Maadhimisho ya 17 ya wiki ya maziwa
nchini yamefungwa leo mjini SONGEA mkoani RUVUMA kwa kutolewa matumaini na Serikali
kuimalisha vituo vyake vya uhamilishaji wa ng’ombe wa maziwa vilivyopo mkaoni
ARUSHA, MWANZA na MBEYA ili kusambaza kwa wafugaji ng’ombe wa kisasa kuongeza
tija katika uzalishaji wa maziwa
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi DAKTA
EMMANUEL NCHIMBI akifunga maadhimisho ya wiki ya maziwa kwa niaba ya waziri wa mifugo
na uvuvi DAKTA MATHAYO DAVID, amesema serikali inalitambua tatizo la upungufu
wa ng’ombe wa maziwa na imeviimarisha vituo hivyo vya kanda vitakavyohudumia pia katika mikoa ya jirani
Naye KAIMU MSAJILI wa bodi ya maziwa
nchini DAKTA MAYASA SIMBA amesema maadhimisho ya mwaka huu yaamefana
ukilinganisha na miaka mingine kutokana na wanafunzi wa shule za msingi na
sekondari pamoja na wananchi wa kawaida kujitokeza kwa wingi
Wiki ya maziwa hapa SONGEA iliambatana
na maonyesho ya bidhaa za maziwa zilizosindikwa ambapo kampuni ya ASASI DAIRIES
ya IRINGA imejinyakulia ushindi wa jumla na meneja mauzo wa nyanda za juu
kusini wa kampuni hiyo JIMMY KIWELU amesema vionjo mbalimbali walivyoweka
kwenye bidhaa zao ndio zimevutia wateja wengi
Wadau wa baraza la maziwa wameadhimia
kutekeleza program ya unywaji maziwa mashuleni na wamekubaliana maadhimisho ya
mwaka kesho kufanyika mkoa wa MARA
Catherine Nyoni -RUVUMA
No comments:
Post a Comment