Thursday, 7 February 2013

TUZO ZA WANAWAKE WENYE MAFANIKIO TANZANIA 2013 ZAZINDULIWA



Mwenyekiti wa kamati ya TWAA Bi Sadaka Gandi akiongea na Waandishi wa Habari Leo
----
DAR ES SALAAM, TANZANIA, – Taasisi ya Tanzania Women of Achievement (TWAA) imezindua Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania msimu wa 2013 zilizopangwa kufanyika katika siku ya wanawake duniani tarehe 8 Mwezi Machi mwaka huu. Tuzo hizi ambazo hufanyika kila baada ya miaka miwili zilizinduliwa mwaka 2009 kwa heshima ya wanawake katika sekta mbalimbali nchini kote ambao kupitia kazi zao wamechangia kwa kiasi kikubwa sana kuleta maendeleo ya jamii zao kwa njia moja au nyingine.
"TWAA inataka kutambua wanawake, waishio Tanzania ambao kupitia kazi zao wameweza kupata mafanikio makubwa sit u kibinasi bali wametumia nafasi zao kuleta maendeleo na mabadiliko ya kimsingi kwenye jamii zinazowazunguka." Alisema Mkurugenzi mkuu wa TWA Bi. Irene Kiwia. "Tuzo hizi mbazo sasa ziko katika msimu wake wa 3 zinatoa fursa nzuri ya kutambua na kupongeza wanawake ambao wamechangia sana kwenye kubadilisha na kuboresha sura ya Tanzania. Kwa wanawake wengi hii itakuwa mara ya kwanza mafanikio na michango yao imetunukiwa na hili ni jambo la kufajiri na kuridhisha sana.”

Vipengele vya tuzo za mwaka huu ni Sanaa na Utamaduni, Biashara na Ujasiriamali, Habari na Mawasiliano, Michezo, Professional (Kazi), Elimu, Afya, Ustawi wa Jamii, Sayansi na Teknolojia, Sekta ya Umma, Kilimo na Mshiriko Mdogo.
Bi Sadaka Gandi, mwenyekiti wa kamati ya TWAA alitoa wito kuwa "tunawasihi mashirika, vyama, wanawake na wanaume kote Tanzania kuteua wanawake wenye mafanikio katika makundi haya na kuonyesha mchango wao katika uwezeshaji wa wanawake. Kuna maelfu ya wanawake wastahili wa tuzo hizi huko nje ambao ni mawakala wa mabadiliko katika jamii zao. Tunataka kuimba mapambio ya mashujaa hawa na kuhamasisha mamilioni ya wanawake wengine wa Tanzania kuiga mifano na kupata msukumo wa kuleta mabadiliko. Kamati ilipokea fomu za nyingi sana za washiriki miaka ya nyuma na hivyo basi tunategemea ushiriki mzuri zaidi mwaka huu. "

Kamati ya TWAA inawajumuisha Bi Mary Rusimbi - Mwanaharakati na Mwanzilishi wa Programu ya Mtandao wa Jinsia Tanzania, Jaji Joaquine De Mello - Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Dk Marcelina Chijoriga- Mkurugenzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bi. Ludovicka Tarimo – Mtaalamu wa Jinsia kutoka USAID, Bwana. Innocent Mungy-Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Sadaka Gandi - Mwanasaikolojia na mfanyakazi za Jamii, Irene Kiwia - Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya mahusiano ya jamii Frontline Porter Novelli. Huko nyuma tuzo hizi zilidhaminiwa na Baileys, Delloite, NBC, Home Shopping Center, TCRA, Songas, Watu wa Marekani, DTP, UN DPG Gender Group, UNFPA, UNESCO, TBL, Multichoice, African Life Assurance, Barrick, Twiga Cement, Vodacom, Farm Equip, RBP, Clouds FM na Frontline Porter Novelli.

