Friday, 8 March 2013

MKURUGENZI WA MAFUNZO YA UFUNDI JESHI LA KUJENGA TAIFA KANALI CHACHA WANYANCHA AFUNGA MAFUNZO YA UZALISHAJI UMEME KWA KUTUMIA NISHATI ITOKANAYO NA BAYOGESI (JKT MLALE)


Mkurugenzi wa mafunzo ya ufundi Jeshi la kujenga Taifa Kanali Chacha Muninka Wanyancha

Injinia wa Wakala wa Nishati Vijijini Enocent Nyemoakitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa mafunzo ya ufundi Jeshi la kujenga Taifa Kanali Chacha Muninka Wanyancha kuhusu mtambo utakao wekwa katika shimo lililochimbwa kwa ajili ya kuweka mtambo.
 Mkurugenzi wa mafunzo ya ufundi Jeshi la kujenga Taifa Kanali Chacha Muninka Wanyancha akisikiliza melezo toka kwa mkuu wa Kambi ya JKT Mlale

..................................................................


Katika hafla ya kufunga mafunzo hayo Kanali Chacha Wanyancha  amewataka wahitimu watambue kuwa wanalo jukumu kubwa mbele yao baada ya kupata mafunzo ya uzalishaji umeme kwa kutumia nishati jadidifu itokanayo na Bayogesi kwa kuwa wao ndio watakaokuwa chachu ya uhamasishaji wa matumizi bora na sahihi ya nishati jadidifu katika  maeneo yao baada ya kuhitimu mafunzo haya. 

“Kufanya kwa mafunzo haya kutawezesha kufikia malengo ya Milenia, MKUKUTA na sera ya Taifa ya Nishati ambayo yanalenga katika upatikanaji wa nishati bora kwa lengo la kukuza uzalishaji mali na kuendeleza huduma za  jamii, pia  kutokana na mafunzo waliopata yatasaidia kupatikana kwa huduma bora za nishati mbadala na endelevu kutachochea kuchangia katika kupunguza  umaskini na uharibifu wa mazingira ambayo kwa sasa ni tatizo kubwa.

Katka  hutuba yake  Kanali Chacha Muninka amezitaja changamoto mbalimbali zinazowakabili wadau kwenye uendeshaji wa vyanzo vya nishati vijijini, kamavile ukosefu wa mitaji, uwezo mdogo wa kiutaalamu  na wa kiufundi, mabadiliko ya hali ya hewa  na athari za mazingira pia kutojua fursa zilizopo katika uwezeshwaji wa kuanzisha miradi ya aina hii. Changamoto hizi zinaweza  kumalizika iwapo kutakuwa na  ushirikiano wa karibu na wadau , wakala wa Nishati Vijijini na Taasisi za ndani na nje zinazojishirikisha  na nishati vijijini na masuala ya mazingira.

Naye Inocent Msua  amesema kuwa wakala wa Nishati vijijini wanatoa ruzuku kwa waendelezaji wa miradi ya nishati vijiji kama sehemu yake ya kuchangia  kukabiliana  na tatizo la mitaji. Wakala  hawa wa Nishati Vijijini wamekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha mabenki na taasisi nyingine za fedha za ndani na nje ya nchi kutoa mikopo yenye riba na masharti nafuu kwa waendelezaji wa miradi ya nishati vijijini hapa Tanzania.
Pia ameongezea kuwa tayari mpango huu kwa sasa unatekelezwa na benki za TIB,CRDB,NBC,NMB,TWIGA BANCORP na AZANIA. 
 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO