Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar
wakiwa wanasubiria Kuingia ndani ya ofisi ya Star Times Mwenge kutokana
na wateja kujaa ndani ya ofisi hiyo kwaajili ya kununua ving'amuzi na
kupelekea wateja hao kuingia kwa kusubiriana. Ikumbukwe kuwa mnamo
tarehe 23 februari 2012 Wizara ya Sayansi na Teknolojia kupitia Mamlaka
ya Mawasiliano nchini TCRA ilitangaza kusitisha urushaji wa matangazo
ya televisheni kwa kutumia teknolojia ya analojia kwenda katika mfumo
mpya wa digitali kufikia tarehe 31 Disemba 2012 saa sita na dakika moja
usiku
Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar
wakiwa wamekaa nje ya ofisi ya Star Time Mwenge wakisubiria wateja
wengine waliopo ndani wapungue ili na wao waweze kuingia na kununua
ving'amuzi vya kampuni hiyo.
Kijana akitoka kununua king'amuzi cha Kampuni ya Star Times tayari kwa kupokea matangazo ya televisheni kwa njia ya digitali
Mkazi
wa Jiji la Dar akiwa tayari kashajinunulia king'amuzi cha Kampuni ya
Star Time tayari kwa kupokea matangazo kwa njia ya digitali ambapo
Tanzania inaingia kwenye mfumo mpya wa urushaji wa matangazo ya
televisheni kupitia mfumo wa digitali. Kufikia saa sita na dakika moja
usiku wa leo Serikali imeagiza wamiliki wote wa vituo vya televisheni
kuzima mitambo yao inayotumia teknolojia ya analojia na kuwasha mitambo
mipya inayotumia teknolojia ya Digitali.
No comments:
Post a Comment