Monday, 10 June 2013

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma aikabidhi SACCOS ya waendesha piki piki Songea piki piki zenye thamani ya milioni kumi

 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akizungumza kabla ya kuwakabidhi piki piki tano viongozi wa SACCOS ya waendesha piki piki wa Manispaa ya Songea.
 Wanachama wa SACCOS ya waendesha piki piki wa Manispaa ya Songea wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.alipokuwa akitoa nasaha zake kabla ya kuwakabidhi piki piki
 Mkuu wa Mkoa Ruvuma Said Mwambungu akijaribu kuwasha moja ya piki piki alizozitoa kabla ya kukabidhi.
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma akijaribu kuendesha piki piki kabla ya kuwakabidhi viongozi wa SACCOS hiyo ya waendesha piki piki wa Manispaa ya Songea.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwanbungu akimkabidhi kadi za piki piki hizo Mwenyekiti wa umoja wa waendesha piki piki wa Manispaa ya Songea Shaban Kassimu.
 Mwenyekiti wa SACCOS ya waendesha piki piki wa Manispaa ya Songea Shaban Kassimu akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma baada ya kumkabidhi kadi na piki piki tano.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa SACCOS hiyo kushoto kwa aliyevaa suti ni Mkuu wa wilaya ya Tunduru Chande Nalicho, Mkuu wa mkoa Ruvuma Said Mwambungu
Viongozi wa SACCOS ya waendesha  Piki piki wakiondoka baada ya kukabidhiwa piki piki
------------------------------------------------------------------
Na Nathan Mtega,Songea
Mkuu wa  Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu amewakabidhi piki piki tano zenye thamani ya shilingi milioni kumi wanachama wa chama cha akiba na mikopo cha  waendesha piki ipiki wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ikiwa sehemu ya kuwafanya waendesha piki piki kuweza kujitegemeza na kumiliki piki piki zao badala ya kuendelea kutumiwa na wamiliki wa piki piki wanaofanya biashara ya kubeba abiria.

 Akizungumza kabla ya kuwakabidhi piki piki hizo mkuu wa mkoa amesema kuwa mara baada ya kufika mkoani Ruvuma alibaini kuwepo kwa waendesha piki piki wengi wanaofanya biashara ya kubeba abiria kwa kutumia piki piki ambazo haziwamiliki hali inayowafanya kuendelea kuwa wategemezi kwa wamiliki wa piki hizo.

Alisema kuwa aliamua kukutana na waendesha piki piki wote wa Manispaa ya Songea wapatao elfu tatu na kuwataka kuwa na umoja utakaowawezesha kuanzisha chama cha akiba na mikopo ili waweze kukopesheka kwa ajili ya kujiinua kiuchumi na kuweza kumiliki piki piki zao badala ya kutumiwa na wamiliki.

Aidha aliwataka baada ya kujiunga na kuanzisha chama cha akiba na mikopo wafunguwe akaunti benki ndipo yeye atatoa piki piki tano kwa ajili ya kuwawezesha kuanza kujitegemeza ahadi ambayo ameitekeleza kwa kuwakabidhi vionhozi wa chama hicho piki piki hizo huku akiahidi kuwapa piki piki nyingine muda wowote na kuwataka kuzintunza na kuzitumia kwa uangalifu kwa sababu  ni mali yao wenyewe tofauti na zile ambazo wamekuwa wakizitumia.

Amesema kuwa uongozi na wanachama wanapaswa kuweka mipango ya namna ya kuzitumia piki piki hizo ili ziweze kuzalisha piki piki nyingine kwa ajili ya wengine kwa sababu hizo ni kianzio cha wao kujitegemeza na amesema kuwa mpango huo wa kuanzishwa kwa vyama vya aikiba na mikopo kwa waendesha piki piki utaendelezwa kwa wilaya zote za mkoa wa Ruvuma.
Akimshukuru Mkuu wa mkoa  kwa niaba ya wanachama wa chama  hicho cha akiba na mikopo cha waendesha piki piki wa Manispaa ya Songea mwenyekiti wa chama hicho Shaban Kassimu alisema kuwa piki piki hizo zitawasaidia wanachama hao kuboresha maisha yao na kujikwamua kiuchumi  pamoja na kupunguza utegemezi uliokuwepo.

Alisema kuwa utawekwa utaratibu mzuri wa kuzitumia piki hizo ili ziweze kuzalisha na kuwakopesha wengine ambao watakuwa wamejiunga kwenye chama hicho pia zitawasaidia waendesha piki piki kuzingatia sheria za usalama bara barani kwa sababu ni mali yao wenyewe tofauti na ilivyokuwa awali hawakuwa na uchungu kwa sababu hazikuwa mali yao.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO