Mwenyekiti
wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw.
Ridhiwan Kikwete akifungua mkutano mkuu wa chama cha waandishi wa
habari za michezo TASWA unaofanyika kwenye Hoteli ya Kiromo View
Bagamoyo mkoani Pwani ambao unajadili mambo mbalimbali ya Maendeleo na
changamoto zinazokabili chama hicho.
Waanishi wa habari za michezo ambao ni wanachama kutoka vyombo mbalimbali nchini wanahudhuria mkutano huo ambao ni wa siku moja.
Mwenyekiti
wa Chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA Bw. Juma Pinto
akimkaribisha mgeni rasmi ili kufungua mkutano huo leo asubuhi
unaofanyika kwenye hoteli ya Kiromo View Bagamoyo.
Katibu
wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo TASWA Bw. Amir Mhando
akizungumza katika mkutano huo, kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa
TASWA Maulid Kitenge, Mwenyekiti Juma Pinto, Mgeni rasmi Ridhiwan
Kikwete na kushoto ni George John Katibu Msaidizi.
Mtaalam
wa SACCOS kutoka Manispaa ya Ilala Bw. Luambano akitoa mada kuweka na
kukopa kwa waandishi wa habari wanachama wa TASWA waliohudhuria katika
mkutano huo
Kutoka
kulia ni waandishi wakongwe Mwina Kaduguda, Mzee Wlly Chiwango na Mzee
Salim Said Salim kutoka Zanzibar wakiwa katika mkutano huo.
Kutoka kulia ni Shafii Dauda, Erasto na Ibrahim Masoud wakiwa katika mkutano huo.
Kutoka kulia ni Elizaberth Mayemba , Timzo Kalugira na Crala Alphonce wakifuatilia mada katika mkutano huo.
Kutoka kushoto ni Elius Kambili, Alfred Lucas na Salum Jaba wajumbe wa kamati ya utendaji ya TASWA wakiwa katika mkutano huo.
Kutoka kulia ni Mgaya Kingoba, Salum Jaba, Richard Mwaikenda na Tulo Chambo wakifuatilia mada katika mkutano huo.
Wajumbe
mbalimbali wakihudhuria mkutano wa Chama cha Waandishi wa habari za
michezo TASWA kwenye hoteli ya Kiromo View mjini nje kidogo ya mji wa
Bagamoyo mkoani Pwani .