Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps, Diresh Solanki akimpa tuzo msanii bora wa kiume katika tasnia ya filamu nchini Jacob Stevin JB wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudguliwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.Picha na www.burudan.blogspot.com |
Pazia ra Tuzo za Steps Bongo Movie Awards ukiwa umefunguliwa na waziri wa Sayansi na Teknolojia Makame Mbawala |
Mzee Majuto akipokea Tuzo ya msanii bora wa uchekeshaji |
Msanii Stiv Nyerere akipokea Tuzo |
Msanii Nice Mohamedi 'Mtunis' akipokea tuzo ya Mwaka 2012 zilizoandaliwa kwa mara ya kwanza na kampuni ya Steps Entatainment tuzo hizi zitakazokuwa
zikitolewa kila mwaka.Picha na www.burudan.blogspot.com
:KAMPUNI ya Usambazaji wa filamu ya
Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita
ilitoa tuzo kwa wasanii bora waliofanya vizuri katika tasnia ya filamu
nchini kwa mwaka 2012 ikiwa ni kwa mara ya kwanza kuanzishwa kwa tuzo
hizo
Akizungumzia tuzo hizo Mkurugenzi wa Kampunu hiyo Direshi Solanki amesema kuwa tuzo hizo watakuwa wakizitoa kila mwaka kwa kuleta maendeleo ya filamu nchini kampuni hiyo iliyojikita katika kusambaza filamu za wasanii wameweka historia ya kuigwa kutokana na kuanzisha tuzo hizo Baadhi ya washindi ambao walipatikana katika tuzo hizo wa kwanza ni Stevin Mangendela 'Stive Nyerere', Issa Mussa 'Cloud 112' Mohamed Nurdini 'Chek budi' Nice Mohamed 'Mtunisi' Iren Paul akinyakuwa msanii bora chipkizi wa kike Wakati katika kinyanganyiro cha kumpata msanii bora wa kiume alinyakuwa Jacob Stevin 'JB' huku msanii bora wa kike ikienda kwa mwana dada Iren Uwoya na msanii bora wa filamu za mapingano ilikwenda moja kwa moja kwa Jimmy Mponda 'Jimmy Masta' Wakati katika kipengere cha muhongozaji bora wa filamu kilikwenda kwa vicent Kigosi' Ray' na kampuni yake ya RJ Filamu mbali na hivyo kulikuwa na tuzo za heshima kwa wasanii waliofanya vizuri rakini kwa sasa awapo duniani moja ni kwa Stevin Kanumba,Saidi Kilowoko 'Sajuki' John Stefano,Hussein Ramadhani Mkiety,'Sharo Milionea' Katika utoaji wa tuzo huzo kulikua na burudani nyingi zikiongozwa na Odama Bendi |
No comments:
Post a Comment