KUHUSU TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA)
TWA ni taasisi isiyo ya kiserikali, ya hiari na kujitegemea inayojihusisha na uwezeshaji wa wanawake iliyoanzishwa mwaka 2009. Lengo kuu la TWA ni kuimarisha ushiriki, na majukumu ya wanawake na uwezo wao katika jamii ya Tanzania kwenye mabo ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. TWA inafanya kampeni, mafunzo, semina, mikutano na warsha ambazo zinakuza ubadilishanaji wa taarifa na ushauri kwa wanawake na wasichana wadogo wa Kitanzania.
Kampeni na mafunzo haya yanalenga zaidi haki za binadamu na za wanawake, usawa wa kijinsia, ushiriki wa wanawake kweye shughuli za kiuchumi na kijamii.Kazi kubwa ya TWA ni kuboresha maisha, kupanua fursa, na kuwasaidia wanawake katika Tanzania kushamiri na kuchangia kwenye ustawi wa nchi. TWA inafanya kazi na viongozi ,watu binafsi, jamii, mashirika yasiyo ya kiserekali, serikali, sekta binafsi na wafadhili wa nje kujenga ufanisi na kuhakikisha malengo ya kuendeleza wanawake yanafanikiwa. Sisi ni kosa kwa maendeleo ya Tanzania kuendelea mpaka kila mwanamke anakuwa mabadiliko. Tumejikita kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea na wanawake ni chachu ya maendeleo hayo.

Wazazi mkoani Lindi watakiwa kusimamia maendeleo ya elimu ya watoto wao



Mama Salma Kikwete akihutubia mamia ya wananchi wa mkoa wa Lindi waliohudhuria sharehe za kutimiza miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi zilizofanyika kimkoa katika kijiji cha Rondo kata ya Chiponda mkoani Lindi tarehe 5.2.2013. PICHA/JOHN LUKUWI   
***************************
Na Anna Nkinda – Maelezo , Lindi

Wazazi mkoani Lindi wametakiwa kusimamia elimu ya watoto wao kwa kuhakikisha kuwa wanaenda shule, wanakagua madaftari yao na kuwarekebisha  pale ambapo wamekosea kwa kufanya hivyo  watafaulu  vizuri katika masomo  na kufanikiwa kimaisha kwani elimu ni msingi wa maendeleo.

Wito huo umetolewa jana na mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizofanyika kimkoa katika kata ya Rondo wilaya ya Lindi  vijijini.

Mama Kikwete ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa toka wilaya ya Lindi mjini alisema kuwa maendeleo ya elimu si mazuri katika mkoa huo hivyo basi kina baba washirikiane na wake zao kuhakikisha kuwa watoto wanahudhuria shule na kufanya vizuri katika masomo yao.

“Ninyi watoto nawasihi msome kwa bidii mkumbuke kuwa huu si wakati wa mtoto kukatisha masomo kwa ajili ya kupata ujauzito  kwani mkiwa na elimu kutakuwa  na uhakika wa kupatikana kwa wataalamu mbalimbali katika mkoa huu na kutatua tatizo la kutokuwa na  wataalamu ambalo limedumu kwa muda mrefu”, alisema Mama Kikwete.

Aidha Mjumbe huyo wa Halmashauri kuu ya CCM taifa aliwataka wanawake kutosubiri nafasi za upendeleo za viti maalum bali wagombee nafasi mbalimbali za uongozi ndani na nje ya chama  ili wafike katika ngazi ya maamuzi na kuachana na fikira kuwa wao hawawezi kumwaga sera wakati wa uchaguzi.

Alimalizia kwa kuwataka  wakazi wa mkoa  huo kudumisha amani, upendo na utulivu, kufanya  kazi kwa bidiii, maarifa na kujituma, wakulima walime kilimo cha kisasa ambacho kitawafanya wavune mazao mengi zaidi pia wafanyakazi  watumie muda wa kazi kufanya kazi na kuwahudumia wananchi.

Mama Kikwete pia alifungua jengo la ofisi ya CCM lenye thamani ya shilingi milioni 35 ambalo limejengwa na Mbunge wa jimbo la Mtama ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe.

Waziri Membe alisema kuwa jengo hilo lina vyumba sita ambavyo ni  ofisi za jumuia zote za chama hicho ambazo ni Vijana, Wanawake, Wazazi, pia kuna ofisi za Mbunge, Mjumbe wa NEC na chumba cha mikutano.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo  Ally Mtupa aliwataka wanachama wa chama hicho  kuwa na  mahusiano mazuri baina yao na  viongozi wanaowaongoza. Wakisikia jambo wasiwe na papara ya kukimbilia kuandamana bali wafanye upelelezi kwanza na wakishabaini ukweli ndipo wachukue hatua.

Mtupa alisema, “Hivi sasa kuna watu wanapita mitaani na kupotosha ukweli kuwa Serikali yetu haijaleta maendeleo, wamesahau kuwa wanatembea katika barabara na kutibiwa   katika Hospitali zilizojenga na CCM, tunawaomba watu hawa wawaheshimu viongozi wanaotawala kwani hata vitabu vya dini  vinasisitiza umuhimu wa kuwatii viongozi waliopewa mamlaka ya kutawala”.

Sherehe hizo zilienda sambamba na mchango wa matembezi ya mshikamono ambapo zaidi ya shilingi milioni mbili zilipatikana, ufunguzi wa ofisi za CCM, ufanyaji wa usafi wa mazingira , kuwatembelea wagonjwa mahospitalini, utoaji wa kadi kwa wanachama wapya ambapo wanachama wa kawaida 286 , jumuia ya wazazi 63 na kutoka vyama vya upinzani 23 walipewa kadi. 

SHEREHE YA KUTANGAZA VIVUTIO SABA VYA ASILI BARANI AFRIKA KUFANYIKA JIJINI ARUSHA TANZANIA TAREHE 11 FEBRUARY 2013


images
Sherehe za kutangaza vivutio vya asili vya bara la Afrika zinategemea kufanyika katika hoteli ya Mt Meru katika jiji la Arusha Tanzania tarehe 11 February 2013 kuanzia saa nane mchana.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Bodi ya Utalii Tanzania viongozi mbali mbali wa kitaifa na kimataifa ambao wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo ambayo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda. 

Rais wa Taasisi iliyoendesha shindano hilo la kutafuta Maajabu hayo Saba la Seven Natural Wonder Dr Philip Imler kutoka Marekani anatarajiwa kuwasili tarehe 9/2/2013 tayari kutangaza vivutio Saba vya Asili vya bara la Afrika.

Tanzania ilikuwa na vivutio vitatu vilivyoingia kwenye kinyanganyiro hicho ambavyo ni Mlima wa Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro na wanyama wanaohama wa Seregeti. Tanzania imekwisha tajwa kuwa miongoni mwa washindi ambao angalau kivutio kimoja ama zaidi Saba ya Asili Afrika.

Macho na masikio ya watanzania ni kujua ni kivutio au vivutio gani hivyo vya Tanzania vimeweza kushinda.

Wednesday, 6 February 2013

SIKU YA MADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA NCHINI KANDA YA SONGEA YAFANA

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma bw:Said Mwambungu
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu amewataka wakazi wa mkoa wa Ruvuma kukataa kwa nguvu zote kuchochewa  kufanya fujo na kusababisha kumwagika kwa damu  za watu wasiokuwa na hatia.

 Mkuu huyo wa mkoa wa Ruvuma ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini yaliyofanyika katika viwannja vya mahakama kuu kanda ya Songea katika manispaa ya Songea.
Kaimu jaji mfawidhi Hamisa Kalombola
Said mwambugu amesema wakazi wa Ruvuma wakikubali kushawishiwa kufanya fujo ndipo watu wanapojichukulia sheria mkononi wakati vyombo vya sheria vipo.
Amesema tabia ya watu kujichukulia sheria mkononi inapaswa kupingwa kwa nguvu zote kwa kuwa vitendo hivyo vinavunja amani ya nchi.

Kaimu jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Songea mheshimiwa Hamisa Kalombola Kuna madhara makubwa ya watu kupuuza utawala wa sheria mfano wananchi wanaojiita wenye hasira na kujichukulia sheria mkononi, na kuua na kujeruhi watu ambao hawana hatia.
Jaji Kalombola amesema utawala wa sheria una umuhimu katika jamii kwa kuwa unaleta usawa kati ya watawala na watawaliwa na ndio maana hata serikali ikikosea inafikishwa mahakamani.
 Baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya siku ya sheria Jaji wa mahakama kuu kanda ya Songea alikagua gwaride .
  

