Hivi ndivyo hali ya mtoto Simon Mlope ilivo kwa sasa
Mtoto Simon Mlope akiwa na mama yake ambaye anaitwa Amina Ally
Angalia Video ya mtoto Simoni Mlope akiwa na Mama yake.
Mtoto simon Mlope mwenye umri wa miaka 11 mkazi wa eneo la mahenge katika manispaa ya songea mkoani Ruvuma amelazimika kukatisha masomo yake ya shule ya msingi akiwa darasa kwanza kutokana na mototo huyo kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo .
Awali tulitoa habari za mtoto huyu akiomba msaada
lakini hadi sasa bado hajapata msaada wowote ule wa kuweza kuokoa maisha yake.
Nahivi sasa hali ya mtoto huyu inazidi kuwa mbaya kiafya .
Mtoto simon Mlope alikubwa na ugonjwa moyo tangu mwaka 2001 mara baada ya
kuzaliwa na kugundulika kuwa moyo wake una tundu hali ambayo
inasababisha kuvuta pumzi kwa shida.
Mama wa mototo simon mlope anayeitwa AMINA ALLY
anawaomba watanzania kumsaidia mtoto wake fedha za matibabu Baada
ya kuambiwa na madaktari kuwa simon anatakiwa kwenda nchini india
kutibiwa,baada ya kupata rufaa kutoka muhimbili mwaka 2006 huku familia
yake ikiwa haina uwezo kabisa.
Majirani wa familia ya simon nao wanasema kuwa mototo
simon anahitaji msaada wa haraka kwa kuwa hali yake sio nzuri na kuwaomba
watanzania wamsaidie.
Kinachosikitisha zaidi baba wa mtoto huyo
anayejulikana kwa jina la SIMON MLOPE ameondoka nyumbani hapo tangu mwaka
2011 na hajulikani aliko kwa sasa, ingawa mwanzoni alisema yuko nchini
Msumbiji.
Kwa anayeguswa na tatizo hili na anataka kumsaidia
SIMONI MLOPE atumie simu namba 0752732290
Picha na habari kwa hisani ya http://demashonews.blogspot.com
No comments:
Post a Comment