Kikao cha kamati cha ushauri cha mkoa wa Ruvuma
kimewaagiza viongozi wa kila wilaya kuhakikisha wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga na kidato cha kwanza kwenda kuripoti shuleni kabla ya mwisho wa mwezi
huu.
Agizo hilo limetolewa na wajumbe wa kikao hicho baada ya
kupata taarifa kutoka kwa afisa elimu wa mkoa wa Ruvuma Mayasa Hashimu kuwa
jumla ya wanafunzi 6300 waliofaulu hawajaripoti shuleni mpaka leo.
Hivyo kikao kikalazika kuwaomba viongozi kila mmoja
kutumia nafasi yake kuwabana wazazi ambao hawajawapeleka watoto wao kuripoti
shuleni.
Wajumbe wa kikao hicho wametoa muda kuwa mwisho wa
kuripoti wanafunzi wote wasioripoti shule ni tarehe 20.3.2013,
Itakapofika tarehe hiyo kila mkuu wa wilaya anatakiwa
kutoa taarifa ya wanafuznzi ambao bado hawajaripoti shuleni na wazazi wao wamechukuliwa hatua gani za
kisheria.
Akizungumzia sakata la wanafuzi wa kidato cha nne kufanya
vibaya katika matokeo ya mtihani wao afisa elimu mayasa hashimu amesema baada
ya kufanya utafiti amegundua kuna changamoto nyingi sana katika pande zote za
wazazi walimu wanafunzi na serikali.
Kwa upande wa wazazi afisa elimu amesema wazazi wengi
wanasahau wajibu wa kuona umuhimu wa watoto kwenda shule na kuhakikisha watoto
wanhudhuria shule kila siku, kuwaandalia vifaa vya shule kama vitabu na
kuhakikisha watoto wao wanapata chakula cha mchana.
Aidha wazazi pia wanatakiwa kutoa michango inayopitishwa
na kamati za shule au bodi ya shule.
Pia wazazi wametakiwa kujenga tabia ya kufuatilia
maendeleo ya shule ya watoto wao na kukagua mahitaji yao na kubwa zaidi
kuwajenga watoto katika maadili mema kwa kuhakikisha wavaa mavazi mazuri na
kuwapatia mahitaji muhimu ya shule.
Afisa elimu huyo aliomba marufuku kuwa ngoma ya saka mimba ambayo ipo katika
wilaya ya Tunduru ambayo inahamasiha watoto kupata mimba.
Kwa upande wa wanafunzi amewataka wajitambue na wawe na
malengo na kujua nafasi yao katika jamii na kujijengea tabia ya kujisomea na
kutembelea maktaba.
Akiwageukia walimu amewataka wafanye kazi zao kwa
uaminifu, watoe notes zinazoendana na mihutasari,walimu watoro wafikishwe
kwenye vyombo vya sheria.
Akizungumzia serikali kuwajibika kwa upande wake kuhusu
elimu amesema serikali inapaswa kuwasikiliza walimu matatizo yao na kuwasaidia
pale wanapokuwa na shida.
No comments:
Post a Comment