Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akifungua mkutano wa Shirika la Hifadhi za Mbuga za Taifa TANAPA na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu Wajibu wa vyombo vya habari katika kukabiliana na Ujangili katika hifadhi za taifa unaofanyika kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo Ofisi za Manispaa ya Iringa, Balozi Kagasheki amewaasa wahariri wa vyombo vya habari kujadiliana kwa undani suala zima la kukomesha ujangili na jukumu la wanahabari katika mkakati huo wakishirikiana na serikali kwa ujumla kupitia taasisi za ulinzi katika mbuga za wanyama, amewataka wahariri kuwa wabunifu kwa kuandika makala na habari za kiuchunguzi ili kuibua mbinu hizo chafu na majangili ili kutokomeza ujangili huo na kupata ufumbuzi kamili wa changamoto hizo za ujangili, ameongeza kwamba wizara yake iko tayari kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wahariri na wadau mbalimbali yatakayofanikisha kupata ufumbuzi wa kutokomeza kabisa ujangili katika mbuga na pia amejiwekea utaratibu wa kukutana na waandishi wa habari kila mwezi atakutana na vyombo vya habari ili kuzungumza na wanahabari kuhusu masuala mbalimbali ya wizara hiyo.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE- IRINGA
Wahariri mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki wakati akifungua mkutano huo.
Wahariri
wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa makini katika kusikiliza wakati
Waziri Balozi Khamis Kagasheki akizungumza katika mkutano huo.
Balozi Khamis Kagasheki akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano huo kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo mjini Iringa
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma akizungumza katika mkutano
huo wakati akimkaribisha Waziri wa Malisiali na Utalii Mh. Balozi Khamis
Kagasheki.
Waziri wa Malisili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akiongozana na
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma wakati akiwasili katika
ukumbi wa mikutano wa Siasa na Kilimo mkoani Iringa ambako mkutano wa
Wahariri wa vyombo vya habari na Shirika la Hifadhi za mbuga za Taifa
TANAPA unafanyika. Mwenyekiti
wa Kamati ya kudumu ya bunge ya Ardhi Mazingira Ndugu James Lembeli
akiingia kwenye ukumbi wa mkutano huku akiwa ameongozana na Mkurugenzi
wa TANAPA Ndugu Allan Kijazi kushoto.
Waziri
wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki wa pili kutoka kulia
akiwa katika mkutano huo kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi
na Mazingira Ndugu James Lembeli na kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa
TANAPA Ndugu Allan Kijazi na Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine
Ishengoma.
Waziri
wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki katikati akiwa katika
mkutano huo kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya Ardhi na Mazingira
Ndugu James Lembeli na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine
Ishengoma
Waziri
Kivuli wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mbunge wa Iringa mjini
Mchungaji Peter Msigwa akizungumza katika mkutano huo huku Waziri wa
Maliasili Balozi Khamis Kagasheki wa pili kutoka kushoto akisikiliza,
wengine ni Ndugu James Lembeli Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi na
Mazingira na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma. Mwenyekiti
wa Kamati ya bunge ya Ardhi na Mazingira Ndugu James Lembeli
akizungumza katika mkutano huo huku waziri wa Maliasili na Utalii Balozi
Khamis Kagasheki akisikiliza kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr.
Christine Ishengoma. Mkurugenzi
wa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akizungumza katika mkutano huo kukaribisha
wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano huo unafofanyika kwenye ukumbi
wa Siasa na Kilimo mjini Iringa
No comments:
Post a Comment