Mbunge wa jimbo la Namtumbo VITA KAWAWA wa kwanza kulia , katikakti ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya namtumbo bwana kinana
kulia ni mkurugenzi wa wilaya ya mbinga na mbunge wa jimbo la mbinga mashariki Gaudence Kayombo wakisikiliza jambo katika kikao cha ushauri cha mkoa.
Serikali
mkaoni Ruvuma imepiga marufuku kuuza kanda zinazoenezanchuki na kuchochea
masuala ya vurugu katika mkoa wa Ruvuma.
Mkuu wa mkoa
wa Ruvuma SAID MWAMBUNGU amepiga marufuku vitendo hivyo katika kikao cha
ushauri cha mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa Songea club katika manispaa ya
Songea.
Amesema
serikali haitamvumilia mtu , kundi au kiongozi yeyote wa dini ama siasa
atakayeonekana kuchochea machafuko na chuki miongoni mwa wananchi katika mkoa
wa Ruvuma.
Ameongeza
kuwa serikali kupitia jeshi la polisi itamkamata mtu yeyote mchochezi na
kumfikisha mbele ya sheria bila kujali nafasi yake.
Mkuu huyo wa
mkoa wa Ruvuma ametumia nafasi ya kikao hicho kuwaomba wakazi wa mkoa wa Ruvuma
kushirikianan na serikali ili kuwafichua na kuwabaini wanaouza kanda za uchochezi
za aina yeyote zinazoeneza chuki za kidini.
Aidha
amewataka viongozi wa dini ya kiislamu na wakristo kupitia misikiti na makanisa
kuhubiri upendo ,amani, na utulivu miongoni mwa wananchi.
Said
Mwambungu amewasihi wakazi wa Ruvuma kudumisha amani, upendo, utulivu na
mshikamano wa kitaifa.
No comments:
Post a Comment