Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Magesa Mlongo akiwakaribisha Wajumbe kwenye
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Kujadili Utekelezaji wa Miradi ya Maji
Vijijini, jijini humo. wananchi
wa vijijini huduma ya maji kwa mwaka 2012/2013 na kuweka mikakati ya
kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji huo.
Waziri
wa Maji Prof. Jumanne Maghembe (Mb) akihutubia wajumbe (hawapo
pichani) kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu kwa ajili ya ufunguzi wa
Mkutano Mkuu wa kujadili Utekelezaji wa Miradi ya Maji Vijijini,
unaojadili utekelezaji wa kuwapatia
Waziri
Mkuu Mizengo K. P. Pinda akihutubia wajumbe (hawapo pichani) wakati
wa ufungunzi wa Mkutano Mkuu wa kujadili Utekelezaji wa Miradi ya Maji
Vijijini, Jijini Arusha unaojadili utekelezaji wa kuwapatia wananchi wa
vijijini huduma ya maji kwa mwaka 2012/2013 na kuweka mikakati ya
kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji huo.
Wajumbe
wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu Mhe. Mizengo K. P. Pinda hayupo
pichani wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa kujadili Utekelezaji wa
Miradi ya Maji Vijijini, Jijini Arusha unaojadili utekelezaji wa
kuwapatia wananchi wa vijijini huduma ya maji kwa mwaka 2012/2013 na
kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika
utekelezaji huo.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda amefungua Mkutano Mkuu wa Kujadili Utekelezaji wa
Miradi ya Maji Vijijini, jijini Arusha mwanzoni mwa wiki hii. Mkutano
huu unalenga kujadili changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa
programu katika mwaka 2012/2013 na namna ya kuzikabili changamoto hizo.
Akifungua
mkutano huo, Waziri Mkuu aliagiza Halmashauri zote kukamilisha ujenzi
wa miundombinu ya maji kwa vijiji 10 na ujenzi wa miradi ya maji
inayoleta matokeo ya haraka katika kipindi cha mwaka 2012/13 na 2013/14.
Waziri
Mkuu alisisitiza kuwa mwelekeo na malengo ya mkutano huu uwe ni kujenga
mkakati endelevu wa kutoa huduma ya maji kwa kuzingatia mahitaji ya
kiuchumi na kijamii hususan wananchi walioko vijijini kwa lengo la
kuwaondolea adha kubwa ya ukosefu wa maji.
“Hili
linawezekana kama kila mmoja wenu anatimiza wajibu wake kwa bidii,
maarifa, juhudi na nidhamu ya hali ya juu, nawakumbusha kuwa, jukumu
mlilopewa na taifa ni kubwa na muhimu sana.” Alisema Waziri Mkuu.
Waziri
wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua
Mkutano huo, aliwataka washiriki kutekeleza jukumu la kuwapatia wananchi
washio vijiji huduma ya maji kwa kutumia fedha zinazotolewa kwa ajili
ya kutekeleza miradi.
“Fedha
tunazopewa ni za wananchi, na ni lazima tuweze kueleza kila shilingi
iliyopokelewa imefanya kazi gani ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji”.
Alisisitiza Waziri Maghembe.
Mkutano
huu umeanza tarehe 3 hadi tarehe 7 Juni 2013, na mada mbalimbali
zitawasilishwa ikiwa ni pamoja na yaliyojitokeza katika ufuatiliaji wa
miradi ya maji nchini kwa mwaka 2012/2013, mpango wa utekelezaji wa
miradi ya maji kwa mwaka 2013/2014.
Nyingine
ni Utekelezaji wa Kampeini ya Kitaifa ya Usafi wa Mazingira,
yaliyojitokeza wakati wa kupitia Mfumo wa Kiteknolojia wa Kutoa Taarifa (MIS),
kila mkoa utatoa taarifa ya hali ya utekelezaji wa miradi ya maji
kwenye vijiji na miradi mingine ya maji, mfumo wa ufuatiliaji wa kikanda
na mapitio ya usanifu wa miradi ya maji.
Washiriki
wa mkutano huu wanajadili namna ya kuongeza kasi ya Utekelezaji wa
Mpango wa Mwaka 2013/2014 ikizingatiwa ni mwaka wa kwanza wa Utekelezaji
wa Mpango Mpya wa Kuleta Matokeo ya Haraka Sasa (Big Result Now). Ambapo baada ya majadiliano washiriki wataingia mkataba wa kiutendaji (Performance Agreement) kati ya Halmashauri na Mkoa na kati ya Mkoa na OWM – TAMISEMI.
Mkataba
huo utakuwa na majukumu ya kila mtekelezaji na hatua anayotakiwa
kufikia katika kipindi cha mwaka 2013/2014 kwa kufuata viashiria
vilivyowekwa kitaifa.
Mkutano
huu unahudhuriwa na Waheshimiwa Wabunge, Wawakilishi wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Wakurugenzi kutoka Wizara
mbalimbali zinazoshirikiana na Wizara ya Maji, Wataalam wa maji kutoka
Wizara ya Maji, Wataalam wa Maji kutoka Sekretarieti za Mkoa,
Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini, na Wahandisi wa Maji kutoka
Halmashauri. Pia, tumewashirikisha Wataalam kutoka katika sekta binafsi
ambao tunashirikiana nao katika kufikisha huduma ya maji kwa wananchi
waishio vijijini.
No comments:
Post a Comment