Monday, 4 February 2013

BALOZI MPYA WA UINGEREZA ATUKUZA TABIa YA WATANZANIA

3-Mh Balozi Dianna Melrose akisema machache 27d4a
                                        
5-Mh Balozi Dianna Melrose akifanya mahojiano na wanahabari Freddy Macha  na Urban Pulse  1 1664a
 Balozi Dianna Melrose akifanya mahojiano na mwanahabari Fredy Macha,na Urban Pulse
Picha na Urban Pulse
Na: Freddy Macha
Balozi mpya wa Uingereza nchini Tanzania, Mheshimiwa Dianna Melrose ameeleza furaha yake kuteuliwa kufanya kazi nchini kwetu na kukiri kwamba anauchangamkia wadhifa huo atakaouanza karibuni.Balozi Melrose alikuwa akiongea katika sherehe ya chakula cha jioni iliyofanywa kwa heshima yake nyumbani kwa Balozi wetu wa Uingereza mheshimiwa Peter Kallaghe na mkewe Joyce Kallaghe jijini London Alhamisi iliyopita “Nimebahatika sana.” Alikiri Mama Melrose. “ Watanzania ambao nimekutana nao wana
hulka ya kirafiki na uungwana sana. Ni watu wenye tabia njema na ninahisi nitafurahia sana maisha yangu kwenu. Nitafurahia kwa sababu wenzangu walioshaishi Tanzania muda mrefu wamebakia na mapenzi makubwa ambayo sijayaona kwa Waingereza walioishi nchi nyingine. Wamebakia na kumbukumbu nzuri na mahusiano ya muda mrefu na Tanzania.”

Balozi aliendelea kufafanua kwamba Tanzania inasonga mbele na ni taifa muhimu kwa Uingereza ambaye ni mwekezaji wake mkuu.
“Wakati Balozi Diane Corner aliyenitangulia, alipokutana na Rais Kikwete , Rais alihimiza kwamba mahusiano ya serikali zetu mbili yamefikia mapatano ya juu sana. Hivyo jukumu langu litakua kuimarisha muungano huu.”

Balozi Diane Corner aliyeshika kiti hicho toka 2009 hadi 2013 amehamishiwa Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo.
Hafla hii ndogo pia ilihudhuriwa na Afisa Ubalozi wa daraja la pili, Allen Kuzilwa( anayehusika na mahusiano ya kimataifa ya ufadhili wa kimaendeleo na elimu ).
Balozi Melrose mwenye uzoefu mkubwa katika shughuli za ujenzi jamii na mahusiano ya kimataifa alikuwa balozi wa Uingereza nchini Cuba toka 2008 hadi 2012.

Mwanadiplomasia huyu ambaye ni mtaalamu wa lugha za Kifaransa na Kispanyola keshaanza kujifunza Kiswahili na alijaribu kuthibitisha maneno machache aliyoshayanyasua.
Akiwa kijana alifanya kazi shirika linalopambana na umaskini na kupigania haki duniani, Oxfam, mwaka 1980. Oxfam linalohudumia nchi 90 duniani lilianzishwa Uingereza mwaka 1942 mjini Oxford.Melrose alizaliwa Zimbabwe mwaka 1952 akamaliza masomo ya shahada ya kwanza ya lugha- kwa alama za juu (Honours) chuo kikuu cha Kings College, London. Akimkaribisha, Mheshimiwa Balozi Kallaghe alikumbusha kwamba kwenda Tanzania itakuwa changamoto kubwa maana taifa letu linapitia mabadiliko makubwa hasa kutoka kwa vijana, majadiliano ya katiba mpya na hali ya Afrika yenye matukio muhimu sasa hivi.

Mabalozi wengine waliohudhuria ni waheshimiwa Ernest Rwamucyo (Rwanda), Nkwelle Ekaney (Cameroon), na balozi wa zamani Canada (aliyeshastaafu), Antony Carey na mkewe Claire. Vile vile mwakilishi wa Tanzania Standard Chartered Bank, Uingereza, Rweyunga Kazaura, wanachama wa Jumuiya ya Watanzania na Waingereza (BTS) Ron Fennel , mkewe Liz, mhariri wa jarida la Tanzanian Affairs, David Brewin na mfanya biashara wa Kitanzania London (Swift Freight) Bwana Abubakar Faraji.

