TUKIO
HILI LIMEFANYIKA JUMAMOSI YA JUNI 8, 2013 KATIKA WILAYA YA TAVETA, KAUNTI YA
TAITA-TAVETA, KATIKA MKOA WA PWANI.
BARAKA
WILLIAM MTANZANIA KUTOKA KLABU YA HOLILI ATHLETICS (HYAC) AKIMALIZA MBIO ZA
MITA 5000 NA KUIBUKA SHUJAA KWENYE MBIO NYINGINE ZA MITA 1500.
Katika
kuhakikisha
riadha nchini Tanzania inafuta uteja kwa wakimbiaji wake kwa wafukuza
upepo wa Kenya, Klabu ya Holili (HYAC) ya Mkoani Kilimanjaro
imedhihirisha hilo katika Taveta Athletics Championship kwa kuwabwaga
Wakenya katika mbio za meta 5000, 1500, 800 na 100.
Michuano
hiyo
ya Taveta imefanyika mwishoni mwa wiki katika Kaunti ya Taita-Taveta
katika Mkoa wa Pwani nchini Kenya katika wilaya ya Taveta kwa
kuwakutanisha wanariadha wa nchini Kenya huku Holili Youth Athletics
Club ikialikwa kutoka nchini Tanzania.
Katika
Mbio
za meta 5,000 alikuwa ni Baraka Williams aliyekimbia kwa dakika
14:45:22 nafasi ya pili ikishikwa na Mtanzania mwingine Abubakar
Joel aliyekimbia kwa muda wa 16:00:00 na nafasi ya tatu ikashikwa
na Mkenya Kivoko Makao ambaye alikimbia kwa muda wa 16:34:00.
Wambura
Lameck,
Mtanzania kutoka katika klabu ya Riadha kwa vijana (HYAC) alionyesha
uwezo katika mbio za meta 100 na 800 kwa wanaume; katika mbio za meta
100 Wambura alikimbia kwa muda wa sekunde 12:67 akiwatupa Wakenya Walter
Kamujalo (13:12), Emmanuel Paulo (13:70) na Joseph
Daudi (14:20).
Mbio
za mita 800 Wambura Lameck alikimbikia kwa muda wa dakika 2:02:16 akimwacha
Mkenya Ropya Nyingi ambaye alichukua muda wa dakika 2:04::14 na nafasi ya Tatu
ikishikwa na Mtanzania kutoka HYAC Paulo Jackson aliyekimbia kwa muda wa dakika
2:05:98, Wakenya wengine Joseph Daudi (3:00:00) na Philip Matheka (3:04) walishika
nafasi mbili za mwisho.
Pia Watanzania waliwaonyesha kazi nyingine Wakenya katika mbio za meta 1500 pale Baraka Williams kutoka HYAC alipowakimbiza na kuongoza baada ya kumaliza kwa muda wa dakika 3:48:77 akifuatiwa na Mkenya Vicent Daniel kutoka Taveta aliyemaliza kwa kutumia muda wa dakika 4:16:85 nafasi ya tatu ikishikwa na Mtanzania mwingine kutoka HYAC Paulo Jackson ambaye alikimbia kwa dakika 5:04:66 na Mkenya Tumuna Ludovick akikimbia kwa muda wa dakika 5:09:07.
Pia Watanzania waliwaonyesha kazi nyingine Wakenya katika mbio za meta 1500 pale Baraka Williams kutoka HYAC alipowakimbiza na kuongoza baada ya kumaliza kwa muda wa dakika 3:48:77 akifuatiwa na Mkenya Vicent Daniel kutoka Taveta aliyemaliza kwa kutumia muda wa dakika 4:16:85 nafasi ya tatu ikishikwa na Mtanzania mwingine kutoka HYAC Paulo Jackson ambaye alikimbia kwa dakika 5:04:66 na Mkenya Tumuna Ludovick akikimbia kwa muda wa dakika 5:09:07.
Kwa
upande wa wanawake Watanzania Furaha Sambeke na Pendo Pamba walifanya kweli katika meta 800 kwa kushika nafasi mbili za juu.
Furaha
Sambeke anayenolewa na Klabu ya Holili Youth Athletics
alikimbia kwa muda wa dakika 2:30:00 na Pendo Pamba akimaliza kwa
dakika 3:10, nafasi ya tatu ilishikwa na Mkenya Emily Wamboi na ya nne
ikishikwa na Mkenya mwingine Cecily Kimale ambao wote walikimbia kwa
muda wa dakika 3:22:00 na 4:12:00.
Akizungumzia
ushindi huo Katibu wa klabu ya Holili Youth atletics, Innocent Mlashane,
wapongeza wanariadha hao kwa ushindi mkubwa
waliouonesha kutoka kwa wapinzani wao na kuahidi kuwa kamwe hawatarudi nyuma.
“Changamoto
tuliyonayo kubwa ni kupata wafadhili hasa wa kuweza kuwahudumia wachezaji wetu
ambao kwa sasa wako katika kambi ya Tarakea, na mchezo waliocheza hapa taveta
inaonesha kuwa tuna wachezaji wazuri hivyo tukipata msaada zai naamini
tutasonga mbele zaidi” alisema
Alisema klabu ya holili imedhamiria kurudisha heshima ya Tanzania kwa nguvu zote hasa katika mchezo wa riadha ambao kwa serikali wameonesha kuusahau.
Alisema klabu ya holili imedhamiria kurudisha heshima ya Tanzania kwa nguvu zote hasa katika mchezo wa riadha ambao kwa serikali wameonesha kuusahau.
Taveta
Athletics
Championship imefanyika ikiwa na makusudi ya kutengeneza Timu ya Riadha
ya Taifa la Kenya ambako mchujo rasmi utafanyika Mjini Mombasa kwa
watanzania walioshinda katika mbio hizo nao watakuwemo katika
kinyang’anyiro hicho kwa ajili ya kupata uzoefu zaidi kutokana na ukweli
kwamba taifa la Kenya limekuwa bora katika riadha barani Afrika.
Mwandishi:
JOHNSON JABIR, Moshi-Kilimanjaro
No comments:
Post a Comment