo mabalimbali ya vijiji na kushambulia
mazao ya wakulima.
Amesema
serikali imeanza kuchukua hatua dhidi ya wale wanaolisha mifugo yao katika
mashamba ya watu na kuomba kikao hicho kiweke mkakati wa haraka kuzuia
uingizwaji wa mifugo hiyo ili kujiepusha na njaa inayoweza kutokea kutokana na
mazao kushambuliwa na mifugo hiyo.
Mkuu wa
wilaya ya Namtumbo ABDALLAH LUTAVI alikuwa akizungumza katika kikao cha ushauri
cha mkoa wa Ruvuma kilichofanyika katika manispaa ya Songea.
Naye mbunge
wa Jimbo la Namtumbo Mheshimiwa vita kawawa amesema ng!ombe hao wakiachwa kwa
kipindi cha mwaka mmoja tu basi wilaya hiyo itakosa kabisa mazao.
No comments:
Post a Comment