JENGO LA PPF TOWER LATEKETEA KWA MOTO JIJINI DAR

Picha ya jengo la PPF ikionesha moshi mkubwa unaofuka kutoka kenye jengo hilo.Shukurani ya picha: A, rafiki wa M.C.na Subi
----
Taarifa zinasema kuwa,hitilafu ya umeme iliyotokea kwenye mitambo ya mawasiliano iliyopo katika chumba cha 11, kilichopo  juu, mwisho kabisa mwa jengo la minara ya PPF lililopo kwenye makutano ya Ohio/Garden Avenue, katikati ya jiji la Dar es Salaam ndiyo iliyosababisha moto asubuhi ya leo majira ya saa moja, na kusababisha jengo hilo ushika moto.

Imetaarifiwa kuwa walinzi  wa  jengo hilo  walishuhudia moshi mzito  ukitoka ndani ya  jengo hilo la ghorofa, ndipo walipotoa taarifa kwa vikosi vya zima-moto.

Kikosi cha uokozi kilifika kwa wakati katika eneo husika na pamoja na kuweko nyenzo katika jengo hilo za kukwea hadi ghorofa ya kumi na moja, ufupi wa mipira ya zima-moto ili kufikisha maji kwenye chumba kinachowaka moto ulikwamisha jitihada za kuuzima moto huo.
 Hata na hivyo, juhudi zilizofanywa na kikosi hicho zimefanikiwa kuuzima moto huo  kabisa mnamo mwendo wa saa tano kasoro za adhuhuri.

Polisi wapo katika eneo hilo ili kulinda mali zisiporwe au kuharibiwa na vibaka.

Hakuna madhara yoyote ya moja kwa moja kwa binadamu yaliyoripotiwa. Thamani ya hasara iliyosababishwa na moto huo nayo haijafahamika.

Saturday, 2 February 2013

NJIA TANO UNAZOWEZA KUFANYA ILI KUONGEZA MAPENZI/FURAHA KWENYE MAISHA YAKO


Leo nilikuwa nasoma research iliyofanywa na Dr(PhD) Brown ambaye pia ameandika kitabu kinaitwa "Gifts of imprefection" anyways, huyu Dr. alikuwa amekaribishwa kwenye kipindi cha Oprah katika OWN kuongelea kwa nini watu wengine wanakuwa na furaha ya maisha/kuishi na wengine wanakuwa wanyonge mara zote. Mara nyingi watu wanakwambia "ningekuwa na pesa nyingi, matatizo yangu yote yangeisha na hata nisingelalamika kuhusu maisha, ningekuwa mwenye furaha saa zote." Well, kama tunavyoona katika dunia hii, hata wenye pesa sana wanamatatizo tena labda kupita kiasi in a sense kwamba hawakai kwa amani na mengine mengi. Ila tusisahau wapo pia wenye hela zao na wanakaa tuu kwa amani pia ila ni wachache. 

Anyways, matokeo kutoka utafiti wa huyu Dr. ulimwonyesha kwamba; Watu wengi walioonyesha kufanikiwa katika maisha yao mfano ya kindoa/kimapenzi/kiurafiki, walionyesha kuwa wakiishi maisha yako "dedicated to the cause" yaani sio mguu mmoja ndani mmoja nje. Pia matokeo yalionyesha kwamba, watu kama hawa, wanawake haswa (Ila wapo hata wanaume ambao wakishaamua kujidedicated katika relationship zao ni wanafanya kweli), anyway, huyu Dr. alisema kwamba, watu wengi wanaofanikiwa katika maisha yao ya ndoa, na nikisema kufanikiwa namaanisha wanaishi kwa amani, upendo, na furaha na wenza wao ni kwasababu watu kama hao wameweza kujikubali (accepting themselves) na kukubali kwamba they are WORTH OF LOVE AND BELONGING. Huyu Dr. alingundua kwamba yaani watu ambao wameshajiaccept na kujua kwamba they can love and belong, it didn't matter what circumstance ya maisha waliyokuwa nayo wedha ni nzuri ama mbaya, watu wenye karactaristics za aina hii wanaweza kuishi maisha ya furaha sana. 
kuelezea kwa kifupi ni kwamba; mara nyingi watu tunaonaga kwamba, ndio tunajipenda na tuko worthy kupendwa na kuwapenda wengine lakini tunasikia kijipenda zaidi kama labda tungeongezwa cheo kazini ama labda kama tungepata gari zuri zaidi na tulilokuwa nalo kwa sasa, ama kama tungeongeza elimu lbada tungejipenda zaidi. Yaani a lot of times watu wanakuwa unhappy kwasababu binadamu ni mgumu kuridhika na alichonacho. Mara nyingi pia mambo yakutoridhika hutokana pia na kupenda kuonekana na watu kwamba wewe ndo uko juu ama mbele zaidi ya wengine ama kupenda kupewa sifa kila mara.
Mara nyingi unakuta watu kama hawa hawanafuraha moyoni ya kila mara kwamaana wanarely on whats next I can do so people can see me again and praise me.

Watu ambao wanaweza kugundua walipokosea na kujikosoa wenyewe au kutokasirishwa wanapo kosolewa ni wachache of course lakini kwa mujibu wa huyu Dr. alichoweza kujifunza ni kwamba watu kama hawa ndo ambao waliweza kuonyesha kuishi maisha ya furaha zaidi. Yaani imani zao kuhusu maisha zimeweza kuwa ndo mwanga wa kila wanachokifanya kila siku wedha kitu wanachokifanya kinakuwa na mafanikio ama hapana bado wanaridhika na siku yao na kukubali kwamba kuna kesho I can do better. Watu kama hawa, hawajifichi wanapochapia ama mambo yanapokwenda ovyo ama wanapo aibishwa, wameshajifunza jinsi ya kudeal na matatizo kiasi cha kwamba wanajua jinsi ya kuface na huhandle most life's challenges na kuibuka imara.
Hivyobasi, hata sisi ambao bado we are working on kuridhika na maisha/becoming/being content with maisha there are a few things we can do ili kuweza kufikia stage kama hizi za walioridhika na wenye furaha katika moyo na maisha kiujumla.
  • Pointi ya kwanza ni kulet go of exhaustion - katika mihangaiko yako ya siku nzima make sure unaweka muda wa kupumzika. Kwa mfano; mara ngapi unajikuta umehangaikaa the whole day na huoni ulichokifanya lakini kama ungeupa mwili na akili nafasi ya kupumzika ungeweza kuisaidia akili kuwa na uwezo wa kufikiria vizuri na juu tena zaidi. Hivyo according to "Whole Hearted People advise" wanasema kwamba ili kuwa na mafanikio na kuweza kufikia kima cha kuwa content/kuridhika na maisha na kuweza kuwa na furaha; KNOW WHEN TO STOP AND REST!
  • Tafuta muda wa kufanya kitu unacho enjoy. Rudi na kuangalia ninini kipaji chako na jaribu kukiendeleza. Mfano; kushona, kufuma, kusoma vitabu, kuimba, gardening etc. sio lazima ufanye siku nzima lakini jipe muda wa kuweza kufanya vitu unavyo enjoy which a lot of times vinakuwa ni vipaji. Na hata wakati mwingine kuwa creative anzisha kitu chako mwenyewe.
  • Kuiacha roho/moyo/akili iwe tulivu (staying calm). Mara nyingi kama binadamu si rahisi kujiambia calm down and get a prompt response, hivyo basi ni muhimu kuchukua muda na kujituliza akili. Kuwa mrahisi wa kusikiliza na kujisikiliza zaidi badala ya kuongea wakati wote. Wanasema mara nyingi mtu ukiweza kustay calm, you can be able to hear what your mind and body is trying to tell you. Ila kwasababu we are so busy telling ourselves what to do all the time basi we shut down what really needs to speaks to us which is our soul.
  • Make room kucheza na familia yako, watoto wako, mume wako n.k. Huu ndo ule wakati wa kuangalia family shows together, kucheza board games (i.e. snake and ladder lol), karata ama hata kupiga hadithi ama kuangalia picha za zamani/utotoni na harusi and laugh, sali ama soma neno la Mungu pamoja na familia etc.

Kitu nilichogundua wakati nasoma na kumsikiliza huyu Dr. ni kwamba, sisi wataswahili tunapendaga kuwa serious sana na maisha and thats why saa nyingine yanatufrustrate. Wakati mwingine we need to let it loose and enjoy just simple things in life, i.e. kukaa na watoto wetu na kuchora funny pictures ama kufanya vitu tuu ambavyo vitakufanya ujione hauko katika element yako lakini at the same time you are enjoying doing it kwasababu you are feeling happy and good. Kumbuka LIFE IS TOO SHORT TO BE STRESSED OUT ALL THE TIME. ITS JUST NOT WORTH IT!!!

TUPE MAONI YAKO